settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna malaika wa kifo?

Jibu


Dhana ya "malaika wa kifo" iko katika dini kadhaa. "Malaika wa kifo" anajulikana kama Samaeli, Sarieli, au Azrael katika Uyahudi; kama Malaki Almawt katika Uislam; kama Yama au Yamaraj katika Uhindu; na kama vile muuaji mkuu katika sayansi bunifu. Katika hadithi nyingi, malaika wa kifo anachukuliwa kuwa kama kitu chochote kutoka kwa takwimu ya mifupa iliyo na mviringo, hadi mwanamke mrembo, na hata mtoto mdogo. Wakati maelezo yanapofautiana, imani kuu ni kwamba kiumbe mfano wa mtu humjia mtu wakati wa kifo, au kwa kweli husababisha kifo au huangalia tu-kwa lengo la kisha kuchukua nafsi ya mtu kwenye makaazi ya wafu.

Dhana hii "malaika wa kifo" haifundishwi katika Biblia. Haman mahali Biblia inafundisha kwamba kuna malaika fulani ambaye anahusika na kifo au ambaye yupo wakati wowote mtu akifa. Wafalme wa pili 19:35 inaelezea malaika aliyeuawa Waashuri 185,000 waliokuwa wamevamia Israeli. Wengine pia wanaona Kutoka sura ya 12, kifo cha kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, kama kazi ya malaika. Huku kukiwa na uwezekano, hamana mahali Biblia inalimbikizia malaika kifo chochote cha wazaliwa wa kwanza ya kifo cha mzaliwa wa kwanza kwa malaika. Kwa hali yoyote, wakati Biblia inaelezea malaika kifo cha wa kwanza. Njia yoyote ile, huku Biblia ikielezea malaika wanaosababisha kifo kwa amri ya Bwana, hakuna mahali popote Maandiko yanafundisha kwamba kuna malaika maalum wa kifo.

Mungu, na Mungu peke yake, ndiye mkuu juu ya wakati wa mauti yetu. Hakuna malaika wala pepo anayeweza kusababisha kifo hata kimoja kabla ya wakati Mungu amenuia kitokee. Kwa mujibu wa Warumi 6:23 na Ufunuo 20: 11-15, kifo ni utengano, kutenganisha nafsi yetu ya roho kutoka kwa mwili wetu (kifo cha kimwili) na, kwa ajili ya wasioamini, kutengana milele na Mungu (kifo cha milele). Kifo ni kitu hutokea. Kifo si malaika, pepo, mtu, au mtu mwingine yeyote. Malaika anaweza kusababisha kifo, na anaweza kuhusika katika kile kinachotokea kwetu baada ya kifo-lakini hakuna kitu kama "malaika wa kifo."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna malaika wa kifo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries