settings icon
share icon
Swali

Ni nani Mikaeli malaika mkuu?

Jibu


Mikaeli malaika mkuu anaelezewa katika Biblia, katika vitabu vya Danieli, Yuda, na Ufunuo, kama malaika shujaa ambaye anahusika katika mapambano ya kiroho. Neno malaika mkuu linamaanisha "Malaika wa cheo cha juu zaidi." Malaika wengi katika Biblia wanaonyeshwa kama wajumbe, lakini Mikaeli ameelezewa katika vitabu vyote vitatu kama kushindana, kupigana, au kusimama dhidi ya pepo na himaya ya mwana mfalme (Danieli 10:13; 21; Yuda 1:9; Ufunuo 12:7). Hatuna picha kamili ya malaika yeyote, na ni wawili tu wametajwa katika Biblia (Gabrieli ni mwingine). Maandiko hutupa tu dokezo ya harakati zao wakati wa matukio ya kibinadamu, lakini ni salama kusema kwamba Mikaeli malaika mkuu ni kiumbe chenye nguvu.

Licha ya uwezo wake mkubwa, Mikaeli bado anajisalimisha kabisa kwa Bwana. Utegemezi wake juu ya nguvu za Bwana huonekana katika Yuda 1:9. Malaika wenye haki wana cheo na wanajisalimisha kwa mamlaka, na kwa sababu hiyo hutumiwa kama picha ya utii wa mke kwa mumewe (1 Wakorintho 11:10). Kuzingatia nguvu ya Mikaeli malaika mkuu, utii wake kwa Mungu ndio rembo zaidi. Ikiwa utii wa malaika ni hoja ya utii wa mwanamke, tunaweza kuona kuwa usalimishaji haukumaanisha kamwe kuondoa nguvu za mwanamke au madhumuni au thamani.

Nabii Danieli ameambiwa kwamba Mikaeli malaika mkuu ni "jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako" (Danieli 12:1). Watu wa Danieli ni Wayahudi, na ukweli kwamba Mikaeli "anawalinda" wao kunaonyesha kwamba Mungu ameweka malaika mbalimbali watakatifu juu ya nchi mbalimbali au makundi ya watu. Mapepo yanaonekana kuwa na mfumo wa mamlka sawa (angalia Danieli 10:20). Ukweli kwamba Mikaeli ni "mfalme mkuu" inaonyesha kwamba ana mamlaka katika ulimwengu wa kiroho. Kuna wengine-Danieli 10:13 inasema kwamba Mikaeli ni "mmoja wa hao wakuu wa mbele."

Mikaeli malaika mkuu ana, inaonekana, jukumu maarufu katika matukio ya nyakati za mwisho. Danieli aliambiwa na malaika wa Bwana kwamba, wakati wa mwisho, Mikaeli "atainuka" na kutakuwa na wakati wa shida zisizozidika-kutaja Dhiki Kuu (Danieli 12:1). Israeli inahakikishiwa ulinzi wakati huu, ambao utafuatiwa na ufufuo mkubwa wa wafu — baadhi kwa uzima wa milele na wengine kwa aibu ya milele (Danieli 12:2). Unyakuo wa kanisa utaambatana na "sauti ya malaika mkuu" (1 Wathesalonike 4:16); hii inaweza kuwa kumbukumbu ya Mikaeli, lakini Maandiko hayamtaji bayana hapa.

Kutajwa kwa mwisho kwa Mikaeli malaika mkuu inaonekana katika Ufunuo 12:7. Wakati wa dhiki, "kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, na yule joka akapigana nao pamoja na malaika zake." Mikaeli na majeshi ya mbinguni wanashinda joka (Shetani), na Ibilisi akatupwa duniani. Huko,ghadhabishwa, Shetani "akaenda zake afanye vita dhidi. . . wale wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu "(Ufunuo 12:17).

Kuna vita vya kiroho vinavyopigana juu ya mioyo na nafsi ya mwanadamu. Mikaeli malaika mkuu ni mkuu wa malaika mwenye nguvu ambaye analinda Israeli na kumtumikia Mungu kwa utii kwa kufanya vita dhidi ya Shetani. Ibilisi anaweza kufanya mbaya zaidi, lakini "hana nguvu ya kutosha" kushinda majeshi ya mbinguni (Ufunuo 12:8).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nani Mikaeli malaika mkuu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries