settings icon
share icon
Swali

Je, kuna malaika kati kati yetu?

Jibu


Katika Maandiko, tunaona matukio mengi ambayo malaika walikuwa sehemu muhimu ya mpango wa Mungu. Mstari mmoja unaonyesha uwezekano wa malaika kutembea miongoni mwetu hii leo: "Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua" (Waebrania 13: 2). Kumbukumbu dhahiri ni kwa Ibrahimu, ambaye malaika wake alimtokea kama wanaume (Mwanzo 18). Aya hii inaweza au isiweze kuthibitisha kwamba malaika kwa kweli hutembea kati kati yetu bila kujua; "Imeonyesha" ni wakati uliopita, hivyo kukutana na malaika wakati wetu siku hizi ni jambo halijatajwa wazi wazi.

Kuna mifano kadhaa ya maandiko ya kukutana na malaika, kwa hiyo tunajua kwamba Mungu anaweza kutumia malaika kutekeleza mambo fulani. Chenye hatujui kwa uhakika ni mara ngapi malaika wanajiruhusu kuonekana na watu. Hapa kuna ya misingi kuhusu malaika kutoka kwa Biblia: Malaika anaweza kuwafundisha watu (Mwanzo 16: 9), kuwasaidia watu (Danieli 6:22), kutoa ujumbe kwa watu (Luka 1:35), kuonekana katika maono na ndoto (Danieli 10: 13), kulinda watu (Kutoka 23:20), na kusaidia kufanya mipango ya Mungu.

Tunajua kwamba Mungu aliumba malaika, na anatumia malaika katika mpango Wake. Malaika wana ufahamu wa kibinafsi, na vile vile wengine wana majina (kama vile Gabriel na Michael) na wote wana majukumu tofauti ndani ya utawala wa malaika.

Lakini wao hutembea kati kati yetu? Ikiwa Mungu huchagua kuwatumia katika mipango Yake iliyowekwa kwa desturi yetu, ndiyo, wanaweza kabisa kutembea kati yetu kufanya mapenzi ya Mungu. Malaika hutajwa katika Mwanzo na katika Ufunuo na kulishuhudia uumbaji wa ulimwengu (Ayubu 38: 7). Mungu ametumia jeshi lake la mbinguni tangu mwanzo wa wakati na bado atawatumia wakati wa mwisho, kulingana na Maandiko. Inawezekana kwamba watu wengi hii leo wamekutana au onana na malaika bila kutambua.

Ikiwa malaika hutembea kati yetu, ni kwa sababu wanahudumia kusudi la Mungu lililowekwa. Biblia inataja mapepo wanaotembea dunia bila kusudi ila tu kuharibu (Mathayo 12: 43-45). Shetani na nguvu zake za pepo zinaweza kuonekana kimwili, kama vile malaika watakatifu wanaweza. Kusudi la Shetani ni kudanganya na kuua. Shetani "anajifanya kama malaika wa nuru" (2 Wakorintho 11:14).

La muhimu kumbuka: Malaika hawatakiwi kuinuliwa au kuabudiwa (Wakolosai 2:18). Wao ni vyombo vinavyofanya mapenzi ya Mungu, na wanajiita wenyewe kama "watumishi wenza" pamoja nasi (Ufunuo 22: 9).

Bila kujali kama tunapata uzoefu wa malaika, jambo muhimu zaidi ni kwamba tunapata wokovu kupitia Yesu Kristo. Yeye you zaidi ya malaika wote na wanadamu wote, na Yeye peke yake anastahili kuabudiwa. "Wewe ndiwe Bwana, wewe peke yako; wewe ulifanya mbingu, mbingu za mbingu, pamoja na jeshi lake lote, dunia na vyote vilivyomo, bahari na vitu vyote vilivyomo, nawe unavihifadhi vitu hivi vyote; na jeshi la mbinguni lakusujudu wewe" (Nehemia 9: 6)

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna malaika kati kati yetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries