settings icon
share icon
Swali

Je, malaika huwaonekania na watu hii leo?

Jibu


Katika Biblia malaika huwaonekania watu katika njia zisizotarajiwa na mbalimbali. Kutokana na kusoma kwa juu juu kwa Maandiko, mtu anaweza kupata wazo kwamba kuonekana kwa malaika kulikuwa kwa kawaida, lakini sivyo. Kuna ongezeko kubwa zaidi kwa malaika kuonekania hii leo, na kuna ripoti nyingi za malaika kuonekania. Malaika ni sehemu ya karibu kwa kila dini na kwa ujumla wanaonekana kuwa na jukumu lile la mjumbe. Ili kujua kama malaika huonekania watu hii leo, lazima kwanza tuone mtazamo wa kibiblia jinzi walivyoonekania hapo hawali.

mara ya kwanza malaika Kuonekania katika Biblia ni katika Mwanzo 3:24, wakati Adamu na Hawa walifukuzwa kutoka bustani ya Edeni. Mungu akaweka makerubi kuzuia mlango kwa upanga wa moto. Kuonekana kwa malaika kwingine ni katika Mwanzo 16: 7, karibu miaka 1,900 baadaye. Hagari, mtumishi wa Misri ambaye alimzaa Ishmaeli kwa Ibrahimu, aliamriwa na malaika kurudi na kunyenyekea kwa bibi yake, Sarai. Ibrahimu alitembelewa na Mungu na malaika wawili katika Mwanzo 18: 2, wakati Mungu alimwambia kuhusu uharibifu uliokua unaikujia Sodoma na Gomora. Malaika wale wawili walimtembelea Loti na kumwambia kuuepuka mji na familia yake kabla ya uharibifu (Mwanzo 19: 1-11). Malaika katika hali hii pia walionyesha nguvu isiyo ya kawaida kwa kuwapofusha watu waovu ambao walikuwa wanatishia Loti.

Yakobo alipoona wingi la malaika (Mwanzo 32: 1), mara hiyo hiyo aliwatambua kama jeshi la Mungu. Katika Hesabu 22:22, malaika alimwambia Balaamu nabii aliyeasi, lakini Balaamu hakumwona malaika mara ya kwanza, ingawa punda wake alimwona. Maria alipata kutembelewa na malaika ambaye alimwambia kuwa angekuwa mama wa Masihi, na Yosefu alionywa na malaika kumchukua Maria na Yesu kwenda Misri ili kuwahifadhi kutoka kwa amri ya Herode (Mathayo 2:13). Wakati malaika wanapoonekana, wale wanaowaona mara nyingi hupatwa na hofu (Waamuzi 6:22; 1 Mambo ya Nyakati 21:30; Mathayo 28: 5). Malaika huleta ujumbe kutoka kwa Mungu na kufanya mapenzi Yake, wakati mwingine kwa njia za kawaida. Katika kila hali, malaika huwaelekeza watu kwa Mungu na kumpa Mungu utukufu. Malaika watakatifu hukataa kuabudiwa (Ufunuo 22: 8-9).

Kulingana na ripoti za kisasa, kuonekaniwa na malaika kunakuja kwa aina mbalimbali. Katika baadhi ya matukio, mgeni huzuia madhara makubwa au kifo na kisha hupotea kwa siri. Katika matukio mengine, malaika mwenye mabawa au amevaa kanzu nyeupe huonekana kwa muda mfupi na kisha kutoweka. Mtu ambaye anaona malaika mara nyingi huachwa na hisia ya amani na uhakika wa kuwepo kwa Mungu. Aina hii ya kutembelewa inaonekana kukubaliana na mfano wa kibiblia kama inavyoonekana katika Matendo 27:23.

Aina nyingine ya mwonekanio ambao mara nyingine huripotiwa leo ni aina ya "malaika waimbaji". Katika Luka 2:13, wachungaji walitembelewa na malaika waimbaji wa mbinguni kama walipoambiwa juu ya kuzaliwa kwa Yesu. Watu wengine wamesema uzoefu kama huo katika maeneo ya ibada. Uzoefu huu hauhusiani na mfano huo vizuri, kwa kawa hauna kusudi lolote isipokuwa kutoa hisia ya viungo vya kiroho. Ujumbe wa malaika katika Injili ya Luka alikuwa akielezea habari maalum.

Aina ya tatu ya kuonekaniwa inahusisha hisia tu za kimwili. Watu wazee wamewahi kusikia hisia kama mikono au mabawa imewakumbatia wakati wa upweke sana. Mungu kwa hakika ni Mungu wa faraja yote, na Maandiko yanazungumzia Mungu akifunika kwa mabawa yake (Zaburi 91: 4). Ripoti hiyo inaweza kuwa baadhi ya mifano hiyo.

Mungu bado anafanya kazi ulimwenguni kama alivyokuwa akifanya, na malaika wake hakika bado wanafanya kazi. Kama vile malaika waliwalinda watu wa Mungu katika siku za mbeleni, tunaweza kuwa nau hakika kwamba wanatuhifadhi hii leo. Waebrania 13: 2 inasema, "Msisahau kuwakaribisha wageni; maan kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua." Tunapotii amri za Mungu, inawezekana tuweze kukutana na malaika Wake, hata kama hatujui. Katika hali maalum, Mungu aliwaruhusu watu Wake kuona Malaika Wake wasioonekana, ili watu wa Mungu watiwe moyo na kuendelea katika huduma yake (2 Wafalme 6: 16-17).

Lazima pia tutii maonyo ya Maandiko juu ya malaika viumbe: kuna malaika walioanguka wanaofanya kazi kwa ajili ya Shetani ambao watafanya chochote ili kutuzuia na kutuangamiza. Wagalatia 1: 8 inatuonya tujihadhari na injili yoyote "mpya", hata kama inaletwa na malaika. Wakolosai 2:18 inaonya kuhusu kuabudu malaika. Kila wakati katika Biblia wakati watu walipiga magoti mbele ya malaika, viumbe hao walikataa kuabudiwa. Malaika yeyote anayepokea ibada, au asiyemtukuza Bwana Yesu, ni mpumbavu. Wa 2 Wakorintho 11: 14-15 inasema kwamba Shetani na malaika wake wanajificha wenyewe kama malaika wa nuru ili kudanganya na kumpoteza yeyote atakayewasikiliza.

Tunahimizwa na fahamu kwamba malaika wa Mungu wanafanya kazi. Katika hali maalum, tunaweza hata kuwa na moja ya ziara hizo za kawaida. Kubwa kuliko fahamu huo, hata hivyo, ni fahamu kwamba Yesu mwenyewe amesema, "Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati" (Mathayo 28:20). Yesu, ambaye aliwaumba malaika na anapokea sala zao, ametuahidi uwepo wake mwenyewe katika majaribu yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, malaika huwaonekania na watu hii leo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries