settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa kutakuwa na kristo wa uongo katika nyakati za mwisho?

Jibu


kristo au masihi wa uongo ni mnafiki anayedai kuwa yule ambaye ametumwa na Mungu kuwaokoa wanadamu. Katika Mathayo 24:23-24, Yesu anasema, “Wakati huo kama mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa!’ Au, ‘Kristo yuko kule,’ msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara kubwa na maajabu mengi ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule hasa”. Hii ni sehemu mojawapo kubwa ya mafundisho kuhusu kile tunacho tarajia katika nyakati za mwisho. Katika Mathayo 24, Yesu anarudia fundisho hili, akiongezea, “Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokeavyo mashariki na kuonekana hata magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu” (aya za 26-27).

“Nyakati za mwisho” humaanisha mambo mengi katika Biblia. Kulingana na Waebrania 1:2, “siku za mwisho” katika Agano Jipya, zinaanza na kukuja kwa Yesu Kristo mara ya kwanza. Hii ndiyo maana katika Matendo 2:16-17, 1Yohana 2:18, na Petro 1:20. Kwa mjibu wa maana hii, tunaishi katika “nyakati za mwisho”; hivyo ni kusema kuwa tuko katika kipindi cha mwisho kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Katika Mathayo 13:49, “nyakati za mwisho” zinarejelea nyakati za hukumu ya ujio wa Bwana mara ya pili. Kurudi kwa Bwana na matukio yatakayotokea kabla ujio wake (ona Ufunuo 6-16) kwa kawaida hii leo hujulikana kama “nyakati za mwisho.” Ijapokuwa uhuenda “nyakati za mwisho” zilianza miaka 2,000 iliyopita, kutakuwa na ongezeko la ishara ambazo Yesu alitoa kuhusu ujio wake unavyo karibia. Tunaamini kuwa “nyakati za mwisho,” vile imeeleweka kwa ujumla zitaanza na unyakuzi wa kanisa.

Makristo wa uongo wamekuja na kwenda tangu karne ya kwanza (Marko 13:22; 2Petro 2:1). Wanatokea pindi mtu anadai kuwa yeye ni Masiha ama wakati bewa la Ukristo linapoondoka kwa mafundisho ya Neno la Mungu na kujaribu kumwelezea Yesu jinsi asivyo. Mitume walipingana na mafundisho ya uwongo katika nyingi za barua zao kwa makanisa, wakiwaonya waumini kuhusu makristo wa uwongo na manabii wa uwongo miongoni mwao (2 Wakorintho 11:13). Yohana alitoa ufafanuzi sahihi kuhusu Kristo: “Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu” (1 Yohana 4:2-3).

Makristo wa uwongo wameendelea kuonekana. Hata miongoni mwa karne iliyopita, watu kama Jim Jones, Sun Myung Moon, na David Koresh wameibuka na umaarufu kwa kudai kuwa wao ni Mungu au msaidizi wake wa karibu. Mara nyingi walianza na Biblia na wakashikilia mstari mmoja au wazo moja na kuunda theolojia yao, huku wakigeuza kundi lao kuwa dhehebu la kujithibitisha. Viongozi wa madhehebu mara nyingi huwavutia wahasiriwa wao kwa kujionyesha kuwa waumini wanaoiamini Biblia. Makundi kama ya waumini wakereketwa wa kanisa la msingi la watakatifu (Latter-day Saints church), kanisa la Kristo liaminilo sayansi, na Mashahidi wa Yehova wote wanadai kuwa Wakristo, lakini wote hukana uungu na kazi ya Yesu, Yesu si Mwana wa Mungu, na kuwa Yesu si njia pekee kwa msamaha na maisha ya milele (ona Yohana 14:6).

Karibu na jibu, kumeibuka ongezeko la makristo wa uwongo katika maeneo hawakutarajiwa: mimbari za makanisa ya Kikristo. Wakati mafundisho yanapo mpendekeza Kristo jinsi asivyo au kwa makusudi kudunisha ukweli wa injili Yake, basi lamdhihirisha kristo wa uwongo. Kwa mfano, mchipuko wa mafundisho ya neema kupita kiasi na mzingatio wa kuishi maisha ya ufanisi wa dunia hii, hupunguza utukufu wa Yesu Kristo kwa manufaa ya ibada ya kibinafsi. Katika visa kama hivyo, ikiwa Yesu atatajwa kamwe, mara nyingi anadhihirishwa kama kitu havifu sana cha kupokea baraka za Mungu. Katika kizazi hiki cha kusoma na akuandika biblia, wasikilizaji wengi humkumbatia Kristo anayependekezwa namna ya teleo hili, na kamwe hawathubutu kuswali kanuni ya dini ambayo imebadilishwa ambayo inakumbatia fundisho kama hili. Hata wakati watu wanapewa fursa ya “kufanya uamuzi” wa kumfuata yesu, mtu lazima ajiulize: ni kwa Kristo yupi waneyejikabidhi kwake?

Timotheo wa pili 4:3-4 ilituonya kwamba wakati utawadia ambapo watu hawatakumbatia mafundisho sahihi. Siku zinavyozidi kuwa ovu na dhambi kuongezeka, kristo anayependeza zaidi anakua vutio kwa wale “watapenda giza kuliko nuru” (Yohana 3:19). Wathesaloniki wa pili 2:11-12 inaelezea ni kwa nini watu wengi wanavutiwa na makristo wa uwongo. Aya ya 10 inasema, “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.” Wakati watu wanakataa kuipenda kweli, Yesu wa ukweli, au neno takatifu la Mungu, Mungu huwapeana kwa mawazo yao wenyewe na makristo wao wa uwongo, ambao hakuna hata mmoja wao aliye na uwezo wowote wa kuokoa (Warumi 1:21-23).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa kutakuwa na kristo wa uongo katika nyakati za mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries