settings icon
share icon
Swali

Makovu-ni nini? Je! Ni ya Kibiblia?

Jibu


Makovu ni kujitokeza ya majereha ya Yesu Kristo kwa mwili wa mtu. Baadhi ya makovu yanajumuhisha uwakilishi wa majeraha kwa mgongo wa Kristo yaliyosababishwa kwa mjeledi na/au majeraha ya kichwa yaliyosababishwa na taji ya miiba. Lakini,kidesturi, makovu yana hoja tano bora: upande (ambapo Yesu alichomwa na mkuki kuhakikisha kwamba Alikuwa amekufa) na mikono yote na miguu yote (majeraha yaliyosababishwa na misumari ya kusulubisha). Makovu pia yanajulikana kama "Majeraha Tano" au "Majeraha Tukufu ya Bwana wetu."

Watu kadhaa binafsi katika historia ya kanisa wamedai kupokea kimuujiza makovu. Hata hivyo, kuna changamoto kali uhalali wa madai hayo ya kujitokeza. Wengi wamethibitishwa kujiumiza katika jaribio kubuni muujiza wa makovu. Hakuna mahali popote Biblia inaagiza yeyote kupata makovu au kusema kwamba Mungu atatoa makovu. Katika Wagalatia 6:17, Paulo anasema, "Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu." Hii haimaanishi Paulo alikuwa na alama ya kusulubiwa halisi. Badala yake, inaonyesha kwamba mwili wa Paulo ulikuwa na alama kwa sababu ya kujitolea kwake kumfuata Kristo. Yesu aliteseka majeraha ili tusiweze kuteseka. Majeraha ya kusulubiwa yamewekwa kimuujiza kwa kujiumiza kwa mwili wa muumini inakinzana na ukweli kwamba mateso kwa dhambi si muhimu: "Bali alijeruhiwa kwa makossa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya Amani yetu ilikuwa juu Yake, na kwa kupigwa Kwake sisi tumepona."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Makovu-ni nini? Je! Ni ya Kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries