settings icon
share icon
Swali

Nini kilichotokea kwa kabila zilizopotea za Israeli?

Jibu


Wakati watu wanataja "makabila yaliyopotea ya Israeli," mara nyingi wana mawazo ya makabila kumi ya Ufalme wa Kaskazini ambao ulianguka kwa Ashuru mwaka wa 722 BC. Makabila haya ni Reubeni, Simeoni, Lawi, Dani, Nafitali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabuloni, na Yusufu (ambaye kabila lake liligawanywa katika kabila za Efraimu na Manase). Wengi wa watu wa Ufalme wa Kaskazini walipelekwa hutumwani huko Ashuru ya kale (2 Wafalme 17: 6). Wayahudi wengi waliosalia katika nchi waliadiliana na watu kutoka Cutha, Ava, Hamati, na Sefavaimu ambao walikuwa wametumwa na mfalme wa Ashuru kukaa Samaria (2 Wafalme 17:24; Ezra 4: 2-11). Kwa hiyo, hadithi kuwa, makabila kumi ya kaskazini ya Israeli "yalipotea" kwa historia na ama kufutwa au kuingizwa katika makundi mengine ya watu. Hadithi hii, hata hivyo, inategemea kisingizio au fikira badala ya mafundisho ya moja kwa moja ya kibiblia.

Kuna siri, hadithi, na mila nyingi kuhusu kile kilichotokea kwa makabila kumi ya Israeli. Hadithi moja inasema kwamba kabila kumi zilihamia Ulaya (Mto wa Danube, wanasema, walipewa jina kutoka kabila la Dani). Nadharia nyingine inasema makabila yamehamia kwenda Uingereza na kwamba Anglo-Saxons wote hii leo ni Wayahudi-hili ni fundisho la uongo kwa Waingeresa waridhi wa Israeli. Idadi ya makundi ya kote ulimwenguni hudai kuwa imetoka katika kabila "zilizopotea": kuna watu nchini India, Nigeria, Ethiopia, Pakistan, Afghanistan, na Amerika ya Kaskazini ambao wote wanadai kuwa wazao vile vile. Nadharia zingine zinawafananisha Wahindi wa Kijapani au wa Amerika na makabila kumi ya "Israeli waliopotea".

Ukweli ni kwamba "makabila yaliyopotea ya Israeli" hayakuwahi kupotea. Wayahudi wengi ambao walibaki katika nchi baada ya ushindi wa Ashuru waliungana tena na Yuda ya kusini (2 Mambo ya Nyakati 34: 6-9). Ashuru baadaye ilishinda na Babiloni, ambaye ilipigana na Ufalme wa Waisraeli wa Kusini, na kuwachukua utumwa kabila mbili zilizobaki: Yuda na Benyamini (2 Wafalme 25:21). Basi kuna uwezekano kuwa watu wa makabila ya kaskazini waliobaki walikuwa baadhi ya waliopelekwa utumwani Babeli. Miaka saba baadaye, wakati Mfalme Koreshi aliwawezesha Waisraeli kurudi Israeli (Ezra 1), wengi (kutoka kabila zote kumi na mbili) walirudi Israeli ili kujenga nchi yao.

Wazo kwamba makabila kumi ya Israeli yalikuwa "yamepotea" ni uongo. Mungu anajua pale ambapo kabila zote kumi na mbili ziko, na kama vile Biblia yenyewe inathibitisha, wote wanaweza hesabika. Katika nyakati za mwisho, Mungu ataita mashahidi kutoka kwa kila kabila kumi na mbili (Ufunuo 7: 4-8). Kwa hiyo, ni dhahiri, Mungu amekuwa akiweka rekodi ya nani katika kabila fulani.

Katika Injili, nabii Anna (Luka 2:36) alitoka kwa kabila la Asheri (moja kati ya makabila kumi yaliyopotea). Anna hakupotea kabisa. Wote Zakaria na Elisabeti-na kwa hiyo Yohana Mbatizaji-wanatoka kabila ya Lawi (Luka 1: 5). Yesu anawaahidi wanafunzi kwamba "na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli" (Luka 22:30). Paulo, ambaye anajua yeye ni wa kabila la Benyamini (Warumi 11: 1), anasema kuwa ahadi "ambayo kabila zetu kumi na mbili wanataraji kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku" (Matendo 26: 7) sio katika wakati sasa. Yakobo anaandika barua yake "kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika" (Yakobo 1: 1). Kwa kifupi, kuna ushahidi mwingi katika Maandiko kwamba kabila kumi na mbili za Israeli bado zipo na zitakuwa katika ufalme wa Kimesiya. Hakuna hata mmoja aliyopotea.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini kilichotokea kwa kabila zilizopotea za Israeli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries