settings icon
share icon
Swali

Je, kabila kumi na mbili za Israeli ni gani?

Jibu


Makabila kumi na mawili ya Israeli yalitoka kwa wana kumi na wawili wa Israeli. "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo (Mwanzo 32:28). Wana wake kumi na wawili ni Rubeni, Simeoni, Lewi, Yuda, Dani, Naftali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabuloni, Yosefu na Benyamini (Mwanzo 35: 23-26;). Wakati kabila lilirithi Nchi ya Ahadi, wazao wa Lawi hawakupokea eneo wenyewe (Yoshua 13:14). Badala yake, wakawa makuhani na walikuwa na miji kadhaa iliyoenea katika Israeli yote. Kabila la Yusufu liligawanywa na kuwa mbili-Yakobo alikuwa amechukua wana wawili wa Yusufu, Efraimu na Manase, kimsingi kumpa Yusufu sehemu mbili kwa ajili ya uaminifu wake kuokoa familia kutokana na njaa (Mwanzo 47: 11-12). Hii ina maana kwamba kabila zilizopokea eneo katika Nchi ya Ahadi walikuwa Reubeni, Simeoni, Yuda, Dani, Naftali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabuloni, Benyamini, Efraimu, na Manase. Katika sehemu fulani katika Maandiko, kabila la Efraimu linajulikana kama kabila la Yusufu (Hesabu 1: 32-33).

Baada ya Mfalme Sulemani kufa, Israeli aligawanyika na kuwa falme mbili. Yuda, ikimiliki kusini, ambayo ilijumisha Yuda, Simeoni, na Benyamini. Makabila mengine yaliwekwa pamoja ili kuunda ufalme wa Israeli kaskazini. Israeli iliharibiwa na Waashuri, na wengi wa Waisraeli waliuwawa au kupelekwa uhamishoni; Waisraeli ambao walibaki kuna uwezekon kuwa walijumuika na ufalme wa Yuda.

Yesu alitoka Yuda, Paulo alitoka uzao wa Benyamini, na Yohana Mbatizaji alikuwa Mlawi, lakini, tangu uhamisho wa AD 70, kutambua kabila la Myahudi wa sasa ni vigumu zaidi. Hiyo haimaanishi kwamba mgawanyiko wa kikabila sio wa maana. Wakati wa dhiki, wakati wengi ulimwenguni wakuwa wamemuacha Mungu na kumfuata Mpinga Kristo, Wayahudi 144,000 watatiwa muhuri na Mungu. Nambari hii inajumuisha 12,000 kutoka kila kabila. Kwa hiyo, hata kama hatujui ni nani katika kabila gani, Mungu amekuwa akiifadhi rekodi. Makabila yameorodheshwa tena katika Ufunuo 7: 5-8, lakini sio kabila lile lililopewa ardhi katika Yoshua. Manase yupo, na Efraimu (chini ya jina la Yusufu). Lakini badala ya Dani, Lawi amejumuishwa. Hakuna ufafanuzi unaotolewa wa ni kwa nini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kabila kumi na mbili za Israeli ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries