settings icon
share icon
Swali

Je, majaaliwa mara mbili ni nini?

Jibu


Majaaliwa mara mbili ni imani kwamba Mungu huwaumba watu fulani ambao kusudi lao kuwepo ni kutumwa kuzimu. Je, dhana hii ni ya kibiblia? Hebu tuangalie swali kutoka kwa kitabu cha Warumi, ambacho kina dhamira mbili kuu. Dhamira ya kwanza ni haki ya Mungu. Ni ujumbe wa injili yenyewe unaoonyesha haki ya Mungu (Warumi 1:16-17). Ni ukweli ulio ndani ya ujumbe wa Injili kwamba kwa imani humtangaza mtu mwenye haki mbele za Mungu (Warumi 4-5). Ni mfano wa kati wa ujumbe wa injili — Yesu Kristo – ambaye anawezesha mtu kuwa mwenye haki (Warumi 6-7). Ni ujumbe wa injili ambao unaonyesha mtu njia ya kuishi kwa haki (Warumi 12).

Dhamira nyingine iliyopatikana katika kitabu cha Warumi ni ile ya ghadhabu. Hasira ya Mungu imefunuliwa – na bado inafunuliwa — dhidi ya vitendo vyote vya dhambi (Warumi 1:18). Mwanadamu anajua kuhusu Mungu, lakini anakataa Mungu katika mawazo yao na katika matendo yao (Warumi 1:21-22). Kwa hivyo, ghadhabu ya Mungu ni kumpa mwanadamu kuishi maisha yake kama anavyopenda (Warumi 1:24, 26, 28), ambayo isipokuwa Mungu inaongoza kwa uharibifu (Warumi 1:28-32). Mtu anamkataa Mungu wa ulimwengu, na Mungu, kwa upande wake, anamwacha mwanadamu. Uingiliaji wa kibinafsi tu kutoka kwa Mungu unaweza kubadilisha njia ya uharibifu ambayo mtu hujipata wakati anajifanya mgumu mwenyewe katika dhambi.

Sasa tunasoma Warumi 9:22, na inasema, "Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhilihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu?" Watu wengi wanafikiri aya hii inafundisha kwamba Mungu amefanya vyombo fulani kwa hasira Yake. Lakini hii sio hoja ya aya. Kusoma hapo juu, mwadadamu tayari amepata hasira ya Mungu. Mwanadamu amejiweka mwenyewe kwa uharibifu. Ni Mungu ambaye huvumilia vyombo hivi — vyombo ambavyo vimejiandaa vyenyewe kwa uharibifu kwa sababu havitaacha dhambi zao na kurejea kwa Mungu.

Angalia mstari unaofuata: Warumi 9:23, "Naye akafanya hivyo ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu." Ona kwamba Mungu huchagua watu fulani tangu zamani kwa utukufu Wake. Kwa maneno mengine, kabla ya msingi wa ulimwengu Mungu alichagua watu fulani kuwa watoto Wake ili apate kutukuzwa (ona Waefeso 1:4). Haisemi kuwa Mungu alichagua watu kwa laana ya milele au watu waliojaaliwa kabla kwa ghadhabu. Biblia haijasema kamwe juu ya majaaliwa mara mbili ambapo Mungu huchagua au kujaalia kabla wengine kuzimu, wengine mbinguni. Wale walio chini ya ghadhabu ya Mungu wako katika hali hiyo kwa sababu wamemkataa Mungu. Wale ambao wana haki ya Mungu wako katika nafasi hiyo kwa sababu Mungu amewachagua kuwa watoto Wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, majaaliwa mara mbili ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries