settings icon
share icon
Swali

Je kunayo maisha baada ya kifo?

Jibu


Je, kunayo maisha baada ya kifo? Bibilia inatuambia, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kasha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe… Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena” (Ayubu 14:1-2,14)?

Kama vile Ayubu, karibu sisi sote tumekabiliwa na swala kama hili. Ni jambo gani hasa hutukia kwetu baada ya kufa? Je, ni kukosa kuwepo duniani tu? Je, maisha ni kufa na kufufuka tu ili tujipatie umaarufu tena duniani? Je, watu wote huenda mahali pamoja, au huenda mahali tofauti? Je, kunayo kweli Mbingu na Jehanamu, au ni maneno tu ya kujitungia?

Bibilia inatuambia yakwamba sio maisha pekee tu baada ya kifo, bali kuna uzima wa milele wenye utukufu mwingi “Hakuna jicho limeshaona, wala sikio kuyasikia,wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao’’ (1Wakorintho 2:9) Yesu Kristo, Mungu katika mwili, alikuja duniani kutupa karama ya uzima wa milele. “Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona’’ (Isaya 53:5).

Yesu alichukua adhabu aliyostahili kila mmoja wetu na akajitoa maisha yake. Siku tatu baadaye, akathibitisha ushindi wake juu ya mauti kwa kufufuka kutoka kaburini, katika roho na katika mwili. Alibaki katika dunia kwa mda wa siku arubaini na kushuhudiwa na maelfu ya watu kabla ya kupaa nyumbani kwake Mbiguni kwenye uzima wa milele. Warumi 4:25 yasema, “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu,na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.’’

Ufufuo wa Kristo lilikuwa ni jambo lililodhihirika Mtume Paulo aliwapatia watu changamoto kwamba wawaulize wale waliokuwapo wakati jambo hilo likitendeka wahakikishe kama jambo hilo si kweli. Hakuna aliyeweza kushindana juu ya ukweli huo. Ufufuo ndio msingi imara (jiwe la pembeni la) wa imani ya Mkristo; kwasababu Kristo alifufuka katika wafu, sisi pia tunaweza kuwa na imani ya kwamba tutafufuliwa.

Paulo aliwaonya wakristo wa kwanza ambao hawakuyaamini haya: “Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka” (Wakorintho 15:12-13).

Kristo alikuwa pekee wa kwanza kati ya mavuno makuu ya wale watakao inuliwa kutoka kwa wafu. kifo kiliingia duniani kuputia mtu mmoja, Adamu ambaye sisi sote ni wa ukoo wake. lakini wale ambao wamefanywa wana wa Mungu kupitia imani juu ya Yesu Kristo watapewa maisha mapya (Wakorintho wa kwanza 15:20-22). Kama vile Mungu alivyofufua mwili wa Yesu, vivyo hivyo ndivyo miili yetu itakavyofufuliwa Yesu atakaporudi (Wakorintho wa kwanza 6:14).

Ijapokuwa sote tutakuwa tumefufuliwa, hatutaenda sote mbinguni mahali pamoja. Mtu sharti afanye uamuzi wa kuchagua sasa juu ya mahali anapotaka kuenda kwa umilele wake. Bibilia inasema ya kwamba imetupasa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu (Waebrania 9:27). Wale waliotakaswa wataenda kwa uzima wa milele mbinguni, lakini wasioamini watapelekwa kwa hukumu ya milele ama jehanamu (Mathayo 25:46).

Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.

Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na ziwa la moto, liwakalo na kiberiti amabpo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.

Maisha ya duniani ya sasa ni mtihani tu; ni matayarisho ya yale yajayo. Kwa waaminio, huu ni uzima wa milele kuweko mbele za uwepo wa Mungu. Basi ni kwa jinsi gani tunafanyinyika wenye haki na kustahili kupokea uzima huu wa milele? Kuna njia moja pekee – kupitia imani na tumaini ndani ya mwana wa Mungu, Yesu kristo. Yesu alisema, “mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Waniaminio mimi wajapokufa wataishi. Wanapawa uzima wa milele kwa kuniamini mimi na hawatapotea…” (Yohana 11:25-26).

Kipawa hiki cha uzima wa milele kinapatikana na ni bure kwa wote lakini kinagharimu kujikana wenyewe raha Fulani za dunia na kutoa sadaka kwa Mungu. “na wote wamwaminio mwana wa Mungu wana uzima wa milele. Wasiomtii mwana hawatapata uzima wa milele bali ghadhabu ya Mungu inadumu juu yao” (Yohana 3:36). Hatutapatiwa nafasi ya kutubu dhambi zetu baada ya kufa kwa kuwa tukimuona Mungu uso kwa uso hatutakuwa na lengine ila kumwamini. Anatutaka tumjilie sasa kwa imani na upendo. Tunapokubali kwamba kifo cha Yesu msalabani ni malipo kamili ya dhambi zetu dhidi ya Mungu, tumeahidiwa si tu maisha mema duniani bali pia uzima wa milele mbele ya kristo.

Ukitaka kumpokea Yesu kristo kama mwokozi wako, hapa kuna ombi rahisi. Kumbuka kusema ombi hili wala lengine hakutakuokoa kutokana na dhambi zako bali kwa kumwamini kristo pekee. Ombi hili ni njia tu ya kujielezea mbele za mungu juu ya kumwamini kwako na kumshukuru kwa kumtoa njia ya wokovu wako. “Mungu, ninajua ya kwamba nimefanya dhambi na ninapaswa hukumu. Lakini Yesu kristo alichukua adhabu yangu ili kwamba kwa kumwamini yeye nipate msamaha wa dhambi zangu. Ninaghairi dhambi zangu sasa na kuziacha. Ninaweka tumaini langu kwake kwa wokovu wangu. Asante kwa neema yako ya ajabu na msamaha – kipwa cha uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je kunayo maisha baada ya kifo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries