settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya mahubiri tafsiri?

Jibu


Mahubiri fafanuzi ni mahubiri ambayo yanazingatia kuelezea maana ya Maandiko katika muktadha wake wa kihistoria na kisarufi. Mahubiri fafanuzi yanahusu kuelezea kile ambacho Biblia inasema kwa wasikilizaji wa kisasa ambao labda hawafahamu mazingira ya kitamaduni na kihistoria ambayo kufungu hicho kiliandikwa.

Neno kufafanua linamaanisha "kuweka wazi au kuelezea." Kwa hivyo mahubiri fafanuzi ni ufafanuzi wa maandiko ambayo hutegemea usomaji wa uangalifu na ufafanuzi wa kifungu. Ni wito wa msingi wa mchungaji au mhubiri kama tunavyoona katika 2 Timotheo 4:2: "lihubiri neno! Uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."

Mahubiri fafanuzi ni muhimu kwa wanaoamini katika msukumo kamili wa maneno ya maandiko ambayo inamaanisha kwamba maandiko ni Neno la Mungu. Kama Neno lililopuliziwa na Mungu, maandiko yanafaa kutangazwa na kuelezwa katika muktadha ambao yaliandikwa.

Kusoma tu Zaburi 119 na kuelewa kwamba maandiko ni "pumzi ya Mungu" (2 Timotheo 3:16) ni ya kutosha kuelewa dhamani na umuhimu wa mahubiri fafanuzi Katika Zaburi 119 tunaona sifa nyingi za Neno la Mungu, lakini zaidi ya yote, sura hii inapaswa kutusaidia kuelewa umuhimu kujua kile Biblia inachosema na inachomaanisha; hii ndio lengo la mahubiri fafanuzi. Ikiwa hatuelewi Biblia, hatuwezi kuifuata, na pia haiwezi kuwa "taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu" (Zaburi 119:105).

Lengo la mahubiri fafanuzi ni kutangaza haswa kile kifungu cha maandiko kinasema. Kwa hivyo muhtasari wa mahubiri ya ufafanuzi yanapata vidokezo kuu na vidogo kutoka kwa maandishi ya maandiko ambayo muhubiri anafafanua.

Inapaswa kuwe na malengo mawili makuu ya mahubiri fafanuzi. Lengo la kwanza ni kugundua na kueleza maana asili, ya kihistoria na ya kisarufi ya kifungu hicho, au kueleza kwa njia ingine, "maana ya Mungu aliyokusudia." Huu ni ujumbe aliokua nao Mungu kwa wasikizi wake, ambao uliongozwa na Mungu. Lengo la pili linahusiana na la kwanza sana- kusaidia watu kutumia maishani yao ukweli uliofunuliwa katika kifungu hicho. Wengine hupuuza uwezo wa mahubiri ya ufafanuzi kuangazia mahitaji ya washirika wengi hii leo, lakini hupuuza ukweli kwamba "Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo" (Waebrania 4:12). Nguvu za kubadilisha maisha zinapatikana ndani ya Neno la Mungu pekee linapotumika kupitia kwa Roho Mtakatifu ndani ya mioyo ya wanaume na wanawake. Uwasilishaji mzuri ni mwema lakini haubadilishi maisha. Huku bado kukiwa na nafasi ya mahubiri ya maudhui, yanahitaji kutimiza mahubiri fafanuzi, sio kuyaondoa kabisa.

Mahubiri ya ufafanuzi ni muhimu kwa sababu, ikiwa yamefuatwa kwa uaminifu, husababisha ufahamu wa ushauri kamili wa Mungu unaohubiriwa. Masomo magumu au yenye utata hayawezi kupuuzwa au kusahau kama vile tunaweza kuona katika mahubiri ya maudhui. Mfafanuzi anashughulika na kile kifungu kinasema, mstari baada ya mstari, sura kwa sura, kitabu baada ya kitabu. Inasaidia kuzuia kuchukua vifungu nje ya muktadha na kumlazimisha mchungaji mwaminifu kwa uagnalifu kushughulikia maswala yenye utata na magumu na masomo.

Baadhi wanaotaka kupuuza umuhimu wa mahubiri fafanuzi wanasema kwamba uwezo wa mhubiri kuwasilisha maudhui yanayofaa ambayo wanaamini kuwa kanisa lao linapaswa kusikia. Wakosoaji hawa wanashindwa kutambua nguvu ya Neno la Mungu, ambalo, linapowasilishwa kwa ukamilifu wa ukweli wake, halitarudi bure (Isaya 55:11).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya mahubiri tafsiri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries