settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya mahubiri ya mada? Je! Mchungaji anafaa kuhubiri mahubiri yaliyo na mada?

Jibu


Mahubiri ya maudhui ni aina ya mahubiri ambayo yanalenga mada fulani. Mara nyingi hulinganishwa na mahubiri fafanusi. Mahubiri ya maudhui yanaangalia kile Biblia inasema kuhusu somo fulani huku mahubiri fafanuzi yanaangazia kile kifungu katika Biblia kinamaanisha na jinzi kitakavyo tumika katika maisha yetu hii leo. Baadhi ya wahubiri angalau uhubiri mahubiri ya maudhui, huku wengine wakiangazia moja kwa moja mahubiri ya maudhui. Mfano huu uwe ni mzuri au mbaya labda inahusiana zaidi na jinsi unavyotumika kuliko kitu kingine chochote. Kuhubiri kwa madhui kunaweza kuwa na ufanisi, lakini kuna upungufu kwa asili ambako ni lazima kueleweke ikiwa kutatumika vizuri.

Mahubiri yanaweza kugawanywa katika aina nne: maandishi, maudhui, maandishi-maundhui, na ufafanuzi. Wengine wameona kuwa vitengo hiviingiani vizuri sana, haswa kwa kuwa kuna mwingiliano kati ya aina hizo. Kwa ujumla, mahubiri ya maandishi hufuata muundo wa maandishi ya Maandiko, ukiruhusu mtiririko wa maneno kutoa hoja za mahubiri. Mahubiri ya maudhui yamepangwa kulingana na wazo, huku vigezo kuu vikipangwa na mhubiri na kuungwa na maandiko ili kuthibitisha. Mahubiri ya maudhui-maandishi yanaunganisha aina hizo mbili, ikiruhusu vidokezo vya mahubiri kutoka kwa maandishi au mawazo ya msemaji. Mahubiri ya ufafanuzi hufuata maandishi ya Maandiko, halafu hutafuta kutoa maana kamili kifungu. Lengo la kila aina ya mahubiri ni kuliweka Neno la Mungu katika maisha ya wasikiaji.

Katika mahubiri ya maudhui, mnenaji ana uhuru wa kuangazia maswala yanayowakabili wasikilizaji wake. Ikiwa hitaji ni kuielewa dhambi vizuri, safu ya mahubiri yanaweza kutengezwa ili kushughulikia mambo anuwai na matokeo ya dhambi. Wakati yamefanywa vizuri, aina hii ya mahubiri itatoa wigo pana la kile Biblia inasema juu ya mada fulani. Kwa kuzingatia maswala kwa njia hii, watu wanaweza kukuza uelewo wa kibiblia wa mada yoyote. Faida nyingine ya mahubiri ya mada ni umoja wa mawazo. Watu wanaweza kufuata mtiririko wa mawazo, ambayo mara nyingi huwasaidia kukumbuka yale waliyosikia. Njia hii inajitolea vizuri kwa karama ya asili ya msemaji, kwa sababu mawazo hutoka kwa moyo mwake.

Huku kuhubiri kwa maudhui kukimruhusu mzungumzaji kukuza mahubiri bora, pia ina hatari zake kadhaa. Ikiwa hiyo ndio njia pekee inayotumiwa, msemaji anaweza kunaswa kwa urahisi katika mahubiri ya mada ambazo zinamvutia au zile ambazo kwa urahisi zinaweza ekwa katika ujumbe. Vivyo hivyo, hadhira inaweza kuegemea ujumbe "mzuri" au "wa kufurahisha", akiachana na mafundisho ambayo hayafanani na mfano huo. Zingatio dhabiti kwa mahubiri ya mada pekee kutasababisha uelewo dhaifu wa shauri lote la Mungu, ingawa masomo kadhaa yataeleweka vizuri. Katika visa vingine, msemaji anaweza kushawishiwa kufikiria zaidi maoni yake mwenyewe kuliko "ukilitumia kwa usahihi neno la kweli" (2 Timotheo 2:15).

Kwa sababu hizi, wachungaji wengi hubadilishana kati ya ujumbe wa mada na maandishi au ufafanuzi. Ujumbe wa mada unawaruhusu kushughulikia maswala yanayo ikabili jamii sasa au maisha ya kanisa, huku ujumbe wa maandishi na ufafanuzi unaundwa juu ya "lengu kuu" la vitabu vyote katika Biblia. Zote mbili ni za muhimu katika kukuza ukuaji wenye usawa katika maisha ya Kikristo. Namna mahubiri yamepangwa sio muhimu sana kama vile kuhakikisha kuwa ni ya kibiblia na yanafaa hali yetu. Ujumbe wa mada unaweza kuwa wa kimaandiko kama ule wa ufafanuzi, na ujumbe wa ufafanuzi unaweza kuwa wa kuvutia kama ule wa mada.

Bila kujali aina ya ujumbe, ikiwa aina hiyo imejikita katika Maandiko na matumishi yake katika maisha kwa mtazamo wa maandiko, utatimiza lengo na kuwavuta watu wamfuate Kristo kwa karibu zaidi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya mahubiri ya mada? Je! Mchungaji anafaa kuhubiri mahubiri yaliyo na mada?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries