settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu magonjwa yanayo enea kwa kasi/magonjwa janga?

Jibu


Mkurupuko mbali mbali wa mogonjwa yaeneayo kwa kasi, kama vile Ebola au virusi vya korona, yamesinikisha watu wengi kujiuliza ni kwa Mungu anayaruhusu au kusababisha magonjwa ya majanga na ikiwa magonjwa kama hayo ni ishara ya nyakati za mwisho. Bibilia hasa Agano La Kale inaelezea matukio mbali mbali wakati Mungu alileta mapigo na magonjwa kwa watu wake na kwa maadui Wake “nikuonyeshe uweza wangu” (Kutoka 9:14,16). Alitumia mapigo kwa wa Misiri ili kumsulutisha Farao kuwaachilia Waisraeli toka utumwani, huku akiwazuia watu wake kutokana na madhara ya mapigo (Kutoka 12:13; 15:26), hii ikionyesha uweza wake mkuu juu ya magonjwa na mateso yoyote.

Mungu pia aliwaonya watu wake kuhusu madhara ya kutotii, hii ikiwa ni pamjo na mapigo (Mambo ya Walawi 26:21,25). Katika matukio mawili, Mungu aliwaangamiza watu 14,700 na vile vile watu 24,000 kwa sababu ya matendo yao mbali mbali ya kijeuri (Hesabu 16:49 na 25:9). Baada ya kuwapa sheria ya Musa, Mungu aliwaamuru watu kuitii sheria hiyo au kukumbwa na maafa, hii inahusisha ugonjwa unaonekana kama Ebola: “Mwenyezi -Mungu atawashambulia kwa kifua kikuu, homa, majipu, joto kali, ukame…mambo haya yatawaandama mpaka mmeangamia” (Kumbukumbu 28:22). Hii baadhi ya mifano michache ya mapigo mengi na magonjwa yalisababishwa na Mungu.

Ni jambo gumu kuwaza kuwa Mungu wetu mwenye upendo na huruma anaonyesha ghadhabu na hasira kwa watu wake. Lakini adhabu ya Mungu kila wakati huelekeza kwenye toba na urejesho. Katika Mambo ya Nyakati ya pili 7:13-14, Mungu alimwambia Solomoni, “Nikiwanyima mvua ama nikiwaletea nzige wale mimea yao au wakipatwa na maradhi mabaya, kama watu wangu walioitwa kwa Jina langu watanyenyekea, na kusali, na kutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi mimi nitawasikiliza kutoka juu mbunguni; nitawasamehe dhambi yao na kuistawisha nchi yao.” Hapa tunamwona Mungu akitumia janga kuwarejesha watu wake, kujibuza toba ndani yao na nia ya kurejea kwake kama wana Wake kwa Baba yao wa mbinguni.

Katika Agano Jipya, Yesu aliponya “kila ugonjwa na kila dhara” vile vile na mapigo katika sehemu alizozulu (Mathayo 9:35; 10:1; Marko 3:10). Kama vile alivyo amua kutumia mapigo na magonjwa ili kuonyesha uweza wake kwa Waisraeli, Yesu aliponya dhihirisho ya nguvu hizo ili kutibitisha kuwa alikuwa mwana wa Mungu wa kweli. Alipeana uweza huo wa uponyaji kwa wanafunzi wake ili kutibitisha huduma yao (Luka 9:1). Mungu bado anaruhusu magonjwa kwa lengo lake pekee, lakini muda mwingine magonjwa, hata yale yameadhiri ulimwengu wote yana sababu ya kipekee ya kiroho, lakini hatujui kuwa Mungu ana uweza wa kudhibiti mambo yote (Warumi 11:36) na atafanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wamjuao na wampendao (Warumi 8:28).

Kuenea kwa ugonjwa kama vile Ebola na virusi vya Korona ni kionjo cha mkurupuko wa magonjwa yatakayo kuwepo nyakati za mwisho. Yesu alitaja tauni za siku za usoni, ambazo zinahusiana na nyakatiza mwisho (Luka 21:11). Mashaidi wawili katika kitabu cha Ufunuo watakuwa na mamlaka ya “kuipiga dunia na tauni za kila aina mara nyingi jinsi wanavyotaka” (Ufunuo 11:6). Malaika saba watasababisha mpigo wa tauni saba mfululizo, hukumu kali za mwisho kama inavyoelezwa katika Ufunuo 16.

Kuoneka kwa mkurupuko wa magonjwa kunaweza au pia kukosa kuunganishwa na hukumu maalum ya Mungu ya dhambi. Inaweza pia kuwa matokeo ya kuishi katika ulimwengu ulioanguka. Kwa vile hakuna yeyote anayejua wakati Yesu atakaporudi, yapaswa tuwe makini tunaposema kuwa mkurupuko wa magonjwa duniani ni dhibitisho kwamba tunaishi katika siku za mwisho. Kwa wale hawajamjua Yesu Kristo kama mwokozi, magonjwa yanafaa yawe ukumbusho kwao kuwa maisha katika ulimwengu huu ni mafupi na yaweza kukatika wakati wowote. Jinsi magonjwa yaeneayo kwa kasi yalivyo mabaya, jahanamu itakuwa mbaya zaidi. Ile hali Mkristo ana uhakikisho wa wokovu na tumaini la milele kwa sababu ya damu ya Yesu Kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu (Isaya 53:5; 2 Wakorintho 5:21; Waebrania 9:28).

Wakristo wanapaswa kukabiliana aje na magonjwa yaeneayo kwa kasi? Kwanza, hawafai kuwa na hofu. Mungu yuko ushukani. Bibilia inasungumzia neno sawia na “usihofu” zaidi ya mara 300. Pili, uwe na busara. Chukua hatua mwafaka kujikinga na ugonjwa, na ulinde familia yako na kuwatunza. Tatu, ona nafasi ya huduma. Kila mara nyingi watu wanaposhikwa na hofu ya maisha yao, huwa tayari kuwa na masungumzo kuhusu maisha ya baadaye. Uwe na ujaziri na mwenye huruma katika kushiriki kwako injili, kila mara nena ukweli katika upendo (Waefeso 4:15).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu magonjwa yanayo enea kwa kasi/magonjwa janga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries