settings icon
share icon
Swali

Mafundisho ya mitume ni nini?

Jibu


Maana ya ndani ya neno mtume ni "aliyetumwa." Mafundisho nayo ni mafunzo. Basi mafundisho ya mitume ni yale mafunzo tuliyopewa kupitia kwa mitume, wale waliochaguliwa na Yesu kupeleka mafunzo yake ulimwengu kote. Wanafunzi wale kumi na wawili ndipo wakawa mitume (Mariko 3:14) pasipo kuweko Yuda, aliyemsaliti. Badala yake ni Mathiya katika Matendo 1:21-26. Mathiya aliteuliwa kuwa mtume kwa maana alikuwa "kaka nao [watume] wakati wote Yesu alipokuwa kaishi nao, tangu wakati wa Yohanna mbatizaji hadi wakati Yesu alipotwaliwa kutoka kwao." Roho mtakatifu alionekana kukubaliana na uamuzi huo. Bila kupinga kuongezwa kwa mathiya kwenye kundi hilo, Mungu pia alichagua Sauli wa Tarso kuwa mtume atakaye peleka ujumbe kwa mataifa (Mtendo 9:15]. Kupitia kwa Agano Jipya, tunaweza kupata ujumbe wa mitume. Kwa sehemu kubwa, Agano Jipya liliandikwa na mitume ama wale waliokuwa na uhusiano wa karibu nao.

Injili kulingana na mathayo iliandikwa na Mtume Mathayo, mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa kwanza.

Injili kulingana na Mariko iliandikwa na Mariko anayetwa katika Matendo kama aliyefanya kazi karibu na Sauli. Historia ya kanisa pia inaelezea kuwa Mariko alikuwa karibu sana na Petero na kuwa injili yake inalenga sana mafunzo ya Petero.

Injili kulingana na Luka na Matendo ya Mitume ziliandikwa na Luka. Luka alikuwa kafanya kazi karibu na Sauli na alikuwa kashuhudia matukio mengi katika Matendo. Ingawa hakuwa mshuhuda kwa maisha ya yesu, alifanya maojiano ambayo yalihusisha hata mitume [Luka 1:3]. Kazi yake nyingi inafanana na ile ya Mariko na Mathayo, kwa hivyo ni wazi kuwa alihusisha sana nakala za mitume.

Injili kulingana na Yohanna, vile vile waraka wa 1, 2,na 3 Yohana na Ufunuo ziliandikwa na mtume Yohana, mmoja wa mitume wale kumi na wawili.

Warumi, 1 na 2 Wakorintho, wagalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1 na 2 Wathesalonike, 1 na 2 Timotheo,Tito, na Filemoni zote ziliandikwa na mtume Sauli.

Yakobo iliandikwa na nduguye wa kambo wa Yesu Yakobo, aliyekuwa kiongozi wa kanisa kule Yerusalemu. Bila shaka alikuwa mshuhuda mkuu kwa matukio mengi kwa maisha ya Yesu. Yeye hajaitwa kuwa mtume bali anaitwa mzee na alifanya kazi karibu sana na mitume. Mtume Sauli katika Wagalatia 2:9 anamtaja Yakobo kuwa "nguzo wa kanisa" pamoja na mtume Petero na Yohana. Inashangaza kuwa Yakobo hakuwa muumini hadi baada ya ufufuo wa Yesu na kujionyesha kwake. 1Wakorintho 15:7 inasema kuwa Yesu alionekana kwanza kwa Yakobo kisha "kwa mitume"inayoweza kuashiria kuwa Yakobo alitambulika kuwa mfuasi wakati ambapo Sauli alikuwa akiandika 1 Wakorintho.

Waraka wa kwanza na wa pili wa Petero uliandikwa na mtume Petero.

Yuda iliandikwa na mmoja wa ndugu wa kambo wa Yesu ambaye alikuwa mshuhuda mkuu kwa maisha ya Yesu na mafundisho yake. Kama vile Yakobo, hakuwa muumini hadi baada ya ufufuo.

Waebrania ndicho kitabu cha pekee kwenye Agano Jipya ambacho mwandishi hajatambulika. Hakuwa mshuhuda wa matendo ya Mungu duniani, ila kazi yake inategemea ushuhuda wa walioshuhudia kama asemavyo katika Waebrania 2:3 "Wokovu huu,ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia."

Mafundisho ya Mitume ni ya muhimu kwa kuelewa ni yapi Mungu ametutendea. Waandishi wa Agano Jipya wanayataja kuwa mafundisho ambayo yanaitwa "imani" ama "injili."Yuda anasema kuwa "imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."Sauli kwa kishindo analaani watu wataobadilisha maana ya injili katika Wagalatia 1:6-9 "Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika nehema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya kristo. Lakini ijapokuwa sisis au malaika wa mbinguni atawahubiria ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiria, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe na Mungu."

Katika orodha ya zawadi za kanisa, Sauli anaorodhesha utume kama zawadi ya kimsingi (Waefeso 2: 20). Baada ya misingi ya kanisa kuwekwa na mafundisho ya mitume kunakiliwa katika maandishi, kazi ya mitume haikuhitajika tena. Kunao umuhimu bado kwa wahubiri, walimu, na wamishenari kueneza neno la Mungu (mafundisho ya mitume) kwa ulimwengu wote. [tazama Mathayo 28:19-20; Yohana 17:20]

Baaadhi ya makanisa hadi sasa wanatumia neno mitume kwa nembo yao. Kwa wengine, hii inamaanisha kuwa wanaamini kuwa zawadi za mitume zinamaana katika kanisa lao. Kama ni hivyo, hii inaweza kuleta kutoeleweka kwa mafundisho ya mitume katika Agano Jipya. Kwa wengine, inaweza kumaanisha wanataka kusisitiza mafundisho ya mitume kama yalivyo katika Agano Jipya. Kama hayo ndiyo kweli wanayofanya, basi hilo ni jambo la busara. Kanisa la mitume, moja ya mashirika ya kiroho, linasema kuwa wanafuata kwa ukaribu mafundisho ya mitume ila kwa bahati mbaya waamini kuwa upatizo wa uzamisho ndani ya maji mingi ni muhimu kwa ukombozi na pia ukombsozi utafuatwa na ishara za zawadi. Vile tuonavyo zawadi za roho zinavyotumika katika kitabu cha Matendo, si mafundisho ya mitume kuwa ubatizo ni wa muhimu katika ukombozi ama kuwa kila mkristo aonyeshe ishara fulani. Katika fungu hili, ingawa jina "mitume," mafundisho hayaambatani.

Wakati kanisa lilianza, Luka alinakiri, waumini wa kwanza "wakawa wakidumu katika mafundisho ya mitume na katika ushirika" [Matendo 2:42]. Hiyo ni kumaanisha, walijitolea kwa kujifunza na kufuata mafundisho ya mitume. Kwa hilo walikuwa na hekima. Ikiwa kanisa la sasa litakuwa na hekima, basi watajitolea kwa mafundisho ya waanzilishi wa kanisa la duniani, waliochaguliwa na Mungu mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mafundisho ya mitume ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries