settings icon
share icon
Swali

Je! Mabakuli saba ya ghadhabu ni nini katika Ufunuo?

Jibu


Bakuli saba au hukumu za bakuli ni hukumu za mwisho za kipindi cha dhiki. Itakuwa hukumu kali zaidi duniani ambazo hazijawahi kuonekana. Bakuli saba zimeelezewa katika Ufunuo 16: 1-21, ambapo zinaitwa "mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu" (Ufunuo 16: 1). Chini ya Mpinga Kristo, uovu wa mwanadamu umefikia kilele chake, na hukutana na ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi. Hukumu saba za bakuli huitwa na tarumbeta ya saba.

Bakuli ya kwanza. Malaika wa kwanza anamimina bakuli ya kwanza juu ya nchi, "Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake" (Ufunuo 16:2). Pigo hili linalenga wale wamejitolea kwa Mpinga Kristo; watakatifu wa unyakuo hawataadhirika na majipu hayo.

Bakuli la pili. Bakuli la pili linamiminwa baharini nayo maji yakabadilika na "kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa" (Ufunuo 16:3). Na thuluthi moja ya viumbe baharini tayari vilikuwa vimeangamia kwa kupigwa kwa tarumbeta ya pili (Ufunuo 8: 9), na sasa viumbe vingine vya baharini vimekufa. Bahari zimekufa.

Bakuli la tatu. Wakati bakuli la tatu la ghadhabu ya Mungu lilimiminwa kwa, mito, na chemi chemii za maji safi pia ziligeuka na kuwa damu (Ufunuo 16: 4-5). Malaika msimamizi wa maji akisema, "Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa, wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu, kwa sababu umehukumu hivyo; kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako na manabii wako, nawe umewapa damu wanywe kama walivyostahili." (Ufunuo 16:5-6). Madhabahu mbinguni yanaitikia, "Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni kweli na haki" (Ufunuo 16:7).

Bakuli la nne. Malaika wa nne anaimimina bakuli yake kwa jua, "nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. Watu wakaunguzwa na hilo joto kali" (Ufunuo 16:8-9). Badala wao watubu dhambi zao, watu waovu walioishi duniani "wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, tena wakakataa kutubu na kumtukuza Mungu" (Ufunuo 16:9). Bakuli la tano. Bakuli la tano kati ya mabakuli saba lilisababisha ufalme wa mnyama uligubikwa na giza totoro. Uchungu na mateso wa waovu unaongezeka, ili watu watafune ndimi zao kwa ajili maumivu (Ufunuo 16:10-11). Bado wafuasi wa Mpinga Kristo "hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu" (Ufunuo 16:11).

Bakuli la sita. Malaika wa sita anamimina hukumu mtoni Frati. Mto huo unakauka kwa kutayarishia njia mfalme wa Mashariki kuelekea uangamizo (Ufunuo 16:12). Yohana anaona roho tatu sisizo safi "zilionekana kama chura" inayotoka mdomoni mwa Shetani, Mpinga Kristo na nabii wa uwongo (Ufunuo 16:13). Mapepo hawa wanatenda ishara na kuwadanganya wafalme wa dunia na kuwakusanya kwa vita vya mwisho vya Siku ya Bwana (Ufunuo 16:14). Chini ya ushawishi wa mapepo, "Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Armagedoni" (Ufunuo 16:16).

Bakuli la saba. Bakuli la saba linamiminwa kwa anga. Sauti kubwa mbinguni inasema, "Imekwisha kuwa!" (Ufunuo 16:17). Bakuli la saba linasababisha radi na tetemeko la ardhi kali sana kiwango kwamba, "Hapajawa kamwe na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, hivyo lilikuwa tetemeko kubwa ajabu" (Ufunuo 16:18). Yerusalemu inagawanyika katika sehemu tatu na miji ya mataifa ikaanguka (Ufunuo 16:19). Viziwa vimefurika na milima ikatoweka (Ufunuo 16:20). Mawe ya theluji kubwa, "yenye uzito wa talanta moja ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu" (Ufunuo 16:21). Wale walio chini hukumu "Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha" (Ufunuo 16:21). Mmoja wa malaika wa hukumu saba za bakuli kisha anamwonyesha Yohana hatima ya Babeli Kuu (Ufunuo 17), wakati Mungu anapolipiza kisasi "damu ya manabii na ya watakatifu, na wote waliouawa duniani" (Ufunuo 18 : 24). Ulimwengu uliomboleza kuanguka kwa Babeli (Ufunuo 18), lakini mbingu ilifurahi (Ufunuo 19). Kisha Yesu Kristo anarudi kwa utukufu kuyashinda majeshi ya Mpinga Kristo katika Armagedoni (Ufunuo 19: 11–21) na kuanzisha ufalme wake duniani (Ufunuo 20: 1–6).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mabakuli saba ya ghadhabu ni nini katika Ufunuo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries