settings icon
share icon
Swali

Maana ya maisha ni nini?

Jibu


Maana ya maisha ni nini? Nawezaje kupata utimilifu, lengo na kutosheka maishani mwangu? Je, nitafanikiwa kuwa na uwezo wa kutimiza jambo la kudumu? Watu wengi hawajaacha kufikiria juu ya maana ya maisha ni nini. Huangalia nyuma na kuhuzunukia uharibifu uliowapata na hata kusahau yale mema waliyofaulu kuwa nayo. Malengo mengi huthibitisha utupu wake baada ya miaka kadhaa kupita yakishughulikiwa.

Katika maisha yetu ya siku baada ya siku, watu hushughulikia malengo mbalimbali wakidhania watapata maana ya maisha ndani yake. Malengo haya ni kama mafanikio ya kibiashara, mali, uhusiano mzuri, mapenzi, tafrija, kutendea wengine mema, na kadhalika. Watu wamewahi kushuhudia ya kwamba hata baada ya kufaikiwa katika malengo yao ya mali, uhusiano, raha, kulibaki bado utupu ndani yao pamoja na kutotosheka ambako hakuna kitu kingine kingejaza.

Muandishi wa kitabu cha mhubiri afafanua hali hii kwa kusema, “Ni ubatili, ni ubatili!...ubatili mtupu! Kila kitu ni ubatili,” mwandishi huyu alikuwa na mali nyingi, hekima kupita wote walioishi naye wakati wake na wetu pia, mamia ya wanawake, ikulu kadhaa na mashamba na alikuwa muonewa wivu wa falme zote, chakula chema na divai pamoja na kila aina ya kitu cha kutumbuiza. Akasema wakati mmoja kwamba kila kitu moyo wake ulichokitamani hakujinyima. Hatimaye akasema “Misha chini ya jua” (maisha ya kuona tu kile kilichoko na kuhisi na hisia zetu kile kilichoko) ni ubatili! Ni kwa nini kuna hali hii ya utupu ndani yetu? Kwa sababu Mungu alituumba kwa ajili ya kituzaidi ya kuona na kuhisi hapa na pale. Suleimani alisema haya kwa ajili ya Mungu, “Ameweka umilele ndani ya mioyo ya wanadamu…”

Ndani ya mioyo yetu tunahisi yakuwa haya siyo yote ambayo tunaishi kwa ajili yake. Katika kitabu cha Mwanzo, kitabu cha kwanza cha biblia, tunaona ya kuwa Mungu aliumba mwanadamu kwa mfano wake (Mwanzo 1:26). Hii ina maana ya kuwa sisi tumefanana na Mungu zaidi kuliko kitu chengine kile kinachoishi. Tunaona ya kwamba mabo ya fuatayo yalikuwa dhahiri kabla ya mwanadamu kuanguka dhambini na laana kuja juu ya ardhi: (1) Mungu alimfanya mwanadamu kuwa kiumbe cha ushikamano na wengine (Mwanzo 2:18-25); (2) Mungu alimpatia kazi mwanadamu (Mwanzo 2:15); (3) Mungu alikuwa na ushirika na mwanadamu (Mwanzo 3:8); (4) Mungu alimpa mwanadamu kuimiliki dunia na vilivyomo (Mwanzo 1:26). Vitu hivi vina umuhimu gani? Ninaamini Mungu alitaka kuongeza ndani yetu vitu hivi kwa utimilifu wetu. Lakini baadhi ya haya (kama ushirika wa mwanadamu na Mungu ulivyo sasa) yaliathiriwa na kuanguka dhambini kwa mwanadamu na laana iliyokuja juu ya ardhi (Mwanzo 3).

Katika kitabu cha mwisho cha biblia, ufunuo wa Yohana, mwisho wa mambo mengi ya mwisho wa dunia, Mungu asema ataziharibu mbingu na dunia za sasa na mahali pake ataleta mbingu mpya na dunia mpya. Hapo atarudisha ushirika na wanadamu waliokombolewa. Wanadamu wengine watakuwa wamehukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo wa yohana 20:11-15). Na laana ya dhambi itaondolewa; dhambi haitakuweko tena, wala huzuni,magonjwa wala kifo, maumivu wala uchungu, na kadhalika (Ufunuo wa yohana 21:4). Waumini watarithi kila kitu; Mungu atakaa pamoja nao na watakuwa watoto wake (Ufunuo wa yohana 21:7). Mungu alituumba ili tuwe na ushirika naye. Mwanadamu akatenda dhambi na kuvunja ushirika huo. Mungu anarejeza uhusiano huo katika umilele na wale waliostahili mbele zake. Sasa, kuishi ukijipatia kila kitu ama chochote halafu ufe ukiwa bado katika hali ya kutengana na Mungu milele ni hasara. Lakini Mungu ametengeneza njia ya kuwezesha kila mtu kufikia tena ushirika huo wa milele (Luka 23:43), pia ameandaa ndani ya njia hiyo maisha yenye kutosheka na maana. Hali hii ya kutamanika yapatikana vipi?

MAANA YA MAISHA YAREJEZWA KUPITIA YESU KRISTO

Maana ya maisha, kama ilivyotajwa hapo awali, ya sasa na hata baadaye yapatikana katika kurejezwa kwa ushirika baina ya mwanadamu na Mungu uliopotezwa wakati wa Adamu na hawa walipoanguka dhambini. Kufikia sasa, ushirika na Mungu wawezekana kupitia mwanawe, Yesu Kristo pekee (Matendo 4:12; Yohana 1:12). Uzima wa milele hupatikana mtu anapotubu dhambi zake (kwa kukataa kuendelea katika maisha ya dhambi na kumuomba Yesu kristo amfanye kiumbe kipya) na kuanza kumtegemea Yesu kristo kama mwokozi (tazama swali “mpango wa wokovu ni nini?” kwa maelezo zaidi juu ya swala hili muhimu).

Maana halisi ya maisha haipatikani tu kwa kumpata Yesu kama mwokozi. Maana kamili ya maisha huanza wakati mtu anapochukua hatua ya kumfuata Yesu kristo kama mwanafunzi, akijifunza juu yake,akitumia wakati kusoma neno lake mara kwa mara, akishirikiana naye katika maombi na pia kumtii katika maagizo ama amri zake. Kama wewe si mmoja wa waumini (ama pengine muumini mpya) Jambo hili lazima liwe linaonekana kama mzigo kwako. Lakini soma maelezo yafuatayo:

“Njoni kwangu nyote mlichoka na kulemewa na mizigo mizito, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu na mjifunze kwangu, kwa kuwa ni mpole na mnyenyekevu wa moyo na mtapata pumziko nafsini mwenu. Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28-30). “Naam, nalikuja ili wawe na uzima na wawe nao teletele” (Yohana 10:10b). “Mtu akitaka kunifuata sharti ajikane mwenyewe na abebe msalaba wake anifuate. Kwa kuwa kila atakayejaribu kuokoa maisha yake atayapoteza, lakini atakayeyapoteza kwa ajili yangu atayapata tena” (Mathayo 16:24-25). “Furahini katika Bwana naye atawapa myatakayo mioyoni mwenu” (Zaburi 37:4).

Yale yanayozungumziwa katika aya hizi ni kwamba tuna nafasi ya kuchagua. Tunaweza kuendelea kuyaongoza maisha yetu wenyewe (huku tukipata matokeo ya maisha ya utupu) au tunaweza kuchagua kumuelekea Mungu na mapenzi yake juu ya maisha yetu kwa moyo mmoja (Itakayoleta matokeo ya maisha makamilifu, kupatikana kwa haja za moyo na kupata kutosheka). Haya yote ni kwa sababu Muumba wetu anatupenda na natutakia mema (si lazima iwe ni maisha rahisi rahisi, lakini yenye utimilifu).

Kwa kumalizia hebu nikupe kidokezo kimoja kutoka kwa rafiki yangu mchungaji. Kama wewe ni shabiki wa michezo na ukiamua kuenda kutazama mashindano ya mabingwa wa michezo, unaweza kulipa ada ndogo na ukapata nafasi ya mbali na wachezaji huko juu ya ukumbi au ulipe pesa nzuri zaidi na upatiwe nafasi ya karibu na wachezaji ili uuone mchezo vizuri. Haya ni sawa na maisha ya kikristo. Kumuona Mungu akitenda kazi maishani mwako si kwa ukristo wa kuenda kanisani tu jumapili. Huwa hujalipa gharama. Matendo haya ya Mungu ni kwa ajili ya mwanafunzi aliyejitolea moyo wake wote na ameacha kutafuta mapenzi yake ili ayatimize mapenzi ya Mungu. Hawa huwa wamelipa gharama (kwa kujisalimisha mikononi mwa kristo na kuamua kutenda mapenzi yake); wanaona maisha yao katika utimilifu na wanaweza kusimama mbele za wenzao na hata Mungu muumba wao bila kujilaumu. Je, umelipa gharama? Je, ukotayari kulipa gharama? Ikiwa ndiyo, hutaona njaa ya maana ama kusudi la maisha tena.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maana ya maisha ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries