settings icon
share icon
Swali

Maana ya jina Yesu ni gani? Jina Yesu lina maana gani?

Jibu


Ikiwa kulikuwa na jina lilijaa umuhimu, ni jina la Yesu. Biblia inasema kuwa Yesu amepewa "Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani" (Wafilipi 2:9-10). Ni kwa nini la Bwana wetu Yesu lina nguvu? Jina Yesu linamaanisha nini?

Jina Yesu, lilitangazwa kwa Yusufu na Mariamu kupitia kwa malaika (Mathayo 1:21; Luka 1:31), inamaanisha "Yawe anaokoa" au "Yawe ni wokovu." Tafsiri kutoka kwa Kiebrania na Aramaiki, jina ni Yeshua. Neno hili ni muungano wa Ya ufupisho wa Yawe, jina la Mungu wa Israeli (Kutoka 3:14); na kitenzi Yasha, kinamaanisha "nusuru" "kukomboa," au "okoa."

Jina Yesu lilikuwa maarufu katika Yudea karne ya kwanza. Kwa sababu hii, Bwana wetu mara nyingi alikuwa anaitwa "Yesu wa Nazarethi," hii ikimtofautisha na maskani yake ya utotoni, mji wa Nazarethi kule Galilaya (Mathayo 21:11, Marko 1:24, Luka 18:37; Yohana 1:45; Yohana 19:19, Matendo 2:22). Mbali na kuwa jina la kawaida, jina Yesu ni la muhimu kwa kiwango kikubwa. Yesu alitumwa na Mungu kwa kusudi Fulani na jina lake la kibinafsi linatoa ushuhuda kwa utume huo. Kama vile Yeshua/Yoshua katika Agano la Kale aliwaongoza watu wake kuwashida Wakanaani, Yeshua/Yesu katika Agano Jipya aliongoza watu wake katika kuishinda dhambi na adui wao wa kiroho.

Wagalatia 4:4-5 yasema, "Lakini wakati ule maalumu ulipotimia, Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke, akaishi chini ya sheria, apate kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria ili sisi tufanywe wana wa Mungu." Mungu alimtuma Yesu kutuokoa (Yohana 3:17). Maana ya jina la Yesu-Yawe/Mungu anaokoa- anafunua utume wake (wa kuokoa na kukomboa) na utambulisho wake kama Mwokozi wa ulimwengu. Kwa wakati huo huo, ukawaida wa jina la Yesu unaonyesha kuwa yeye ni mwanadamu na mnyenyekevu. Mwana wa Mungu alijifua utukufu wake na akawa mtu mnyenyekevu (Wafilipi 2:6-8).

Jina la Yesu in la maa kwa sababu ya maana yake na kwa sababu ya yule linawakilisha. Kunazo nguvu na mamlaka katika utu wa Kristo Yesu, hata hivyo huyo mtu anaonekena kwa jina hilo. Hasa kupita majina mengine, tunahusisha jina la Yesu na tabia yake maalum, sifa na kazi, vile inavyoonekana katika kweli za biblia zifuatazo:

Wokovu uu katika jina la Yesu pekee: "Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo" (Matendo 4:11-12; angalia pia Yohana 14:6; 20:31; Matendo 2:21; Yoeli 2:32; 1 Wakorintho 6:11; 1 Yohana 2:12).

Msamaha wa dhambi unapatika kupitia kwa jina la yesu: "Manabii wote waliongea juu yake kwamba kila mtu atakayemwamini atasamehewa dhambi zake zote kwa jina lake" (Matendo 10:43; ona pia Matendo 22:16).

Waumini wanabatizwa katika jina la Yesu: "Petro akajibu, "Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile ahadi ya Roho Mtakatifu'" (Matendo 2:38; ona pia Mathayo 28:19; Matendo 8:12, 15-16; 10:48; 19:5).

Uponyaji na miujiza zilifanywa kwa jina la Yesu: "Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote" (Matendo 3:16; ona pia aya ya 6-8 na Matendo 4:30).

Yesu anawafunza waumini kuomba katika jina lake; hiyo ni kuomba, kwa mamlaka yake, aina ya maombi ambayo angeomba yatakuwa: "Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni" (Yohana 14:13-14; ona pia Yohana 15:16; 16:23-24).

Kwa njia, miniendo yake Yesu analingana na jina lake. Jina Yesu hutukumbusha sisi nguvu, uwepo na kusudi la Kristo aliyefufuka. Linatuakikishia kuwa nia ya neema ya Mungu ya kutuokoa. Bwana wetu Yesu alimleta Mungu kwa mwanadamu na sasa anawaleta wanadamu kwa Mungu kupitia wokovu aliotununulia. Katika Biblia, wakati watu walinena au kutenda katika jina la Yesu, walifanya hivyo kama wawakilishi wa Mungu walio na mamlaka. Maisha ya muumini yeyote anafaa kuishi kwa jina la Yesu (Wakolosai 3:17) na kwa kufanya hivyo inamletea Mungu utukufu: "Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo" (2 Wathesaloniki 1:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maana ya jina Yesu ni gani? Jina Yesu lina maana gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries