settings icon
share icon
Swali

Je! Mkanamungu anaweza kuwa na maadili mema?

Jibu


Je, mkanamungu anaweza kutenda kwa njia za wema na maadili? Hakika, anaweza. Wanadamu wote bado wako na mfano wa Mungu juu yao, hata baada ya kuanguka kwa Adamu na Hawa katika dhambi. Sura ya Mungu iliathiriwa katika anguko, lakini haikufutiliwa mbali, na kwa hivyo mwanadamu bado anaelewa mema na mabaya, haijalishi wanajaribu kusema vingenevyo. Hata wakanamungu huonyesha hisia kwa ufahamu huu wa asili wa mema na mabaya, wengine hata kufikia kiwango cha kuishi maisha ya kielelezo.

C.S Lewis alieleza hili vizuri. Alifahamu kwamba ikiwa mtu anamwona mwingine akiwa hatarini, silika ya kwanza ni kukimbia ili amsaidie. Lakini sauti ya pili ya ndani inaingilia kati na kusema, “La, usijihatarishe,” ambayo inaambatana kijihifadhi. Lakini bado sauti ya tatu ya ndani inasema, “La, unafaa kusaidia.” Lewis anauliza, hiyo sauti ya tatu inatoka wapi?” hii ndio inajulikana kwetu kuwa “uhakika” wa maisha. Maadili ni kile ambacho watu hufanya, lakini wema huelezea kile watu wanapaswa kufanya. Naam, watu wanajua kile wanapaswa kufanya, lakini hiyo haimanishi kwamba kila mara wao hutenda kadri na ufahamu huo.

Tofauti kati ya mkanamungu na Mkristo katika hali hii ni kwamba mkanamungu anaweza kutenda kimaadili kwa ajili ya sababu fulani (kwa mfano, kwa kutotaka kwenda jela, kuvuruga utaratibu wa kijamii, hii huwafanya waonekane wema kwa watu, nk”, lakini hana sababu kuu ya kimaadili ya kutenda hivyo kwa sababu hamna mamlaka kuu ya kimaadili ambayo yako juu ya kila nyanja ya maisha yake. Bila mamlaka hii kuu, kila mkanamungu hufafanua maadili kwa maneno yake mwenyewe, ijapokuwa maadili yake yameathiriwa na yale maadili ya Mungu yaliyosalia kutokana na mfano wa Mungu ndani yake, pamoja na mfumo na vizuizi vya utamaduni na jamii ambamo mkanamungu anaishi.

Mkristo kwa upande mwingine anatenda kiadili kutokana na ufahamu wa sheria ya maadili iliyotolewa na Mungu katika Neno Lake na upendo kwa Mtoa-Sheria Mwenyewe. Zaidi ya hayo, ufahamu huzidi kuongezeka na kubinafsishwa na Roho wa Mungu anayekaa ndani yake, ambaye jukumu lake ni la kumleta Mkristo “katika kweli” (Yohana 16:13). Kutoka ndani ya muumini, Anaelekeza, kuongoza, kufariji na kutushawishi, vile vile kukuza ndani yetu matunda ya Roho (Wagalatia 5:22-23). Kwa mkanamungu ambaye hana Roho, ukweli wa Mungu ni “upumbavu” kwa sababu hii “hutambulika kiroho” (1 Wakorintho 2:14), na tunda pekee la uadilifu ni uadilifu wa kibinafsi, na sio uadilifu wa Kristo.

Wanapokabiliwa na hali ambayo inayomhitaji Mkristo na mkanamungu kufanya uamuzi wa kiadili, hali ambayo vikwazo vya kijamii vimeondolewa, itikio la kila mmoja litakuwa tofauti sana. Kwa mfano, ikiwa jamii inaonekana kukubali kiadili kuua watoto ambao hawajazaliwa, mkanamungu hataona sababu ya kupinga tendo hilo. Sheria yake mwenyewe ya kiadili inamwambia zaidi kuwa ni jambo la huruma kufanya ikiwa mimba ilikuwa kwa sababu ya ubakaji au kujamiiana. Huku Mkristo akijua kwamba uavyaji mimba ni makosa kwa sababu chaguo la maadili yake inategemea sheria ya mtoa maadili ambaye ametangaza uhai wote wa wanadamu kuwa wa mtakatifu kwa sababu umeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mtoa-Sheria ametangaza, “Usiue” (Kutoka 20:13) na kwa Mkristo, hio ndiyo mwisho wa jambo hilo.

Kwa hivyo mkanamungu anaweza kutenda kiadili? Kwa hakika ndio, lakini hana sababu kuu ya kufanya hivyo na hana mamlaka kuu ya kuiga ili ahakikishe mapito yake yamenyooka na hayana ulegevu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkanamungu anaweza kuwa na maadili mema?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries