settings icon
share icon
Swali

Je, maadili ya Kiyahudi-Kikristo ni nini?

Jibu


Neno “Uyahudi-Ukristo” linamaanisha kitu ambacho kina chanzo chake katika misingi ya kawaida ya Uyahudi na Ukristo. Biblia inajumuisha Maandiko ya Kiyahudi ya Agano la Kale, kwa hiyo misingi ya maadili iliyowekwa katika Uyahudi yameimarishwa katika Ukristo. Matumizi ya kwanza ya neno “maadili ya Kiyahudi-Kikristo” yalionekana na mwanafalsafa Mjerumani Friedrich Nietzsche katika kitabu chake cha 1888 The Antichrist: Curse on Christianity (Mpinga Kristo: Laana kwa Ukristo). Matumizi ya awali ya neno “maadili ya Kiyahudi-Kikristo” yalirejelea mizizi ya Kiyahudi na utambulisho wa kanisa la kwanza la Kikristo, lakini halikutumiwa kuzungumzia kundi la uadilifu hadi pale wakati wa baadaye.

Mnamo 1952 Rais mteule Dwight Eisenhower, akizungumza na Wakfu wa Uhuru huko New York, alisema, “Hisia zetu za serikali hazina maana isipokuwa zimeanzishwa katika imani ya kidini, na sijali hiyo ni nini. Kwetu ijapokuwa ni dhana ya Kiyahudi-Kikristo, lakini lazima iwe dini ambayo watu wote wameumbwa sawa.” Hii ilianzisha matumizi ya kisasa ya neno hilo katika duru za kisiasa na kijamii za Marekani. Tangu siku za Eisenhower hadi sasa, neno hili limehusishwa haswa na wahafidhina wa kisiasa huku Marekani, ingawa kuna matumizi mapana zaidi. Katika shule zetu za kijeshi za Marekani, inafundishwa kwa kawaida kwamba kanuni za kisasa za vita, kama vile ulinzi wa mateka na wasio wapiganaji, zinatokana na mada za Biblia, Utawala wa Kimarekani umeegemezwa katika maadili ya Kiyahudi-Kikristo na husherehekea ukweli huo kwa kazi mbalimbali za sanaa kote Washington, D.C. Katika Baraza la wawakilishi kuna picha 23 za usaidizi wa marumaru za watoa sharia wakuu, akiwemo Musa, ambaye anapewa kipaumbele sana. Sanamu zilizo juu ya lango kuu la jengo la Mahakama Kuu zimeelekezwa kwa Musa akiwa na zile Amri Kumi, na kuna viwakilishi vingine kadhaa vya Musa na Amri Kumi katika sehemu mbalimbali kote katika jengo hilo.

Ingawa kuna vipengele vingi vya maadili ya Kiyahudi-Kikristo, baadhi ya yale ya kawaida zaidi ni utakatifu wa maisha ya binadamu, wajibu wa kibinafsi, heshima kubwa kwa ndoa, na huruma kwa wengine. Mengi ya yale yaliyo bora zaidi katika ustaarabu wa Magharibi yanaweza kuhisika moja kwa moja na maadili ya Kiyahudi-Kikristo. Mwanahistoria Thomas Cahill, akionyesha mada za pamoja za Ukristo na Uyahudi alisema, “Kiini cha Torati sio utiiivu kwa kanuni kuhusu utaratibu maalum wa chakula-chenye mtu anaweza kula, mtu mwenye anaweza kula naye, jinsi mtu anaweza jitayarisha kabla ya chakula-lakini kwa tzedakka, haki kama vile haki ya Mungu, haki kwa waliokandamizwa.” Misingi ya maadili ya Kiyahudi-Kikristo inaweza kufupishwa katika “Kanuni ya Dhabihu” ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake katika Mathayo 7:12 “Kwa hiyo chochote mnachotaka mtendewe na watu, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii ndiyo Sheria na Manabii.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, maadili ya Kiyahudi-Kikristo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries