settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema kuhusu jinsi ya kupata lengo la maisha?

Jibu


Bibilia iko wazi kuhusu vile lengo linastahili kuwa katika maisha. Wanadamu katika Agano La Kale na Agano Jipya walitafuta na kugundua lengo la maisha yao. Suleimani mtu mwenye hekima sana ambaye aliishi, kugundua lisilo leta maana katika maisha wakati peke tutakavyoishi kulingana na ulimwengu huu. Anapeana wosia huu wa mwisho katika kitabu cha Mhubiri: “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya” (Mhubiri 12:13-14). Suleimani anasema maisha yote ni kumheshimu Mungu na mawazo yetu na maisha na kuzitunza amri zake, kwa maana siku moja tutasimama mbele yake kwa hukumu. Sehemu ya lengo letu katika maisha ni kumcha Mungu ana kumtii.

Sehemu nyingine ya lengo letu ni kuyaona maisha katika dunia hii kwa taswira. Kuliko wale angazo lao liko katika maisha haya, Mfalme Daudi alitafuta ridhisho katika wakati uchao. Alisema, “Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Naimkapo nishibishwe kwa sura yako”( Zaburi 17:15). Kwa Daudi ridhisho itakuja siku ile wakati ataamka (katika maisha yafuatayo) huku akishika uso wa Mungu (kuwa na ushirika nawe) na kuwa kama Yeye ( 1 Yohana 3:2).

Katika Zaburi 73, Asafu anazungumza jinsi alivyojaribiwa kuwatia wivu wale waliononekana kutojali na kujenga juu ya falsafa zao katika mabega yao kwa wale waliojinufaisha kwa niaba yaw engine, lakini alichunguza hatima yao. Kwa ulinganisho wa yale waliyo yafatufa, anasema, katika aya ya 25 chenye kilisumbua sana: “Ni nani niliye naye mbinguni; Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.” Kwake Asafu uhusiano na Mungu ulikuwa jambo kubwa sana kuliko kitu cho chote katika maisha. Bila huo uhusiano, maisha kweli hayana lengo.

Mtume Paulo alizungumza juu ya yale yote aliyoyapokea kutoka kwa dini za vikao kabla akutane na Kristo aliyekuwa amefufuka, na anatamatisha kuwa yote yalikuwa kama mlima wa mbolea akilinganisha uzuri wa hekima ya Kristo Yesu. Katika Wafilipi 3:9-10, Paulo anasema kuwa hataki kitu kingine zaidi kuliko kumjua Kristo na “kupatikana ndani yake” kuwa na utakatifu wake na kuishi kwa Imani ndani yake, hata kama ingemaanisha kuwa angepata mateso na kufa. Lengo la Paulo ilikuwa kumjua Kristo, kuwa na utakatifu unaopatikana kupitia kwa imani kupitia ndani yake, na kuishi katika ushirika na Yeye, hata wakati hayo yangeleta matezo ( 2 Timotheo 3:12). Hatimaye, alitazamia wakati ambao atakuwa mmojawapo wa watakao “fufuka kutoka kwa wafu.”

Lengo letu katika maisha, vile Mungu alivyokwisha tuumbia awali ni 1) kumtukuza Mungu na kufurahia ushirika na Yeye, 2) kuwa na uhusiano mwema na wengine, 3) tufanye kazi, na 4) tuwe na mamlaka juu ya nchi. Lakini kwa kuanguka kwa mwanadamu katika dhambi, ushirika na Mungu umevunjwa, uhusiano na wengine umearibika, kazi kila mara inaoneka kuwa ya shida, na mwanadamu anataabika kutunza mamlaka juu ya anga. Ni kupitia kwa urejesho na Mungu peke, kupitia kwa imani katika Yesu Kristo, lengo katika maisha linaweza gunduliwa.

Lengo la mwanadamu ni kumtukuza Mungu na kumfurahisha milele. Tunamtukuza Mungu kwa kumwogopa na kumtii, kwa kuangazia ule mji uajo kutoka mbinguni, na kumjua kwa ukaribu sana. Tunamfurahia Mungu kwa kufuata lengo lake katika maisha yetu, ambayo inatuwezesha kuwa na furaha isiyo na mwisho- wingi wa maisha ambaye anataka tuwe nayo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema kuhusu jinsi ya kupata lengo la maisha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries