settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuvunja laana za kizazi?

Jibu


Biblia inataja "laana za kizazi" katika maeneo kadhaa (Kutoka 20: 5, 34: 7; Hesabu 14:18; Kumbukumbu la Torati 5: 9). Inaonekana kuwa halali kwa Mungu kuwaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao. Hata hivyo, hii ni kuitizama kutoka mtazamo wa kidunia. Mungu anajua kwamba madhara ya dhambi hupunguzwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Wakati baba ana maisha ya dhambi, watoto wake huendelea pia kuwa na tabia sawa ya dhambi. Kwa hiyo Mungu hatakuwa asiye mwenye haki kwa kuadhibu dhambi kwa kizazi cha tatu hadi cha nne — kwa sababu wanafanya dhambi sawia na baba zao. Lakini wanaadhibiwa kwa dhambi zao wenyewe, sio dhambi za baba zao. Biblia inatuambia waziwazi kwamba Mungu hawachukulii watoto kuwajibika kwa ajili ya dhambi za wazazi wao (Kumbukumbu la Torati 24:16).

Kuna mwenendo katika kanisa hii leo wa kujaribu kulaumu kila dhambi na shida kwa aina fulani kuwa ni laana ya kizazi. Hii sio kibiblia. Zuluhisho la laana za kizazi ni wokovu kupitia Yesu Kristo. Tunapokuwa Wakristo, sisi huwa kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17). Je! Mtoto wa Mungu anawezaje kuwa chini ya laana ya Mungu (Waroma 8: 1)? Kwa hiyo, tiba, kwa "laana ya kizazi" ni imani katika Kristo na maisha yaliyowekwa wakfu kwake (Warumi 12: 1-2).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuvunja laana za kizazi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries