settings icon
share icon
Swali

Kwa nini nisijiue?

Jibu


Nia yangu inawalenga wale ambao wana azima ya kujiua. Ikiwa ni wewe saa hii, moyo wako unaweza kukuambia mambo mengi na kukujaza hisia kama kukata tamaa maishani. Waweza kujihisi kama umo ndani ya shimo refu na hakuna matarajio yoyote juu yakutoka kwako humo. Hakuna mwenye kukujali wala kutaka hata kukuelewa katika hali zako unazopitia.maisha ni kama hayana umuhimu wa kuyaishi je upo?

Hisia za kuvunja moyo huwapata wengi mara kwa mara. Maswali yaliyonijia nilipokuwa katika shimo hilo la kihisia yalikuwa, “je haya ni mapenzi ya Mungu aliyeniumba?” “Je, Mungu ni mdogo sana kiasi cha kuwa hawezi kunisaidia?” “Je, shida zangu ni kubwa sana kuliko uwezo wa Mungu?”

Ninafuraha kukujulisha ya kwamba, kama utachukua wakati kiasi umfanye Mungu awe Mungu halisi maishani mwako saa hii atadhihirisha ukuu wake! Kwa kuwa hakuna kisichowezekana kwa Mungu” (Luka 1:37). Pengine makovu kutika majeraha ya kitambo yapo na yamekuachia kutokubalika ama kukataliwa hasa. Hii inaweza kusababisha kujionea huruma, hasira, uchungu, mawazo ya kisasi, uoga na kadhalika, na huenda ikawa imesababisha shida katika uhusiano wako muhimu. Hata hivyo kujiua kutasaidia tu kuleta huzuni na upweke kwa wale wakupendao ambao hukutaka kuwaudhi wala wahuzunike na kusababisha Makovu mengine ambayo yatadumu maishani mwao mwote.

Kwa nini usijiue? Rafiki yangu,haijalishi mambo ni mabaya kiasi gani maishani mwako,kuna Mungu wa upendo anayekungojea. Mruhusu akuongoze kuvuka hali hiyo ya kukata tamaa na akufikishe katika uhalisi wa nuru yake. Yeye ni tumaini lako la uhakika. Jina lake ni Yesu.

Huyu Yesu, mwana wa Mungu Mtakatifu anafanana nawe katika hali hii ya kukataliwa na kudhalilishwa. Nabii Isaya aliandika juu yake na kusema, “Hana umbo wala thamani hata tumtazame. Wala sura ya kuvutia hata tuvutiwe naye. Alidharauliwa na kukataliwa na watu. Mtu mwenye huzuni ajuaye sikitiko na kama mmoja wa wengine ambao wanadamu huzuia nyuso zao wasiwaone akadharalauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Kwa hakika alijitwika fadhaa zetu nasi tukamdhania kuwa amepigwa na Mungu na kuteswa. Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya dhambi zetu; aliumizwa kwa uovu wetu na Kwa kupigwa kwake tumepona. Sote kama kondoo tumepotea. Kila mmoja amefuata njia yake. Lakini bwana amem’bebesha uovu wetu sote” (Isaya 53:2-6).

Rafiki yangu, haya yote Yesu aliyavumilia ili dhambi zako zote zipate kusamehewa! Haijalishi unabeba kiasi gani cha mzigo wa hukumu moyoni mwako atakusamehe ukitubu kwa unyenyekevu (toka dhambini umgeukie Mungu). “Niite siku ya dhiki. Nitakuokoa (na kukuweka huru), nawe utanitukuza (Zaburi 50:15). Hakuna chochote ulichokifanya ambacho Yesu ni vigumu kusamehe. Baadhi ya watumishi wake wazuri katika biblia walitenda dhambi kubwa kama kuua (Musa) kuzini (Mfalme Daudi) na kutesa wengine (mtume Paulo). Na wakapata msamaha na uzima tele wa milele katika Bwana. “Nioshe kabisa uovu wangu na pia unioshe dhambi zangu” (Zaburi 51:2). “ Kwa hivyo, mtu akiwa ndani ya kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya” (Wakorintho wa pili 5:17).

Kwa nini usijiue? Rafiki yangu, Mungu yuko tayari kukiunda upya kile “kimevunjika”… kama yale maisha uliyonayo sasa unayotaka kuyamaliza kwa kujiua. Nabii Isaya aliandika: “Roho wa bwana yu juu yangu,kwakuwa bwana amenipaka mafuta niwahubiri habari njema watesekao; amenituma kuwarejeza waliovunjika moyo, kutangaza kuachiliwa kwao waliotekwa na kufunguliwa kwao waliofungwa….. kuwafariji wote waombolezao; kuwapatia wale waombolezao…taji la urembo badala ya jivu; mafuta ya furaha badala ya kuomboleza; taji la shangwe badala ya roho iliyozimia. Nao wataitwa miti ya haki, mapando ya Mungu ili atukuzwe” (Isaya 61:1-3).

Njoo kwa Yesu, ili akuregeshee furaha na umuhimu wako huku ukimtumainia yeye kuanza kazi mpya maishani mwako. “Nirudishie furaha ya wokovu wako na unipe roho ya kukubali. “Bwana fungua kinywa changu ili nikatangaze sifa zako. Kwa kuwa wewe hupendezewi nadhabihu, maana ningekutolea; hufurahishwi na sadaka za kuteketeza. Dhabihu za Mungu ni moyo uliopondeka, moyo uliovunjika na mnyenyekevu, Mungu hataudharau” (Zaburi 51:12, 15-17).

Je, utampokea Bwana kama mwokozi na mchungaji wako? Ataongoza njia zako,na mawazo yako, siku moja moja kila mara, kupitia Neno lake Biblia. “nitakuongoza na kukufundisha katika njia ile ambayo ni uiendee. Nitakushauri na jicho langu likiwa juu yako” (Zaburi 32:8). “naye atakuwa tegemeo la nyakati zako; utajiri wa wokovu,hekima na maarifa; kumhofu Bwana ndiyo hazina yake” (Isaya 33:6). Ndani ya Kristo, utakuwa na mapambano pia, lakini sasa utakuwa na TUMAINI. Yeye ni “Rafiki akaaye karibu mno kuliko ndugu yako” (Methali 18:24). Neema ya Bwana Yesu kristo iwe nawe majira haya unayofanya uamuzi wako.

Ukiwa unatamani kumwamini Yesu kristo awe mwokozi wa maisha yako, sema maneno haya moyoni mwako kwa Mungu. “Mungu, ninakuhitaji maishani mwangu. Tafadhali nisamehe kwa yale yote nimetenda. Ninaweka imani yangu kwa Yesu sasa na ninaamini kuwa yeye ni mwokozi wangu. Tafadhali nisafishe, uniponye na unirudishie furaha ya maisha yangu. Ahsante kwa kunipenda na Yesu kufa kwa ajili yangu.”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini nisijiue?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries