settings icon
share icon
Swali

Kwa nini kuoleka?

Jibu


Tamaduni nyingi ulimwenguni leo zinapoteza ufahamu wa jinsi ndoa ilipaswa kuwa. Tunaishi katika ulimwengu ambao unasema tunapaswa kupata kile tunachotaka njia yoyote tunaweza kuipata. Ndoa wakati mwingine huonekana kama kufungwa ambako kunaweza kuharibu uwezo wetu wa kuwa na kile tunachotaka wakati tunapokitaka. Ndoa leo wakati mwingine hudhihakiwa kama taasisi ya kale ambayo imepoteza umuhimu wake.

Ndoa ni nini? Je, imepitwa na wakati? Ni muhimu kutambua kwanza kwamba ndoa si dhana ya mwanadamu. Mungu alipomumba mtu wa kwanza kwa mfano wake mwenyewe (Mwanzo 1:27; 2: 7), Alimpa mtu huyo kila kitu ambacho alihitaji ili kuridhika. Lakini, Mungu alisema,"Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye." (Mwanzo 2:18). Kwa hivyo Mungu aliumba mwanamke kutoka ubavu wa Adamu na kumleta kwa mtu huyo. Ndoa ya kwanza ilitokea wakati Mungu alimuumba mwanamke kukamilisha mahitaji ya mwanaume ili wanapounganakatika agano, wawe mwili mmoja. Wazo la "mwili mmoja" linamaanisha muhuri wa kudumu. Yesu alipoulizwa kuhusu talaka, Akajibu, "Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe."(Mathayo 19: 5-6) Tazama kwamba ni Mungu ambaye huunganisha na mwanamume na mwanamke katika ndoa. Katika Malaki 2:14, Mungu anatukumbusha kwamba alikuwa" shahidi kati yako na mke wa ujana wako. "Mungu huchukulia ndoa kwa uzito sana.

Ndoa ilikuwa taasisi ya kwanza ambayo Mungu aliumba. Ilikuwa kabla ya kuanzishwa kwa kanisa ama au serikali. Ndoa ilikuwa taasisi ya kwanza ya kijamii. Binadamu kwa kawaida hufanya kazi bora wakati wanaunganishwa katika njia njema kwa wengine, na mpango wa Mungu wa ndoa ni kuanzisha familia imara. Biblia ina maagizo mengi kwa wajumbe kuhusu jinsi wanapaswa kutendea wengine ili mahitaji ya kihisia kutimizwa(Waefeso 5: 21-33; 6: 1-4; Wakolosai 3: 18-21; 1 Wakorintho 7: 2-5 , 10-16). Mungu aliunda ndoa kuwa ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja kwa maisha yote, na kupotoka kutoka kwa mpango huo ni kupotosha nia yake (Mathayo 19: 8; Warumi 1: 26-27).

Wakorintho wa Kwanza 7: 1-2 inatupa sababu nzuri ya kuolewa: " ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

"Mungu alikusudia ngono ifurahikiwe tu ndani ya mipaka ya ndoa .. Shughuli yoyote ya ngono nje ya mipaka hiyo ni dhambi (Wagalatia Wakolosai 3: 5) Kama mtu ana hisia zaidi ya ngono, mara nyingi ni wazo nzuri kuoleka ili kupunguza tamaa na kuepuka maovu(Yakobo 1: 13-15). Kushiriki ngono na mtu ambaye sio mkewe mumewe ni dhambi na husababisha maumivu na maafa (Methali 6: 26-29; 1 Wakorintho 6:18).

Hata hivyo, hakuna amri katika Maandiko kwamba kila mtu lazima aoleke. Kwa kweli, mtume Paulo alichagua kutooa kama njia ya kujitoa kwa muda zaidi kumtumikia Mungu (1 Wakorintho 7: 7-9, 32-35). Kuna baadhi ambao hawana hisia ya kuolewa, na hakuna kitu kibaya na jambo hilo. Watu wa watawa wanaweza kuwa na maisha yenye kutimiza na kupata msaada wa kihisia kwa marafiki, familia, na huduma. Hata hivyo, jamii yetu imeanza kulinganisha utawa na uasherati, na hiyo ni mbaya sana. Paulo aliunga utawa hivyo kwamba mtu apate kuzingatia kabisa mambo ya Kristo. Utawa haupaswi kamwe kutumika kama sababu ya kuishi katika dhambi ya ngono. Lakini ikiwa mtawa anaweza kudhibiti tamaa zake na kuishi maisha safi, hakuna haja ya kujisikia kulazimishwa kuolewa (1 Wakorintho 7:37).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini kuoleka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries