settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu hutujaribu?

Jibu


Tunapouliza kwa nini Mungu anatujaribu au anaruhusu tujaribiwe, tunakubali kwamba kujaribiwa kwa kweli hutoka kwake. Wakati Mungu anajaribu wana Wake, Anafanya kitu muhimu. Daudi alitaka kujaribiwa kwa Mungu kumuuliza kuchunguza moyo wake na akili kuona kwamba zinamstahili yeye, (Zaburi 26: 2, 139: 23). Wakati Ibrahimu alijaribiwa na Mungu katika suala la kumtoa dhabihu Isaka, Abramu alitii (Waebrania 11: 17-19) na alionyesha kwa ulimwengu wote kwamba yeye ni baba wa imani(Warumi 4:16).

Katika Agano la Kale na Jipya, maneno yaliyotafsiriwa "mtihani" inamaanisha "kuthibitisha kwa majaribio." Kwa hivyo, wakati Mungu anajaribu watoto Wake, kusudi lake ni kuthibitisha kwamba imani yetu ni halisi. Sio ya kwamba Mungu anahitaji kujithibitisha yeye mwenyewe kwa vile anajua vitu vyote, lakini Yeye anatuhakikishia kwamba imani yetu ni halisi, kwamba sisi ni watoto Wake kweli, na kwamba hakuna jaribio litashinda imani yetu.

Katika mfano Wake wa Mkulima(mpanzi), Yesu anawatambua wale ambao huanguka kama wale wanaopokea mbegu ya Neno la Mungu kwa furaha, lakini, mara tu wakati wa majaribio unapokuja, huanguka. Yakobo anasema kwamba kujaribiwa kwa imani yetu huendeleza uvumilivu, ambayo inasababisha ukomavu katika safari yetu na Mungu (Yakobo 1: 3-4). Yakobo anaendelea kusema kwamba kujaribiwa ni baraka, kwa sababu, wakati majaribio yameisha na "tumesimama," tutapata ,"heri mtu astahimiliye majaribu;kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima,Bwana aliyowaahidia wampendao".(Yakobo 1: 12). Majaribio yanatoka kwa Baba yetu wa mbinguni ambaye anafanya kazi zote kwa ajili ya wema kwa wale wanaompenda na ambao wanaitwa kuwa watoto wa Mungu (Warumi 8:28).

Upimaji au majaribio tunayopata huja kwa njia mbalimbali. Kuwa Mkristo mara nyingi hutuhitaji tuondoke katika maeneo yetu ya faraja na kwenye haijulikani. Uvumilivu katika majaribio uleta ukuaji wa kiroho na ukamilifu. Ndio maana Yakobo aliandika, "Ndugu angu,hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali" (Yakobo 1: 2). Ujaribio wa imani unaweza kuja kwa njia ndogo na muwasho wa kila siku; zianaweza pia kuwa na mateso kali (Isaya 48:10) na mashambulizi kutoka kwa Shetani (Ayubu 2: 7). Chochote chanzo cha majaribio, ni kwa manufaa yetu kupitia majaribio ambayo Mungu anaruhusu.

Akaunti ya Ayubu ni mfano mkamilifu wa Mungu kuruhusu watakatifu wake kujaribiwa na Ibilisi. Ayubu aliyashinda majaribio yake kwa uvumilivu na "katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi,wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu" (Ayubu 1:22). Hata hivyo, akaunti ya kujaribiwa kwa Ayubu ni ushahidi kwamba uwezo wa Shetani wa kutujaribu ni mdogo na udhibiti wa Mungu wa uhuru. Hakuna pepo anayeweza kutujaribu au kututesa zaidi ya kile ambacho Mungu amechagua. Majaribio yetu yote yanafanya kazi kwa kusudi la Mungu kamili na faida yetu.

Kuna mifano mingi ya matokeo mazuri ya kujaribiwa. Mtunga-zaburi anafananisha majaribio yetu kama kusafishwa kwa fedha (Zaburi 66:10). Petro anazungumzia imani yetu kama "ya thamani zaidi kuliko dhahabu," na ndiyo maana "tunateswa huzuni katika kila aina ya majaribu" (1 Petro 1: 6-7). Katika kujaribu imani yetu, Mungu hutufanya kukua kuwa wanafunzi wenye nguvu ambao wanaishi kwa imani na bali si kwa kile tunachokiona (2 Wakorintho 5: 7).

Tunapopatwa na dhoruba za uzima, tunapaswa kuwa kama mti ambao huchimba mizizi yake kwa undani ardhini ili kushikilia vizuri. Tunapaswa "kuchimba mizizi yetu" kwa undani zaidi katika Neno la Mungu na kushikamana na ahadi zake ili tuweze kukabiliana hali yoyote ya dhoruba inayotupinga.

Faraja kwa zote ni kuwa, tunajua kwamba Mungu hatatuacha kamwe kujaribiwa zaidi ya kile tunaweza kushughulikia kwa nguvu Yake. Neema yake inatosha kwetu, na nguvu zake hufanyika kamili katika udhaifu wetu (2 Wakorintho 12: 9). "Ndo maana, Paulo alisema," kwa hiyo napendezwa na udhaifu ,na ufidhuli ,na misiba,na adha,na shida,kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. "(2 Wakorintho 12:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu hutujaribu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries