settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuzaliwa upya?

Jibu


Dhana ya kuzaliwa upya haina msingi kabisa katika Biblia, ambayo inatuambia wazi kwamba tunakufa mara moja na kisha kuhukumiwa (Waebrania 9:27). Biblia haijataja kamwe watu kuwa na nafasi ya pili katika maisha au kurudi kama watu tofauti au wanyama. Yesu alimwambia mhalifu msalabani, "Leo utakuwa pamoja nami katika paradiso" (Luka 23:43), sio "Utakuwa na nafasi nyingine ya kuishi maisha duniani." Mathayo 25:46 inatuambia waziwazi kwamba waumini huenda kuishi katika uzima wakati wasioamini wanaendelea adhabu ya milele. Kuzaliwa upya tena imekuwa imani maarufu kwa maelfu ya miaka, lakini haijawahi kukubaliwa na Wakristo au wafuasi wa Kiyahudi kwa sababu ni kinyume na Maandiko.

Kifungu kimoja ambacho baadhi watu huthibitisha kama ushahidi wa kuzaliwa upya ni Mathayo 17: 10-12, ambayo huunganisha Yohana Mbatizaji na Eliya. Hata hivyo, kifungu hicho hakisemi kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa Eliya aliyezaliwa tena lakini kwamba angetimiza unabii wa kuja kwa Eliya ikiwa watu walikuwa wameamini maneno yake na hivyo wakamwamini Yesu kama Masihi (Mathayo 17:12). Watu hasa walimwuliza Yohana Mbatizaji ikiwa alikuwa Eliya, na akasema, "La, si mimi" (Yohana 1:21).

Imani ya kuzaliwa upya ni jambo la kale na ni dhana kuu kati ya mila ya kidini ya Hindi, kama vile Uhindu, Sikizimu , na Janizimu. Wapagani wengi wa kisasa pia wanaamini kufufuliwa tena na vilevile harakati za kisasa, pamoja na wafuasi wa roho. Kwa Mkristo, hata hivyo, bila shaka: kuzaliwa upya sio kibiblia na lazima itupiliwe mbali kama uongo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuzaliwa upya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries