settings icon
share icon
Swali

Je! Sisi sote tumezaliwa tukiwa wenye dhambi?

Jibu


Naam Biblia inafundisha kwamba sisi sote tumezaliwa watenda dhambi tukiwa na asili ya dhambi na ubinafsi. Isipokuwa tuzaliwe mara ya pili kwa Roho wa Mungu, kamwe hatutauona ufalme wa Mungu (Yohana 3:3).

Wanadamu wamepotoka kabisa; yaani sisi sote tuna asili ya dhambi ambayo huathiri kila sehemu yetu (Isaya 53:6; Warumi 7:14). Swali ni, je, asili ya dhambi ilitoka wapi? Je, tulizaliwa tukiwa wenye dhambi, au tulichagua tu kuwa watenda dhambi muda fulani baada ya kuzaliwa?

Tunazaliwa tukiwa na asili ya dhambi, na tuliirithi kutoka kwa Adamu. “Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Kila mmoja wetu aliathiriwa na dhambi ya Adamu; hakuna ubaguzi. “kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote” (aya ya 18). Sisi sote ni wenye dhambi, na sisi sote tunashiriki hukumu moja, kwa sababu sisi sote ni watoto wa Adamu.

Maandiko yanaonyesha kwamba hata watoto wana asili ya dhambi, ambayo inaunga mkono ukweli kwamba sisi sote tumezaliwa wenye dhambi. “Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto” (Mithali 22:15). Daudi anasema, “Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu” (Zaburi 51:5). “Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao, toka tumboni mwa mama zao ni wakaidi na husema uongo” (Zaburi 58:3).

Kabla hatujaokolewa, “Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu” (Waefeso 2:3). Kumbuka kwamba tulistahili ghadhabu ya Mungu sio kwa sababu ya matendo yetu, bali kwa sababu ya asili yetu. Asili hiyo ndiyo tulirithi kutoka kwa Adamu.

Tunazaliwa tukiwa wenye dhambi na kwa sababu hiyo hatuwezi kufanya mema ili kumpendeza Mungu katika hali yetu ya asili, au mwili: “Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu” (Warumi 8:8). Tulikuwa wafu katika dhambi zetu kabla Kristo hajatufufua kwa uzima wa kiroho (Waefeso 2:1). Hatuna karama yoyote nzuri ya kiroho.

Hakuna mtu anayepaswa kumfundisha mtoto kunena uongo; badala yake, ni lazima tujitahidi kwa hatua kushawishi watoto kuhusu thamani ya kusema ukweli. Watoto wachanga kwa asili ni wabinafsi, na wao kwa kuzaliwa ingawa kimakosa wanaelewa kuwa kila kitu ni “chake.” Tabia ya dhambi huja kwa kawaida kwa watoto wadogo kwa sababu wanmezaliwa wenye dhambi.

Kwa sababu tulizaliwa wenye dhambi, ni lazima tupate kuzaliwa mara ya pili, kiroho. Tumezaliwa mara moja katika familia ya Adamu na kwa asili sisi ni wenye dhambi. Wakati tumezaliwa mara ya pili, tunazaliwa kwa familia ya Mungu na kupewa asili ya Kristo. Tunamsifu Bwana kwa kuwa “Wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Hawa ndio wasiozaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu” (Yohana 1:12-13).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Sisi sote tumezaliwa tukiwa wenye dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries