settings icon
share icon
Swali

Je! Watu wote wamezaliwa wakiwa wema?

Jibu


Kunayo imani ya kawaida hii leo kwamba watu huzaliwa wakiwa “wema” na watu wengi hubakia kuwa wema moyoni maishani mwao yote. Kulingana na nadharia hii, uovu ambao watu fulani huonyesha ni matokeo ya mambo ya kimazingira-watu hubadilika na kuwa “waovu” wakati nguvu za nje zilizo nje ya uwezo wao zinapowapotosha kutoka kwa wema wao wa kimsingi. Huu ni mtazamo wa uongo, usio wa kibiblia wa asili ya mwanadamu.

Biblia inafundisha kwamba hakuna hata mmoja wetu aliye mwema. Sisi sote tumezaliwa na hali ya kutenda dhambi na ya ubinafsi tuliyorithi kutoka kwa Adamu. Tusipozaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu, hatutauona ufalme wa Mungu kamwe (Yohana 3:3).

Zaburi 14:2-3 inapinga wazo kwamba mtu yeyote ni “mwema”: “Bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja.” Ongeza kwa maneno haya kauli ya Yesu kwamba “Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake” (Luka 18:19), na tunaona kwamba sisi sote tuna hatia mbele za Mungu.

Hapo mwanzo, Mungu aliumba ulimwengu mkamilifu. Mungu aliita uumbaji wake kuwa “mzuri sana” katika Mwanzo 1:31. Bustani mwa Edeni ilikuwa mazingira mazuri kwa wanadamu wa kwanza, Adamu na Hawa. Hata katika mazingira hayo makamilifu, mahitaji yao yote yakikidhiwa na kuishi katika hali ya kutokuwa na hatia, Adamu alichagua kutomtii Mungu. Adamu hangeweza kulaumu mambo ya kimazingira kwa chaguo lake la dhambi; ilikuwa tu kitendo cha mapenzi yake kuasi.

Wakati Adamu alimwasi Mungu, wanandoa wa kwanza walipoteza kule kutokuwa na hatia, walifukuzwa kutoka Bustani na la muhimu zaidi, asili yao ya msingi ilipotoshwa (Mwanzo 3:7-12). Dhambi na kifo vikawa sehemu ya uumbaji. Baadaye, Adamu alipopata mtoto wa kiume, Biblia inaeleza tukio hilo kwa njia hii: “alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake” (Mwanzo 5:3). Kama baba, kama mwana. Mwenye dhambi alimzaa mwenye dhambi. Sasa dhambi ya Adamu imeenea kwa viumbe wote: “Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wametenda dhambi” (Warumi 5:12).

Watu hawazaliwi wakikiwa “wema” kwa sababu kila mmoja wetu ameathiriwa na dhambi ya Adamu; hakuna ubaguzi. Andiko la Warumi 5:18 linasema kwamba “Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote.” Sisi ni wenye dhambi kwa sababu mbili: sisi weneye tunatenda dhambi (sisi ni watenda dhambi kivitendo), na tunatwaa tabia ya dhambi iliyopitishwa kutoka kwa Adamu (sisi ni wenye dhambi kwa asili). Hiyo ndio maana sisi sote tunakabiliwa na kifo cha kimwili: “Katika Adamu watu wote wanakufa” (1 Wakorintho 15:22).

Ni vigumu kuwaza kuwa mtoto mzuri, asiye na hatia kuwa mwenye mwenye dhambi, lakini Biblia inaonyesha kwamba hata watoto wana asili ya dhambi. Kimantiki, ikiwa asili yetu ya dhambi imerithiwa kutoka kwa Adamu, basi lazima watoto wachanga wawe na mwelekeo wa kutenda dhambi. “Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto” (Mithali 22:15). Kuimarisha kikamilifu ukweli wa mithali hii, tabia ya mtoto yenye asili ya dhambi inaanza kujitokeza yenyewe mapema sana katia ukuaji wake; pindi tu mtoto ataanza kung’amua kati ya utiifu na kuasi, ataanza “kuijaribu” kuasi. Kiasili watoto ni wabinafsi, na tabia yao ya upotovu ni dhahiri kwa mtu yeyote ambaye amewahi kuwa karibu na watoto.

Kifungu cha uhakika juu ya ukweli kwamba watu hawajazaliwa wakiwa “wema” ni Zaburi 51:5. Hapa Daudi anazungumza kuhusu asili yake ya dhambi kuanzia wakati wa kutungwa mimba: “Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.”

mmHakuna kitu “kizuri” ndani ya mtu yeyote kati yetu. Hakuna kitu ndani yetu ambacho kinaweza kutuletea wokovu, na sisi wenyewe hatuna uwezo wa kustahili kupata kibali cha Mungu. Tunastahili ghadhabu ya Mungu pekee (Waefeso 2:3). Tumekufa katika dhambi zetu (Waefeso 2:1). Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye alichagua kumtuma Mwanawe, Yesu, ulimwenguni. Yesu aliishi bila dhambi, na kifo chake msalabani kililipa adhabu tuliyostahili.

Wimbo wa Charles Wesley “And can It be/Na Inaweza kuwa?” kwa kweli anamsifu Bwana kwa upendo wake wa ajabu:

“Aliacha kiti cha enzi cha Baba yake mbinguni,
Huru sana, neema yake isiyo na kikomo!
Alijiweka tupu kwa yote isipokuwa upendo,
Na kumwaga damu kwa ajili ya jamii ya wanyonge ya Adamu…
Upendo wa ajabu! Inawezaje kuwa
Kwamba Wewe, Mungu wangu, ufe kwa ajili yangu?”

Upendo mkuu wa Mungu kwetu ndio sababu kuu anatupa zawadi kama hiyo ya ajabu-zawadi ya msamaha wa dhambi! Yohona 3:16-18 inasema, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Watu wote wamezaliwa wakiwa wema?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries