settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kufanikiwa kumlea kijana?

Jibu


Wazazi wengi Wakristo wanashangaa kama watafanikiwa katika kumlea kijana. Vijana kawaida huwa na sifa fulani. Kwanza, wanapitia hatua ya maisha ambapo wanaamini wanajua mambo yote na ambayo hawayajui haina maana kujua. Pili, homoni na kemikali katika akili zao na miili yao zinawazuia mara nyingi kufikiria kama watu wazima wenye busara. Wanataka kile wanachotaka wakati wanataka, na mara nyingi hawana wazo lolote kwamba wanachoazima kitawaumiza. Ni kazi ya wazazi kuwalinda kutoka kwao wenyewe wakati wanapopitia wakati huu mgumu wa maisha.

Yesu anatufundisha hili katika Mathayo 7: 9-10 wakati anasema, "Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe?Au akiomba samaki, atampa nyoka? Hakika sivyo! " Wakati mwingine watoto huomba vitu vinavyoonekana kuwa vyema kwao, lakini vinaweza kuwaangamiza, hivyo basi ni wajibu wa wazazi kufanya kile kilicho bora zaidi. Tuna sheria sawa — ikiwa tunamwomba Mungu kitu ambacho tunadhani ni kizuri, lakini kile ambacho Mungu anajua sio kizuri, Yeye hatatupa.

Kuwa na Yesu katika nyumba yako ndiyo njia bora ya kuwalea watoto. "Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee." (Mithali 22: 6). Ikiwa umekuwa Mkristo kwa kumkaribisha Yesu ndani ya moyo wako, basi Roho Mtakatifu anaishi ndani yako na atawafundisha vitu vyote (Yohana 14:26, 1 Yohana 2:27), na hii inajumuisha jinsi tunavyolea watoto wetu. Watoto wanajifunza kutoka kwa yale wanayoona kutoka kwetu zaidi kuliko kile tunachowaambia, hivyo kuwa mfano mzuri ni muhimu sana.

Biblia inatufundisha umuhimu wa nidhamu. " Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema" (Mithali 13:24). " Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake." (Mithali 19:18). "Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako." (Methali 29:17). Ni muhimu kuweka sheria na kutekeleza. Watoto wanapojua kwamba wanachofanya ni uhalifu, adhabu ya aina fulani inapaswa kufuata, lakini inapaswa kuwa sahihi kwa "uhalifu" huo. Kwa mfano, kudanganya kunaonyesha kwamba mtoto hawezi kuaminika, hivyo labda mpaka imani hiyo inaweza kurejeshwa, wakati unaotumiwa nje ya nyumba lazima uwe mdogo sana. Watakuhitaji uwaamini tena, kwa hivyo watajifunza kutoka kwa hilo. Jambo baya zaidi tunaweza kufanya ni jaribu kuwa rafiki wa watoto wetu badala ya mzazi.

Kumrudi mtoto inapaswa kufanyika na maslahi bora ya mtoto kama msukumo. Waefeso 6: 4 inasema hatupaswi kuwakasirisha watoto wetu kwa njia tunavyowatendea (hii haimaanishi kutoweka nidhamu, inamaanisha msiwe na hasira katika kumrudi mtoto au kuchanganyikiwa), lakini uwalee kwa nidhamu na mafundisho yaliyopitishwa na Bwana. Hakikisha unamwambia mtoto wako kwa nini tabia hiyo ni sahihi, kwa nini hukubaliani na tathmini yao ya kitu fulani, na kwamba unafanya mambo unayofanya kutokana na upendo kwa ajili yake. Waebrania 12: 7 inatuambia kwamba Mungu anawaadhibu watoto wake wote tunapofanya makosa kwa sababu Yeye anatupenda na haitakuwa nzuri kwetu ikiwa hatofanya hivyo. Wakati watoto wanajibizana kuhusu kuadhibiwa, ambayo hakika watafanya, mzazi mwenye hekima anajibu, "Ni wajibu wangu kukuonya, na kama sitofanya hivyo, nitakuwa na maswali ya kumjibu Mungu."

Hatimaye, mambo kadhaa ni muhimu ili kufanikiwa katika kulea vijana: hisia ya ucheshi, hisia ya kuamini kwamba unafanya jambo lililo sawa, kutegemea hekima ya Mungu katika Neno Lake, na sala, sala, sala! Mambo haya hayatawasaidia wazazi "kufanikiwa" katika kulea tu lakini pia yatawasaidia kuwa na uzazi mzuri, ambao vijana watatumia wakati wa kuwa wazazi wenyewe.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kufanikiwa kumlea kijana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries