settings icon
share icon
Swali

Ni jinsi gani sala ni ya kuwasiliana na Mungu?

Jibu


Kwa kuelewa asili ya mawasiliano ya Mungu kwetu, na sisi kwake, tunahitaji kuanza na chache za maagizo muhimu. Kwanza ni Mungu hunena ukweli tu. Yeye kamwe hasemi uongo, na Yeye kamwe hadanganyi. Ayubu 34:12 inasema, "Naam hakika, Mungu haatenda mabaya, wala Mwenyezi hatapotosha hukumu." Amri ya pili ni kwamba Biblia ni neno sana Mungu. Neno la Kiyunani la "Maandiko," graphe, limetumika mara 51 katika Agano Jipya kuelezea maandishi ya Agano la Kale. Paulo anathibitisha katika 2 Timotheo 3:16 kwamba maneno haya halisi ni "pumzi na Mungu." Neno graphe pia linatumika katika Agano Jipya, hasa wakati Petro anaita nyaraka za Paulo "andiko" katika 2 Petro 3:16 , na pia wakati Paulo ( katika 1 Timotheo 5:18 ) ananukuu maneno ya Yesu vile yanapatikana katika Luka 10:7 na anayaita "maandiko." Hivyo, pindi tu tutakapothibitisha kwamba maandishi ya Agano Jipya hupatikana katika kikundi maalum cha "maandiko," basi sisi tu sahihi katika kutumia 2 Timotheo 3:16 kwa kuwa maandishi hayo pia, na kusema kwamba maandishi hayo pia yana sifa ambazo Paulo anaipa "Kila andiko lote." Ni "pumzi ya Mungu," na maneno yake yote ni neno ya Mungu.

Ni kwa nini habari hii ni ya muhimu kwa somo la maombi? Sasa kwa vile tumethibitisha kuwa Mungu anaongea ukweli na kwamba Biblia ni neno la Mungu, tunaweza fikia kimantiki hitimisho mbili zifuatazo kwa mawasiliano na Mungu. Kwanza, tangu Biblia inasema kwamba Mungu anasikia mwanadamu (Zaburi 17:6, 77:1, Isaya 38:5), mwanadamu anaweza kuamini kwamba wakati yeye ana uhusiano sahihi na Mungu na yeye anaongea na Mungu, Atapata kumsikiliza. Pili, tangu Biblia ni maneno la Mungu, mwanadamu anaweza kuamini kwamba wakati yeye yu katika uhusiano sahihi na Mungu na yeye anasomaji Biblia, yeye halisi husikia neno la Mungu linalosungumwa. Uhusiano mzuri na Mungu ambao ni muhimu kwa mawasiliano mazuri kati ya Mungu na mwanadamu ni vile inavyothibitishwa katika njia tatu. Kwanza ni kugeuka kutoka dhambi, au kutubu. Zaburi 27:9, kwa mfano, ni ombi la Daudi kwa Mungu ili kumsikiliza na si kugeuka mbali kutoka kwake kwa hasira. Kutokana na hili, tunajua kwamba Mungu anafanya kugeuza uso wake mbali na dhambi ya mwanadamu na kwamba dhambi inazuia mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu. Mfano mwingine wa hili unapatikana katika Isaya 59:2, ambapo Isaya anasema watu , "Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu; dhambi zenu zimeuficha uso wake, ili yeye hataki kusikia."Kwa hiyo, wakati kuna dhambi haijaungamwa katika maisha yetu, itazuia mawasiliano yetu na Mungu.

Muhimu pia kwa ajili ya mawasiliano na Mungu ni moyo wa unyenyekevu. Mungu anasema maneno haya katika Isaya 66:2 , " lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu." Jambo la tatu ni maisha ya haki. Huu ndio uzuri wa kugeuka kutoka dhambi na ni alama hasa kwa ufanisi katika maombi. Yakobo 5:16 inasema, "Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii."

Hotuba yetu kwa Mungu inaweza kuwa ya sauti, katika akili zetu, au andishi. Tunaweza kuwa na uhakika kwamba atatusikia na kwamba Roho Mtakatifu hutusaidia kuomba chenye tunapaswa kuomba. Warumi 8:26 inasema, "Kadhalika roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini roho mweneyew hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa."

Vile vile inavyohuzisha mawasiliano ya Mungu kwetu, ni lazima tutafute Mungu kuzungumza nasi hasa kwa njia ya maandiko, badala ya kuamini kwamba Mungu daima huweka mawazo moja kwa moja katika akili zetu ili kutuongoza sisi kwa vitendo au maamuzi maalum. Kwa sababu ya uwezo wetu wa ubinafsi udanganyifu, si busara kwa kukubali wazo lolote linaingia katika akili zetu kuwa linatoka kwa Mungu. Wakati mwingine, kuhusu masuala maalum katika maisha yetu, Mungu haneni nasi moja kwa moja kupitia maandiko, na inaweza kuwa jaribio kuangalia ufunuo zaidi ya Biblia katika matukio hayo. Hata hivyo, katika nyakati hizo, ni vyema - ili kuepuka kuweka maneno katika kinywa cha Mungu na / au kufungulia sisi wenyewe kwa udanganyifu -kupata majibu kwa kurejelea kanuni za kibiblia ambazo Yeye tayari ametupa.

Pia ni vyema kwa kuomba kwa bidii kwa ajili ya hekima kufikia hitimisho sahihi, kwa sababu ameahidi kutoa hekima kwa wale ambao huomba kwa ajili yake. "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei naye atapewa" (Yakobo 1:5). Ni jinsi gani sala ni kuwasiliana na Mungu? Maombi ni kuzungumza kwetu kutoka moyoni kwa Baba yetu wa mbinguni, na katika kurudi, Mungu akizungumza na sisi kwa neno lake na kutuongoza kwa uongozi wa Roho wake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni jinsi gani sala ni ya kuwasiliana na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries