settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anatarajia sisi sote kuwa na watoto?

Jibu


Sio suala hasa ikiwa Mungu "anatarajia" sisi kuwa na watoto, kwa kuwa Yeye ndiye mwenye nguvu na mwenye maarifa yote na anajua nani atakayekuwa na watoto na mwenye hatakuwa na watoto. Swali moja hasa ni ikiwa kuwa au kutokuwa na watoto ni mahitaji kwa Wakristo na ikiwa tunaweza kuwa tumetimiza maisha ya utii katika Kristo bila watoto.

Biblia inatuambia kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Zaburi 127:3-5 inasema, "Tazama, wana ndio urithi wa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani. Heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu wanaposema na adui langoni." Hii haimaanishi kwamba wale wasio na watoto hawajabarikiwa au kwamba watoto ndio baraka pekee ya Mungu. Ina maana tu kwamba watoto wanapaswa kuonekana kama baraka, si laana au usumbufu.

Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha"(Mwanzo 1:28). Baada ya gharika, Mungu alimwambia Nuhu, "Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi" (Mwanzo 9:1). Kuzaa ni sehemu ya amri ya Mungu kwa wanadamu, na kwa hakika Yeye "anatarajia" watu wengi kuwa na watoto. Pia tunaona kuwa na watoto kama sehemu ya agano la Mungu na Ibrahimu. Alimwambia Ibrahimu, "Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki. . . na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa"(Mwanzo 12:2-3). Hili hatimaye lilitimizwa kupitia Yesu Kristo, Mwokozi ambaye ni Mungu kamili na mwanadamu kamili-na ambaye alizaliwa kutoka kwenye mstari wa Ibrahimu.

Katika Agano la Kale, watoto walionekana kama ishara ya kimwili ya baraka za Mungu. Hata hivyo, na ingawa watu wengi wa wakati huo wangeweza kujihisi tofauti, ugumba/utasa haikuwa ishara ya kuaminika ya chuki ya Mungu. Wanandoa wengi katika Biblia, kama vile Elkana na Hana (wazazi wa nabii Samweli), Ibrahimu na Sara (wazazi wa Isaka), na Zakaria na Elizabeth (wazazi wa Yohana Mbatizaji), walikuwa wanaume na wanawake wa kiungu ambao kwa miaka walikuwa gumba/tasa.

Katika Agano Jipya, watoto bado wanaonekana kama baraka. Yesu aliwakaribisha watoto na kuwafundisha wanafunzi Wake kwamba watoto huonyesha mfano wa maadili mengi ya ufalme wa Mungu. Mtume Paulo alitoa maagizo kwa wazazi na watoto kuhusu kuishi vizuri pamoja (Waefeso 6:1-4). Mojawapo ya mahitaji ya msimamizi katika kanisa ni kwamba, ikiwa anaolewa na watoto, lazima awe mwenye usimamizi mzuri wa nyumba yake mwenyewe; ikiwa hawezi kutunza familia yake mwenyewe, hawezi kuwa na uwezo wa kutunza kanisa (1 Timotheo 3:4-5). Hakuna swali kwamba familia ina thamani ya juu sana kwa Mungu. Lakini Agano Jipya linalenga zaidi juu ya mafanikio na uzidishaji wa kiroho kuliko juu ya baraka za kimwili. Waumini katika Yesu wakawa watoto wa Mungu (Yohana 1:12). Ni familia Yake hasa ambayo tunataka kupanua. Tunaitaji kufanya wanafunzi (Mathayo 28:19), si tu watoto wa kibiolojia.

Watoto ni na daima watakuwa baraka kutoka kwa Mungu-bila kujali jinsi mtoto atakuwa sehemu ya maisha ya mtu. Lakini ingawa Mungu ametangaza watoto kuwa baraka kutoka Kwake na kuzaa ni sehemu ya mamlaka kwa binadamu kwa ujumla, hakuna mahali ambapo Biblia inasema kuwa kila wanandoa walioana lazima wawe au tamani kuwa na watoto. Tena, ugumba/utasa-katika umri wowote-sio ishara ya chuki ya Mungu. Wanandoa bila watoto kwa njia yoyote sio wa thamani au umuhimu ndogo kwa ufalme wa Mungu kuliko wale walio na watoto. Kwa kweli, mtu anaweza kufanya kesi kwamba wanandoa wasio na watoto wanaweza kujitolea kwa nguvu zaidi na kuzingatia kazi ya ufalme kuliko wale walio na watoto, kama vile watu wasio na waenzi (ona 1 Wakorintho 7:32). Aliyeolewa, asiye na mwenzi, aliye na watoto, au bila watoto, kila mtoto wa Mungu ni mwanachama muhimu wa familia Yake na ni sehemu muhimu ya mwili wa Kristo. Mapenzi maalum ya Mungu kwa kila mtu na kila ndoa ni tofauti. Kwa wengi, mapenzi ya Mungu ni pamoja na kuwa na watoto, ikiwa kwa kawaida au kwa kuasili. Kwa wengine, mapenzi yake hayahusishi kuwa na watoto.

Kwa wale ambao wanataka watoto bado hawawezi kuwa nao kwa sababu yoyote, kupeleka tamaa kwa Mungu katika sala ni bora. Anaweza kukusaidia kutembea kupitia uchungu wa safari na pia kukusaidia kuishi ubora Wake katika msimu huu. Kwa wale ambao hawataki kuwa na watoto, kupeleka tamaa kwa Mungu katika sala pia ni bora. Wakati mwingine ukosefu wetu wa tamaa ni ya kupewa na Mungu. Nyakati zingine, inaendeshwa na maumivu ya zamani, hofu, au ubinafsi. Tunapofungua mioyo yetu kwa uaminifu mbele ya Mungu, Yeye anaweza kutusaidia kutatua fujo, kuleta uponyaji, na kutupa tamaa za moyo Wake.

Ni rahisi sana kwa tamaa zetu kwa maisha yetu wenyewe kuwa sanamu. Hata tamaa njema, inapochukua nafasi ya Mungu katika maisha yetu, inakuwa sanamu. Sisi sote, bila kujali hali au hatua yetu ya maisha, fanya vizuri kuchunguza mioyo yetu, kuwa mwaminifu na Mungu katika sala, tafuta Neno lake kwa ajili ya hekima, na tutoe maisha yetu Kwake. Hatimaye, ni Mungu ambaye hutimiza mioyo yetu, na maisha yetu yanapaswa kuishi kwa utukufu Wake peke yake (Warumi 12:1-2; Zaburi 37).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anatarajia sisi sote kuwa na watoto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries