settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini inatupasa kuvaa vizuri tunapoenda kanisani?

Jibu


Ni muhimu kwetu kutafakari ni kwani tunavaa vile tunavaa. Mwanzo 35:1-3 inaweza kutupa mwanga katika jambo hilo: "Kisha Mungu akamwambia Yakobo, 'Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako." Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, "Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.'"

Kuna uwezekano kwamba Yakobo alianza safari hii ya Imani kwenda Betheli akiwa na Mungu, alitambu kiwango ambacho Mungu alikuwa amemtendea, na kiwango alichomhitaji Mungu! Itikio lake lilikuwa kumchukua kila mtu pamoja naye katika safari hii ya imani, ili waweze kujionea Mungu wao wenyewe. "Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni" inamaanisha haja kuwa na umoja katika "kuwa wasafi" mbele za Mungu. "Kwa maana wote wamefanya dhambi ..." (Warumi 3:23). Wengi wakati huo walikuwa na "sanamu zoa nyumbani" ambazo walizitegemea, vile vile na Mungu. Hawakutumaini Mungu peke yake. "Badilisha nguo zako" inamaanisha mbadiliko wa moyo dhidi ya dhambi. Ilikuwa iwe wakati kuhoji kile kilichokuwa kimefanyika kutoka "ndani."

Sisi zote tutanufaika kutoka kwa "uhuisho kiroho" ili tukiri na kuachana na dhambi zetu kabla twende kanisani. Kwa kufanya hivi tunajitakaza. Kwa watu wengine usafi ndio "chaguo" lao. Kwa wengine mioyo yao inawaambia kwamba kuvaa nguo zao bora ni kuonyesha jinsi Mungu anavyowadhamini. Na bado kwa wengine kunastahili kuwe na onyo kwao kwamba kilicho bora kwao hakipaswi kuwa cha kijigambia.

Kila wakati Mungu huangalia moyo kuliko mambo ya nje. Walakini, kile tunachovaa kwenda ibada kumwabudu Mungu wetu mtakatifu, na msafi inaweza kuonyesha hali penye miyo yetu ipo. Kama haujawai kufikiria hivyo mbeleni, jiulize, "Je! inajalisha vile ninavyoonekana ninapoenda kanisani kumwabudu Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana? Cha muhimu kujua, je! inajalisha kwake?" lazima sisi zote tuwe waamuzi wetu wenyewe. Ni chaguo la mtu, ukikumbuka kwamba kuwa na nia njema kwake Mungu Mwenyewe ni jambu la muhimu katika kujitayarisha kwa ibada ya kanisa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini inatupasa kuvaa vizuri tunapoenda kanisani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries