settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuvaa mavazi ya jinsia tofauti /kukingamana? Kukingamana ni dhambi?

Jibu


Kumbukumbu la Torati 22:5 inashughulikia suala la kuvaa nguo za jinsia nyingine/kukingamana (wanaume wanavaa nguo za wanawake na wanawake vile vile). Katika kifungu hiki Mungu anaamuru kwamba mwanamke asivae mavazi yanayompasa mwanamume na mwanamume asivae mavazi yanayompasa mwanamke, kwa maana wote wanaofanya hivyo ni “chukizo.” Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “chukizo” lamaanisha “kitu cha kuchukiza, chukizo, katika maana ya kidesturi (ya chakula najisi, sanamu, ndoa ya makabila), katika maana ya kiadili ya uovu.” Kwa hivyo, sio tu kwamba Mungu anazungumzia tu ukweli kwamba mwanamke anaweza kuvaa vazi la mwanamume au mwanamke kuvaa lile la kiume. Pia, hii sio amri kwamba mwanamke asivae suruali/kanzu kwani wengine hutumia kifungu hiki kufundisha hivyo. Maana hapa ni kwamba huku “kuvaa nguo za jinsia nyingine” na mkingamano unafanywa ili kudanganya au mtu kujionyesha kuwa mtu tofauti. Kwa maneno mengine, hii inamzungumzia mwanamke kubadilisha mavazi na sura yake ili aonekane mwanaume na mwanaume kubadilisha mavazi na sura yake ili aonekane ni mwanamke. Huu ndio ufafanuzi wa kuvaa mavazi ya jinsia nyingine au ukingamano.

Pia tunaweza kuhoji kwamba kinachochochea jambo hili ni kuacha kile ambacho ni cha asili na kuchukua kile kilichoitwa katika Neno la Mungu kuwa si asili (Warumi 1:24-27). Paulo analiambia kanisa la Korintho kwamba jinsi mwanamke anavyovaa nywele zake ni kielelezo cha utaratibu wa Mungu na kwa hivyo mwanamke anayekata nywele ili aonekane kama mwanamume au mwanamume mwenye nywele ndefu ndio aonekane kama mwanamke huwaletea aibu (1 Wakorintho 11:3-15). Suala hapa ni nia na mtazamo wa moyo unaothibitishwa katika chaguo la kuasi viwango vya Mungu vya utiivu.

Hizi ni kanuni tunazoweza kutumia kuhoji matumizi yake. Haijalishi desturi iliyo maarufu, wanaume na wanawake wanapaswa kuvaa mavazi yanayolingana na jinsia yao, kuvaa kwa heshima na kwa utaratibu (1 Wakorintho 14:40). Ili kutumia kanuni hii, Biblia inatia kuvaa nguo za jinsia nyingine au kukingamana kuwa chaguo ambalo ni dhihirisho la kutoamini na uasi dhidi ya Mungu na utaratibu Wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuvaa mavazi ya jinsia tofauti /kukingamana? Kukingamana ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries