settings icon
share icon
Swali

Inawezekana umuuzie shetani nafsi yako?

Jibu


Katika hadithi ya fikra ya Dr. Faustus, mtu hufanya mkataba na shetani: kwa mwili wake na nafsi yake, huyo mtu ili apokee nguvu isiyo ya kawaida na raha kwa miaka 24. Ibilisi anakubaliana na biashara hiyo, na Dr. Faustus anafurahia raha za dhambi kwa msimu tu, lakini adhabu yake imefungwa. Mwishoni mwa miaka 24, Faustus anajaribu kuzuia mipango ya shetani, lakini ankutana na hofu ya kutisha, hata hivyo. Hadithi hii inafanya vizuri kama itakua ni hadithi ya maadili na kama mfano wa mshahara wa dhambi, lakini maelezo ya njama yake sio ya kibiblia.

Biblia haina mfano wa mtu "anauza nafsi yake" kwa Shetani, na haisemi kwamba kuna uwezakano kubishana na shetani. Hii ndio baadhi ya yale Maandiko yanatufunulia kuhusu Shetani:

1) Shetani ana uwezo wa kupinga hata malaika (Yuda 9; Danieli 10: 12-13).

2) Shetani anajaribu kudanganya kwa kujibadilisha kuwa kama malaika wa nuru (2 Wakorintho 11: 14-15).

3) Mungu ametoa njia za kujitetea dhidi ya mashambulizi ya Shetani (Waefeso 6: 11-12).

4) Nguvu za Shetani zimezuiliwa kwa mapenzi ya Mungu (Ayubu 1: 10-12; 1 Wakorintho 10:13).

5) Kama "mungu wa ulimwengu huu," Shetani ana mamlaka juu ya wale wanaoishi bila Kristo duniani (2 Wakorintho 4: 4).

Hakika, kuna wale wanaoteseka chini ya udhibiti wa shetani, kama vile vijana wa Filipi (Matendo 16: 16-19). Na kuna wale ambao wamejitolea kwa kazi ya shetani, kama vile Simoni mchawi (Matendo 8: 9-11) na Elymas (Matendo 13: 8). Hata hivyo, katika kila moja ya mifano hii mitatu, nguvu ya Mungu inashinda utumwa wa Shetani. Kwa kweli, Simoni anapewa fursa ya kutubu katika (Matendo 8:22). Kwa hakika, hakukuwa na "kuuza" nafsi ya Simoni.

Bila Kristo, sisi sote tuko chini ya hukumu ya kifo (Warumi 3:23). Kabla ya kuokolewa, sisi sote tuko katika utumwa wa shetani, kama 1 Yohana 5:19 inasema, "Na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu." Bwana na asifiwe kwa kuwa, tunaye mtwalisi mpya, Mmoja ambaye anaweza kuvunja minyororo ya dhambi yoyote na kutuweka huru (1 Wakorintho 6: 9-11; Marko 5: 1-15).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inawezekana umuuzie shetani nafsi yako?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries