settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya Kristo kutwaa mwili?

Jibu


Utwalizi wa mwili ni neno linalotumiwa na wanatheolojia kuonyesha kuwa Yesu, Mwana wa Mungu, aliuchukua mwili wa mwanadamu. Hii ni sawa na muungano wa uungu na uanadamu katika mwili mmoja. Tofauti ni kwamba uungano huu unaelezea namna hasili mbili za Yesu zimeunganishwa, na Utwalizi wa mwili unadhibitisha uanadamu wake.

Neno utwalizi linamaanisha "tendo la kufanyika mwili." Linatoka kwa tafsiri ya Kilatini ya Yohana 1:14, ambayo katika Kingereza yasema hivi, "Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu." Kwa sababu ya ukaribu wa kutumi Biblia ya Kilatini peke yake kanisani katika Umri wa Katikati, neno la Kilatini likawa ndilo la kiwango.

Uungwaji wa uanadamu wa Yesu ni mwingi. Injili inaripoti mahitaji ya Yesu ya kiuanadamu ikiwa in pamoja na usinginzi (Luka 8:23), chakula (Mathayo 4:2; 21:18), na ulinzi wa kimwili (Mathayo 2:13-15; Yohana 10:39). Dalili zingine za uanadamu wake ni alitokwa na jasho (Luka 22:43-44) alotokwa na damu (Yohana 19:34). Yesu pia alionyesha hisia hii ikiwa ni pamoja na furaha (Yohana 15:11), huzuni (Mathayo 26:37), na hamaki (Marko 3:5). Wakati wa maisha yake, Yesu alijirejelea kama mwanadamu (Yohana 8:40), na baada ya ufufuo wa mwili wake binadamu bado alitambulika (Matendo 2:22).

Lakini lengo la Utwalizi halikuwa la kuonja chakula au kuhisi huzuni. Mwana wa Mungu alikuja katika mwili ili awe mwokozi wa mwanadamu. Kwanza, kulikuwa na haja ya kuzaliwa "chini ya sheria" (Wagalatia 4:4). Sisi wote tomekosa kutimiza Sheria ya Mungu. Kristo alikuja katika mwili, chini ya sheria, ili atimize sheria kwa niapa yetu (Mathayo 5:17; Wagalatia 4:5).

Pili, kulikuwa na haja ya Mwokozi kumwaga damu yake kwa ondoleo la dhambi (Waebrania 9:22). Dhabihu ya damu, huitaji mwili wa nyama na damu: 'Hukutaka tambiko wala sadaka, lakini umenitayarishia mwili'" (Waebrania 10:5). Bila Utwalizi, Kristo hangekufa, na msalaba hautakuwa na maana.

Mungu alifanya kazi ya ajabu kwa kumtuma Mwana Wake wa pekee ulimwenguni na kutupatia wokovu ambao hatukustahili. Bwana na asifiwe kwa wakati huo ambao "Neno lilikuwa mwili." Sasa tumekombolewa "bali kwa damu ya thamani ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa" (1Petro 1:19).

Yesu alikuwa mwanadamu na Mungu mtawalia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya Kristo kutwaa mwili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries