settings icon
share icon
Swali

Ikiwa wachumba wanapata mimba kabla ya ndoa, nilazima waolewe?

Jibu


Ngono kabla ya ndoa imekuwa kawaida sana katika jamii yetu, hata kufikia hatua ya kutarajiwa, kwamba wengi wanaodai kuwa Wakristo hawafikiri kuwa ni dhambi. Utamaduni wetu unashiria kwamba watu hawana kiasi cha kujidhibiti muhimu kwa kuepuka ngono mpaka ndoa, hivyo wazo hali imefanywa kuwa haiwezekani. Neno la Mungu halibadiliki, hata hivyo, na Biblia inatuambia kuwa ngono nje ya ndoa ni mbaya (Mathayo 15:19, 1 Wakorintho 6: 9, 6:13, 7: 2; 2 Wakorintho 12:21; Wagalatia 5:19 ; Waefeso 5: 3).

Mtu yeyote ambaye amekuwa Mkristo aliyezaliwa mara ya pili kwa kuweka imani yake kwa Kristo tena huwa sio mmiliki wa nasi yake mwenyewe. Wakorintho wa kwanza 6: 18-20 inasema, " Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au humjui kwamba mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu, aliye ndani yanu, mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi sio mali yenu wenyewe, maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu na miili yenu. "

Kupuuza mpango wa Mungu wa ndoa, ngono, na familia daima husababisha matokeo haya ya kiroho au ya kimwili: kuhuzunisha Roho Mtakatifu (Waefeso 4:30), hatia, aibu, majuto, kupoteza heshima yako na wengine, mgawanyiko katika familia na kati ya waumini, mfano usio mzuri,maumivu kwa wachumba watarajiwa, mimba zisizohitajika, utoaji mimba, magonjwa ya zinaa. Mungu anatarajia ngono kuwa kielelezo cha karibu cha upendo na kujitolea, kushiriki tu kati ya mume na mke. Ngono tu kwa ajili ya radhi ya kimwili yake hutuharibu kiroho na inatuvuta mbali na ushirika na Mungu.

Mtu yeyote ambaye amefanya kosa la kufanya ngono nje ya ndoa anaweza kusamehewa, hata ikiwa kosa limesababisha mimba isiyopangwa. Yohana wa Kwanza 1: 9 inasema, "Lakini tukikiri dhambi zetu kwake, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." Hii inamaanisha kugeuka mbali na dhambi zetu na kujitolea kumpenda na kumtumikia Kristo.

Kuna baadhi ya matukio ambapo kuoa kabla ya mtoto kuzaliwa itakuwa busara. Ikiwa wanandoa waliojitolea ambao tayari walikuwa tayari kupanga ndoa hufanya uzinzi na kusababisha ujauzito, ingewezekana iwe rahisi kwa familia kuolewa kabla ya motto kuzaliwa. Lakini ikiwa wanandoa wasiojitolea wanafanya dhambi sawa na hii, kuoana hakutawafanya sawa machoni pa Mungu. Katika hali hiyo, kufunga harusi kutafanya kuvunjika kwa ndoa hiyo. Biblia haiwaamrishi watu watu kuhusu kuoana au kutooana katika hali kama hii, ingawa wazazi wote bado wana wajibu wa kumsaidia mtoto kihisia, kiroho na kifedha.

Hakuna hata mmoja wetu anayefanyika haki mbele ya Mungu kupitia matendo. Tunaokolewa kwa imani peke yake, tukiamini Yesu Kristo kutuokoa kutoka kwa dhambi zetu. Biblia inasema, "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Waroma 6:23). Mungu hataki tujaribu kuwa haki wenyewe; Anataka sisi tumpe mioyo yetu. Kwa kuweka chini mapenzi yetu na kujisalimisha kwa ukuu wa Mungu, tunaweza kuwa na uhakika wa maisha yenye kutimiza duniani na pahali mbinguni pa milele.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa wachumba wanapata mimba kabla ya ndoa, nilazima waolewe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries