settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kujifunza kutumaini katika Mungu?

Jibu


Hatuwezi kumtumaini mtu tusiyemjua, na hiyo ndiyo siri ya kujifunza kumtumaini Mungu. Wakati mtu anasema, "Niaminieni," tuna athari moja kati ya mbili. Tunaweza kusema, "Naam, nitakuamini," au tunaweza kusema, "Kwa nini napaswa?" Katika kesi ya Mungu, kumtumaini Yeye kwa kawaida hufuata wakati tunaelewa kwa nini tunapaswa.

Sababu kuu tunapaswa kumtegemea Mungu ni kwamba Yeye anastahili tumaini letu. Tofauti na binadamu, Yeye hawezi kudanganya na kamwe hawezi kukosa kutimiza ahadi zake. "Mungu si mtu, aseme uongo; wala si mwanadamu, ajute; iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?"(Hesabu 23:19; Zaburi 89:34). Tofauti na watu, ana uwezo wa kupitisha kile anachopanga na makusudio ya kufanya. Isaya 14:24 inatuambia, "Bwana wa majeshi ameapa, akisema, hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea." Aidha, mipango Yake ni kamili, takatifu, na yenye haki, na anafanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya wema kwa wale wanaompenda na wameitwa kulingana na kusudi lake takatifu (Warumi 8:28). Ikiwa tutajitahidi kumjua Mungu kwa njia ya Neno Lake, tutaona kwamba Yeye anastahili tumaini, na tumaini letu ndani yake litakua kila siku. Kumjua ni kumtumaini.

Tunaweza kujifunza kumtegemea Mungu tunapoona jinsi alivyothibitisha mwenyewe kuwa mwaminifu katika maisha yetu na maisha ya wengine. Katika 1 Wafalme 8:56 tunasoma, "Na ahimidiwe Bwana, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake." Rekodi ya ahadi za Mungu zimo katika Neno Lake kwa wote kuona, kama vile rekodi ya utimilifu wao. Nyaraka za kihistoria zinathibitisha matukio hayo na kusema juu ya uaminifu wa Mungu kwa watu Wake. Kila Mkristo anaweza kutoa ushuhuda binafsi juu ya uaminifu wa Mungu tunapoona kazi Yake katika maisha yetu, kutimiza ahadi zake kwa kuokoa nafsi zetu na kututumia kwa madhumuni Yake (Waefeso 2: 8-10) na kutufariji kwa amani ambayo hupitia ufahamu wote vile tunakimbia mbio Yeye amepanga kwa ajili yetu (Wafilipi 4: 6-7; Waebrania 12: 1). Tunapoona zaidi neema yake, uaminifu, na wema, tunamtumaini zaidi (Zaburi 100: 5; Isaya 25: 1).

Sababu ya tatu ya kumwamini Mungu ni kwamba hatuwezi kuwa na mbadala ya busara. Je, tunapaswa kujiamini sisi wenyewe au kwa wengine ambao ni wenye dhambi, wasiotabirika, wasiotegemeka, wenye hekima ndogo, na wenye mara nyingi hufanya uchaguzi na maamuzi mabaya yanayoshawishiwa na hisia? Au tunaamini kwa mwenye busara yote, wenye kujua yote, wenye nguvu zote, wenye fadhili, wenye rehema, Mungu mwenye upendo ambaye ana nia nzuri kwetu? Uchaguzi unapaswa kuwa kawaida, lakini tunashindwa kumwamini Mungu kwa sababu hamtujui Yeye. Kama ilivyoelezwa hapo awali, hatuwezi kutumaini mtu ambaye ni mgeni kwetu, lakini hiyo ni rahisi kurekebishwa. Mungu hakujifanya kuwa vigumu kupatikana au kujua. Yote tunayohitaji kujua kuhusu Mungu, ametupatia kwa rehema katika Biblia, Neno Lake takatifu kwa watu Wake. Kumjua Mungu ni kumtumaini.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kujifunza kutumaini katika Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries