settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kutosamehe?

Jibu


Biblia ina mengi ya kusema kuhusu kusamehe kutosamehe. Labda mafundisho maarufu zaidi juu ya kutosamehe ni mfano wa Yesu wa mtumishi asiye na huruma, iliyoandikwa katika Mathayo 18: 21-35. Katika mfano huo, mfalme anasamehe deni kubwa sana (kimsingi moja ambayo hawezi kulipwa) ya mmoja wa watumishi wake. Baadaye, hata hivyo, mtumishi huyo anakataa kusamehe madeni madogo ya mtu mwingine. Mfalme alisikia juu ya jambo hili na kufuta msamaha wake wa awali. Yesu anahitimisha kwa kusema, "Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake." (Mathayo 18:35). Vifungu vingine vinatuambia kwamba tutasamehewa tunaposamehe (tazama Mathayo 6:14; 7: 2; na Luka 6:37, kwa mfano).

Usichanganyike hapa; Msamaha wa Mungu hautegemei kazi zetu. Msingi wa msamaha na wokovu ni katika utu wa Mungu na kwa kazi ya Yesu ya ukombozi msalabani. Hata hivyo, matendo yetu yanaonyesha imani yetu na kiwango ambacho tunaelewa neema ya Mungu (angalia Yakobo 2: 14-26 na Luka 7:47). Hatustahili kabisa, lakini Yesu alichagua kulipa dhamana ya dhambi zetu na kutupa msamaha (Warumi 5: 8). Tunapofahamu kweli wa ukuu wa karama ya Mungu kwetu, tutashiriki karama hio. Tumepewa neema na tunapaswa kutoa neema kwa wengine. Katika mfano huo, tunastaajabishwa na mtumishi ambaye hakusamehe deni la madogo baada ya kusamehewa deni lake lisilolipika. Hata hivyo, wakati tunakosa kusamehe, tunatenda kama mtumishi katika mfano huo.

Kutosamehe pia hutunyang'anya maisha kamili ambayo Mungu anatutarajia. Badala ya kuhamasisha haki, kutosamehe kwetu husababisha uchungu. Waebrania 12: 14-15 inonya hivi, " Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. "Vivyo hivyo, 2 Wakorintho 2: 5-11 inonya kwamba kutosamehe inaweza kuwa njia ya Shetani ya kutupotosha.

Tunajua pia kwamba wale ambao wametenda dhambi dhidi yetu — ambao hatungependa kusamehe — wanajibika kwa Mungu (tazama Warumi 12:19 na Waebrania 10:30). Ni muhimu kutambua kuwa kusamehe sio kupuuza makosa au kupatanishwa. Tunapochagua kusamehe, tunaweka huru mtu kutoka kwa deni lake kwetu. Tunawacha haki ya kulipiza kisasi. Tunaamua kusema hatutashikilia makosa yake dhidi yake. Hata hivyo, hatuwezi kumruhusu mtu huyo kurejea kwa Imani yetu au kumweka huru kabisa mtu huyo kutokana na matokeo ya dhambi yake. Tunaambiwa kwamba "mshahara wa dhambi ni kifo" (Warumi 6:23). Ingawa msamaha wa Mungu hutuondoa kutoka kifo cha milele, haitukomboi daima kutokana na matokeo ya dhambi (kama vile uhusiano uliovunjwa au adhabu inayotolewa na mfumo wa haki). Msamaha haimaanishi sisi kutenda kama hakuna makosa yamefanyika; inamaanisha sisi tunatambua kwamba neema nyingi ambayo tumemepewa na kwamba hatuna haki ya kushikilia makosa dhidi ya mtu mwingine.

Mara kwa mara, Maandiko yanatusihi tusameheane. Waefeso 4:32, kwa mfano, anasema, tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.'' Tumepewa mengi katika njia ya msamaha, na mengi yanatarajiwa kutoka kwetu jibu (tazama Luka 12:48). Ingawa mara nyingi ni vigumu kusamehe, kutosamehe ni kutomtii Mungu na kupunguza ukuu wa karama Yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kutosamehe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries