settings icon
share icon
Swali

Je! Utengano na nini? Je! Inamaanisha nini kuwa tumetengwa na Mungu?

Jibu


Utengano ni hali ya kuondoka au kujitenga toka kwa kikundi, mtu, au hali ambayo mbeleni mtu alikuwa amehusika nayo. Utengano ni neno linguine la farakana. Waefeso 4:18 inawaeleze wasio Wakristo kuwa "Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao." Kutengwa kutoka kwa Mungu inamaanisha sisi wenye tumejifanya wageni kwake kwa sababu ya dhambi zetu.

Mungu aliwaumba wanadamu kuishi katika uhusiano wa karibu Naye (Mwanzo 1:27). Tulipangiwa kuwa kama Mungu kuliko kiumbe chochote, ile hali tuna hiari huru ya kuchagua ikiwa tunataka kumpokea Bwana kama Mungu wetu au ikiwa tutakuwa miungu wetu wenyewe. Uamuzi huo unaamua uhusiano wetu Naye, ikiwa tunaishi kama wageni au kama Wanawe wapendwa (Yohana 1:12). Tunazaliwa na hali ya dhambi, na hali hiyo inatufanya maadui na utakatifu wa Mungu (Warumi 5:12). Hali yetu ya dhambi inaifanya vigumu kuwa na ushirika na Mungu au kumpendeza Yeye kwa namna yoyote (Warumi 8:8). Tunaishi katika hali ya untengano kutoka Kwake, haijalishi jinsi tunavyojaribu kuwa wema kwa sababu kiwango chake ni kikamilifu na hakuna yeyote miongoni mwetu anaweza kufikia kiwango hicho (Warumi 3:10, 23; 6:23).

Yesu Kristo alikuja ulimwenguni kugeuza utengano huo na Mungu. Alikuja ili awe amani yetu (Waefeso 2:14), kutupatanisha na Mungu (Warumi 5:10; 2Wakorintho 5:18). Utengano wetu na Mungu ulihuzisha deni tusingeweza kulipa. Malipo pekee ya haki kwa makosa ya jinai dhidi ya Muumba wetu ni milele kutumikia ziwa la moto (Yohana 3:16-18, 36; Warumi 6:23; Mathayo 25:46). Jahannam ni mahali pa mwisho pa utengano bila tumaini wa kuwai patana na Mungu au wale tuanao wapenda. Katika hukumu ya mwisho, uamuzi wa Yesu dhidi ya wale ambao wametengwa na Yeye utaimarisha utengano huo milele yote: "Ndipo nitakapowaambia wazi, 'Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!'" (Mathayo 7:23).

Ili atuokoe kutoka na utengano na Mungu wa kudumu, Baba alimtuma Mwanawe alipe deni ambayo hatungeweza kuilipa sisi wenyewe na kuichukua adabu tuliyohistahili (2 Wakorintho 5:21). Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu, Mungu anaweza kutangaza deni ya dhambi zetu "Inalipwa Kikamilifu" wakati tunapokuka kwa Kristo katika toba na imani (Wakolosai 2:14). "Mungu… ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo!'" (2 Wakorintho 5:18).

Waefeso 2:18-19 inasema, "Kwa maana kwa kupitia kwake, sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu." Wazazi mara nyingi hawanunulii kila mtoto katika maeneo wanamoishi viatu na bidhaa za shule. Wanaweza kufanya hivyo kwa sababu ya ukarimu na wana mapato ya kutosha, lakini hawawajibiki kwa watotot ambao sio wao. Vivyo ilivyo na Mungu. Wakati tunaishi katika hali ya kutengwa Naye, Munug hawajibiki kuyasikia maombi yetu, kutufariji, au kutukinga na mabaya yoyote (Mithali 10:3; 28:9; Zaburi 66:18). Lakini wakati anatutwaa kupitia kwa Imani katika kifo cha Yesu na ufufuo wake, tunakuwa watoto Wake wapendwa (Yohana 1:12; Warumi 8:15). Yesu alituwezesha sisi wote ambao tulikuwa tumetengwa na Mungu, sasa tunaweza patanishwa kama watoto Wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Utengano na nini? Je! Inamaanisha nini kuwa tumetengwa na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries