settings icon
share icon
Swali

Je! Ni suluhisho gani la kibiblia la kutatua matatizo ya ndoa?

Jibu


Ndoa ni uhusiano wa karibu zaidi wanadamu wanaoweza kupata, baada ya uhusiano tu na Mungu. Ndoa huweka hadharani wema na ubaya wa watu wengi, watu wawili tofauti wanapojitahidi kuishi kama "mwili mmoja" (Mathayo 19: 6; Marko 10: 8). Chanzo cha matatizo mengi ya ndoa ni ubinafsi. Wakati mume au mke au wote wawili wanapochagua kuishi kama kwamba mahitaji yake yanastahili kuzingatiwa zaidi, migogoro hutokea.

Kuna mistari maalum inayozungumzia tabia ya waume na wake. Baadhi ya hayo ni 1 Petro 3: 1-8, Wakolosai 3: 18-19, na Tito 2: 3-5. Wafilipi 2: 3-13 ni kichocheo bora cha kutatua matatizo ya ndoa Ingawa haizungumzii ndoa moja kwa moja. Kifungu hiki kinatuambia tutekeleza nia ambayo Kristo alionyesha wakati aliweka kando haki na faida kama Mwana wa Mungu na kuja duniani kama mtumishi mnyenyekevu. Mstari wa 3 na 4 husema, "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine." Wakati ushauri huo unatumika kwenye ndoa, kila kikwazo chochote kinaweza kushindwa.

Hakika, kutafuta ushauri kutoka kwa mchungaji au mshauri mkristo wa ndoa ni jambo la kibiblia la kufanya (Methali 19:20). Kupata ushauri ni njia bora ya kufuta mawazo yasiyofaa juu ya majukumu ya ndoa, kuona hali kutoka kwa mtazamo mwingine, na kutofautisha kati ya viwango vya Mungu na yale ya ulimwengu.

Waefeso 5: 21-33 hutoa maagizo maalum kwa waume na wake. Mume ni kumpenda mke wake "kama Kristo anavyopenda kanisa na kujitoa kwa ajili yake" (mstari wa 25). Upendo huo wa kujitolea hujenga mazingira ambapo mke anaweza kunyenyekea kwa urahisi kwa uongozi wa mumewe. Mume akijitolea kuonyesha upendo kwa mkewe, na mke amejitolea kwa upole kuruhusu mumewe kuongoza, ndoa itafanya kazi.

Pia ni busara kuzingatia mistari inayotangulia kabla ya maagizo ya ndoa maalum. Waefeso 5: 18-21 inasema, "Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

Angalia amri zote zinazotangulia maelekezo ya ndoa. Wakristo wote wanapaswa
• kukataa kulewa
• kujazwa na Roho
• kuhimizana
• kuimba nyimbo za sifa
• kuwa na mtazamo wa ibada ya daima
• kuwa na roho ya shukrani
• kujiwasilisha kwa neema kwa kila mmoja

Tunakosa ukweli muhimu wakati tunapokwenda moja kwa moja kwenye mafundisho ya ndoa bila kutumia miongozo kwa vitendo katika aya zilizotangulia. Wakati kila mwanandoa anapotumia ukweli huo kwa maisha yake na anajitahidi kufanya uhusiano wake na Bwana lengo kuu, matatizo ya ndoa huisha. Wakati Wakristo wawili wanakusudia kutafuta moyo wa Mungu na kufuata mapenzi Yake bila kujali, hakuna tatizo ambalo hawawezi kutatua.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni suluhisho gani la kibiblia la kutatua matatizo ya ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries