settings icon
share icon
Swali

Je! Ninawezaje kutafakari Neno la Mungu?

Jibu


Mazoezi ya kiroho ya kutafakari sio jambo geni kwa Ukristo. Dini nyingi zisizo za Kikristo na vikundi vya kilimwengu hufanya mazoezi ya kutafakari. Walakini, wakati Biblia inazungumza juu ya kutafakari, kama vile inavyofanya mara nyingi, sio aina ya kutafakari ambayo hutafuta kujitenga, kimya, au kufunua akili, kama vile ilivyo katika aina ya dini za kutafakari mafumbo ya akili au tafalaro ua Wabudha. Maandiko yanafundisha tafakari ambayo hushughulisha sana akili kwa kusudi la kuelewa Neno la Mungu na kuliweka katika matumizi. Je! Tunawezaje kutafakari Neno la Mungu ili lizae ndani yetu maisha yenye matunda na matakatifu mbele za Mungu?

Katika ulimwengu wa kale wa Kiebrania, kutafakari wakati mwingi kulihusisha kutumia na kushirikisha akili. Thomas Watson, mchungaji wa Wa-puritani wa karne ya kumi na saba, alitumia muda mwingi katika maisha yake kuitafakari Biblia, huku akiiweka katika mazoezi na kufundisha juu yake. Alifafanua vyema sana nidhamu hiyo katika kitabu chake Heaven Taken by Storm kama "mazoezi matakatifu ya akili, ambayo kwayo tunaleta ukweli wa Mungu katika kumbukumbu, na kuyatafakari kwa uzito, na kuyatumia sisi wenyewe."

Kwa mjibu wa ufafanuzi wa Watson, tunaweza kutafakari juu ya Neno la Mungu kwa kukumbuka ukweli Wake. Kukumbuka kunahitaji kukumbuka kwa bidii na kwa ufahamu wa kile tunachokijua juu ya Mungu kutoka kwa Neno Lake: "Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku" (Zaburi 63: 6). Kulingana na Zaburi 1: 2, mtu aliyebarikiwa, anayezaa matunda, na mwenye haki hufurahia Neno la Bwana "naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana." Tafakari hii ni ya endelefu ("mchana na usiku") na inazingatia Neno la Mungu ("sheria yake"). Tunalitafakari Neno la Mungu kwa kujaza akili zetu na Neno hilo mchana na usiku.

Mungu alimwita Yoshua kutafakari kwa uhodari na kwa kuendelea: "Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi" (Yoshua 1: 8). Hapa, kutafakari kwa kibiblia kunapanuka kutoka kufikiria tu hadi usemi ("kwenye midomo yako"). Kifungu hiki pia kinasema kusudi la tafakari, ambayo ni, kutii Neno la Mungu, ambalo huzaa mafanikio na ufanisi mbele za Mungu.

Maelezo ya Watson ya kutafakari hujumuisha na kutafakari kwa uzito au kutafakari ukweli wa Mungu. Zaburi 119: 15 inasema, "Nitajifunza maagizo yako na kuziangalia njia zako." Kwa hivyo tafakari ya kibiblia inajumuisha kutafakari kwa kina na kujifunza Neno la Mungu. Tunapoisoma Biblia, je, tunaisoma pole pole na kwa makusudi? Je! Tunafikiria juu ya umuhimu wa maneno na jinsi yanahusiana na maisha yetu na maisha ya wengine? Ikiwa ndivyo, basi tunatafakari juu ya Neno la Mungu.

Kutafakari kunahitaji wakati na bidii. Hakuwezi kuharakiswa. Kunajumuisha kujiondoa kwenye usumbufu wa maisha haya ili tuweze kuweka mawazo yetu kwa Mungu na Neno Lake. Kwa kufunga kelele za ulimwengu huu, tunaweza kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na kuelewa njia zake: "Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako" (Zaburi 119: 99).

Hatimaye, kama vile Watson alivyogusia, tafakari ya kibiblia inatafuta kutumia Neno la Mungu kwa maisha yetu. Zaburi 19:14 inaonyesha ukweli huu: "Maneno ya kinywa change na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu." Kutafakari juu ya Neno la Mungu kunapendeza machoni pa Mungu kwa sababu husababisha mabadiliko ya maisha yetu. Tunaposoma na kunena ukweli wa Mungu na kuutafakari kwa bidii, Roho Mtakatifu hutuwezesha kuutumia ukweli huo katika vitendo. Katika Wafilipi 4: 8–9, mtume Paulo anatupa taswira hii nzuri na kamili ya tafakari ya kibiblia: "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Mambo yote mliyojifunza au kuyapokea au kuyasikia kutoka kwangu, au kuyaona kwangu, yatendeni hayo. Naye Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi."

Kutafakari ni njia ya kuzingatia Neno la Mungu kwa ndani —kuliweka ndani ya mioyo yetu — ili Roho Mtakatifu aweze kufanya kazi kupitia kwalo ili atuongoze, atufundishe, atutakase na kutubadilisha kutoka ndani. Tunaweza kuisikiliza Biblia ikisomwa, tuisome, na kukariri Maandiko ili tuingize akilini mwetu, lakini pia lazima tuitafakari kila wakati mioyoni mwetu ili tuweze kuielewa zaidi na jinsi inavyotumika katika maisha yetu.

Hapa kuna vidokezo vinne vya kutafakari juu ya Neno la Mungu:

1. Chagua wakati na mahali maalum kila siku wakati hautaweza kusumbuliwa au kuachishwa ili uwe upate kuwa peke yako na kutafakari Neno la Mungu.

2. Anza na maombi na mwombe Mungu akusaidie katika kutafakari kwako. Unaweza kumwuliza Bwana akulete karibu naye, afungue macho yako kwa ukweli Wake, akusaidie kuuweka ukweli huo maishani mwako, na akubadilishe unapotafakari juu ya Neno la Mungu.

3. Chagua sehemu ndogo ya Maandiko. Fikiria juu ya kile kifungu hicho kinamaanisha. Jifunze kwa kina ili uweze kukielewa katika muktadha. Andika hati. Uliza maswali. Kariri kifungu hicho. Muulize Mungu anataka kusema nini nawe kupitia maandishi hayo.

4. Fikiria jinsi unaweza kutumia kifungu hicho katika maisha yako kwa njia za vitendo, na umwombe Mungu akusaidie kuifuata kwa kutii kile Anachokuonyesha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ninawezaje kutafakari Neno la Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries