settings icon
share icon
Swali

Je! Kusudi la malaika ni gani?

Jibu


Makerubi walio uchi, na mabawa, wa nuru na wato warembo sana katika michezo ya Krismasi ni baadhi ya picha ambazo huja akilini tunapofikiria juu ya malaika. Lakini neno la Mungu linatupa picha tofauti kabisa. Waebrania 1:7 inasema, “Huwafanya malaika wake kuwa pepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.” Malaika ni roho walioumbwa ili kutumikia madhumini ya Mungu.

Maandiko yanatupa picha duku ya ulimwengu usio wa kawaida, lakini inatosha kujifunza kwamba malaika hufanya kazi mbali mbali na hutumiwa kwa madhumuni kadhaa:

1. Kuhudumia watu ambao Mungu huokoa. Kusudi moja la malaika ni kuwahudumia wateule wa Mungu: ”Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?” (Waebrania 1:14). Paulo alionekeaniwa na malaika wakati wa dhoruba baharini. Malaika alimletea faraja (Matendo 27:23-24). Watu wengine ambao wamehudumiwa na malaika ni pamoja na Eliya (1 Wafalme 19:3-8) na Petro (Matendo 12:6-10).

2. Kuwasilisha ujumbe. Neno malaika linaanisha “mjumbe.” Katika Biblia, malaika kwa kawaida walionekana kama mwanadamu wakati walipowasilisha ujumbe kutoka kwa Mungu kwa watu (angalia Mwanzo 18:1-13). Malaika Gabrieli aliwaonekania angalau watu watatu katika Biblia. Alifafanua ndoto ya Danieli (Danieli 8:1-3), alimwambia Zekaria kuhusu kuzaliwa kwa Yohana mbatizaji (Luka 1:19), na akamtangazaia Maria kuwa atakuwa mama wa Masiha (Luka 1:26). Malaika katika mfano wa mwanadamu pia walimwonya Loti kuhusu hukumu ya Mungu kwa Sodoma na Gomora (Mwanzo 19:1).

3. Kupigana na vita vya kiroho. Kusudi lingine la malaika ni kupigana na nguvu za giza kiroho ambao hujaribu kuzuia mipango ya Mungu (Waefeso 6:12; Yuda 1:9). Wakati malaika alimwonekania Danieli ili wasilishe ufafanusi wa ndoto, malaika alisema kwamba Mikaeli malaika mkuu atamsaidia kupigana na majeshi ya adui (Danieli 10:10-14). Ukubwa kamili wa vita vya kimalaika haujulikani kwetu, lakini hivi vidokezo vichache vinatosha kupendekeza kwamba vita vikali vya ulimwengu vinafanyika bila kuonekana.

4. Kumwadu Mungu. Malaika daima wamezunguka kiti cha enzi cha Mungu, wakiabudu na kupasa sauti za sifa Zake (Zaburi 148:1-2; Isaya 6:3; Waebrania 1:6; Ufunuo 5:8-13). Kwa kuwa malaika waliumbwa ili wamwabudu Mungu, wakikataa kusudi hilo ni jambo lisiloweza kusamehewa. Wakati Ibilisi, malaika mkuu, alikataa kumwabudu Mungu na badala yake na kusisitiza kuwa malaika wamwabudu yeye, Mungu alimtupa kutoka mbinguni (Isaya 14:12-18). Malaika walioshirikiana na Ibilisi walifukuzwa pamoja na yeye.

5. Kutumikia. Malaika wapo ili kutenda mapenzi ya Muumba wao. Wanaenda kwenye Mungu anawatuma, wanasema kile anawapa waseme, na kuwahudumia watoto wake duniani (Zaburi 103:20; Ufunuo 22:9; Waebrania 1:14). baada ya kujaribiwa kwa Yesu siku arobaini nyikani, malaika walikuja na kumhudumia (Mathayo 4:11). wakati wenye haki wanakufa, inaonekana kwamba malaika huwachukua moja kwa moja hadi mahali pa pumziko la Mungu (Luka 16:22).

6. Kutekeleza hukumu. Sio malaika wote huleta mung’ao na furaha. Vile vile wanatekeleza maagizo ya Mungu ya uharibifu. Kitabu cha Ufunuo kinatabiri matendo mengi ya kimalaika ambayo yataleta uharibifu wa mwisho wa ulimwengu (Ufunuo 7:1; 8-10). wakati Farao alikataa kuwaruhusu watu wa Mungu waondoke Misri, Mungu alimtuma malaika kumuua kila mzaliwa wa kwanza (Kutoka 12:12,23). malaika walihusika katika kifo cha Herode (Matendo 12:23) na adhabu kwa Yerusalemu (1 Mambo ya Nyakati 21:15).

7. Kusaidia katika kueneza Neno la Mungu. Waebrania 2:2 ikizungumzia juu ya Sheria ya Musa inauita ”ujumbe ulionenwa na malaika.” Kwa namna fulani, malaika walihusika kitika harakati ya Musa kupokea sheria katika mlima wa Sinai, ikifunua kusudi lingine la malaika.

Mungu hutumia malaika kwa njia yoyote anayochagua. Kwa sababu hatujui lolote kuhusu ulimwengu mbali na ulimwengu wetu wa halisi, hatuwezi kuelewa makusudi yote ambayo malaika hutimiza. Lakini Wakristo wana ujasiri kwamba malaika watakatifu wa Mungu wamesimama wakiwa tayari kulinda na kuwakomboa watoto wa Mungu wanaoweza kufa (Zaburi 91:11). Ingawa malaika ni viumbe walioumbwa, vile sisi tulivyoumbwa, na hawapaswi kamwe kuabudiwa, tunaweza kumshukuru Mungu kwa ajili yao na vile anawatumia kunufaisha maisha yetu kwa njia isiyoonekana.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kusudi la malaika ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries