settings icon
share icon
Swali

Je! Tunapaswa kusimama wakati Biblia inasomwa?

Jibu


Katika Nehemia 8: 5, kuhani Ezra aliwakusanya watu ambao walikuwa wamejenga upya ukuta wa Yerusalemu kwa minajili ya usomaji wa sheria ya Mungu: "Ezra akakifungua kile kitabu. Watu wote waliweza kumwona kwa sababu alikuwa amesimama juu zaidi, naye alipokifungua watu wote wakasimama." Makanisa mengine hii leo hufuata tamaduni hii na kufundisha kwamba tunapaswa kusimama wakati Neno la Mungu linaposomwa.

Kusimama ukusikiliza Biblia ikisomwa hakika ni ishara ya heshima. Walakini, hakuna amri ya kibiblia inayofundisha kwamba ni lazima watu wasimame wakati Maandiko yanasomwa. Kwa kweli, Ezra hakuwa anaisoma Biblia kanisani. Ezra alisoma kutoka kwa Torati, akiwa amesimama kwenye jukwaa la nje huko Yerusalemu katika hafla ya mara moja mamia ya miaka kabla ya kanisa kuanza (ona Matendo 2). Ingawa tunaweza kujifunza kanuni nyingi nzuri kutoka kwa kifungu hiki, hakuna amri ya wazi ya kutulazimisha kuwa turudie tendo hili wakati wa mikutano ya kanisa hii leo.

Fauka ya hayo, kusimama kulikofanyika katika Nehemia 8: 5 hakukudumu kwa muda mrefu. Mstari ufuatao unasema, "Ezra akamsifu Bwana, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, "Amen! Amen!" Kisha wakasujudu na kumwabudu Bwana hali nyuso zao zikigusa ardhi." (Nehemia 8: 6).

Mistari ya 7-8 inaongeza, "Watu wakiwa wamesimama pale, Walawi wafuatao waliwafunza ile Sheria… Walisoma kutoka kile Kitabu cha Sheria ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa." Wanaume hawa walisaidia katika kufafanua na pengine kutafsiri mafundisho ya Sheria kwa watu wa Yerusalemu.

Nehemia 8:12 inasema kwamba siku ile Ezra alipoyasoma Maandiko ilikuwa siku ya furaha: "Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa, na kupeana sehemu ya chakula, na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa walifahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa." Kama vile Zaburi 119: 162 inavyosema, "Nafurahia ahadi zako kama mtu aliyepata mateka mengi."

Kwa kusikiliza Neno la Mungu, Waisraeli walijifunza juu ya Sikukuu ya Vibanda. Walichagua kuisherehekea kwa mara ya kwanza tangu warudi Yerusalemu. Sikukuu hiyo ilidumu kwa siku saba, ikifuatiwa na siku kuu bila kufanya kazi yoyote.

Kama watu wa Yuda wakati wa siku za Ezra, tunapaswa kuonyesha heshima kwa Neno la Mungu kila wakati. Kusimama huku likisomwa ni njia moja ya kuonyesha heshima, lakini kuna njia zingine. Njia bora ya kuonyesha kuheshimu kwa Neno la Mungu ni kulitii na kuliruhusu libadilishe maisha yetu. " "Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi" (Zaburi 119: 11).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunapaswa kusimama wakati Biblia inasomwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries