settings icon
share icon
Swali

Je! Kusihi damu ya Yesu ni ya kibiblia?

Jibu


"Kusihi damu ya Yesu" katika sala ni mafundisho ambayo yanaweza kufuatiliwa kwa baadhi ya viongozi wa kwanza wa harakati ya Neno la Imani. Wakati watu wanazungumzia "kusihi damu ya Yesu katika sala" wanataja mazoezi ya "kudai" nguvu ya Kristo juu ya tatizo lolote na kila moja kwa kutumia maneno "Ninakiri damu ya Yesu juu ya _______."

"Kusihi damu ya Yesu" hauna msingi wowote katika Maandiko. Hakuna mtu yeyote katika Biblia aliwahi "kukiri damu" ya Kristo. Wale ambao "wanakiri damu" hufanya hivyo kama kuna kitu cha maajabu katika maneno hayo au kwa kuyatumia maombi yao kwa njia fulani yatakuwa na nguvu zaidi. Mafundisho haya yanazaliwa kutokana na mtazamo uliopotoka na uasi wa sala kwamba maombi sio kitu Zaidi kuliko njia ya kumfanya Mungu ili kupata kile tunachotaka badala ya kuomba kwa mapenzi Yake kufanyika. Harakati ya Neno la Imani nzima linatokana na mafundisho ya uwongo kwamba imani ni nguvu na ikiwa tutaomba kwa imani ya kutosha, basi Mungu anatuhakikishia afya, utajiri, na furaha na atatuokoa kutoka kwa kila tatizo na kila hali. Katika mtazamo huu, Mungu ni njia tu ya kupata kile tunachotaka badala ya kuwa Muumba mtakatifu, mwenye nguvu, mkamilifu na mwenye haki ambaye Biblia inafunua Yeye kuwa.

Wale wanaofundisha Neno hili la Imani la uwongo wana maoni ya kutukuza mtu na "haki" yetu ya kusihi kile tunachotaka na kumfanya Mungu kujibu jinsi tunavyotaka. Hii ni kinyume na imani halisi ya kibiblia iliyoonyeshwa katika maisha ya Paulo na mtazamo wake kwa mateso na majaribu. Paulo aliandika katika 2 Timotheo kwamba "wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa" (2 Timotheo 3:12). Lakini Neno la Imani inafundisha kwamba ikiwa tutateseka au kuwa wagonjwa au kupambana na dhambi, ni kwa sababu hatuna imani ya kutosha au kwamba hatusihi damu ya Yesu kutupa kile kilicho chetu kihalali. Lakini hatuoni Paulo akitetea damu ya Kristo au kudai kilichokuwa "chake kihalali" wakati alipokuwa anakabiliwa na majaribu na mateso. Badala yake tunaona imani yake thabiti katika Kristo bila kujali hali: "Kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile" (2 Timotheo 1:12).

Paulo alikuwa "amejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu"(Wafilipi 4:11-13). Imani ya Paulo ilikuwa ndani ya Kristo peke yake, na angeweza kusema kwa imani, "Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina"(2 Timotheo 4:18).

"Kusihi damu" kama ilivyo kawaida inafanana zaidi na mafundisho ya kumfikia Mungu kwa tafkira-kukariri virai vya ajabu na kutumaini itafanya kazi-kuliko ilivyofanya na sala ya kibiblia. Kusema maneno fulani hayafanyi maombi yetu nguvu Zaidi kwa kiajabu. Zaidi ya hayo, "kutetea damu" ya Kristo haihitajiki kumshinda Shetani. Tayari ameshindwa, na ikiwa tumezaliwa tena kwa kweli, Shetani hana nguvu juu yetu isipokuwa kile Mungu anaruhusu kwa kusudi Lake na utukufu. Wakolosai 1:13 imeweka hili waziwazi kabisa: "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi."

Badala ya "kusihi damu" ya Kristo kwa ajili ya ulinzi au nguvu, Wakristo wanapaswa kutii amri katika Yakobo 4:7, "Basi mtiini Mungu. Mpigeni Shetani, naye atawakimbia" Badala ya kufanya mfano wa maombi yasio ya kibiblia, tunapaswa kufuata maagizo rahisi ya maandiko-kuongoza maisha safi mbele ya Mungu, kuchukua mawazo yetu yote mateka ili kuepuka kupa dhambi nafasi, kukiri dhambi zetu tunaposhindwa maagizo hayo mawili ya kwanza, na kuvaa silaha kamili za Mungu kama ilivyoelezwa katika Waefeso 6:13-17.

Biblia inatupa maagizo mengi katika maisha ya kushinda katika Kristo, na kusihi "damu ya Yesu" sio moja yao. Tumeoshwa kwa damu ya Kristo, na Yeye ndiye Mkuhani wetu Mkuu na mpatanishi ambaye "yu hai siku zote ili atuombee" (Waebrania 7:25). Kama kondoo Wake tuko tayari chini ya ulinzi wake; tunahitaji tu kuishi kila siku kwa kumtumaini kwa kile ameahidi na kutoa tayari.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kusihi damu ya Yesu ni ya kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries