settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kushughulika na watu wenye kiburi?

Jibu


Sisi sote tunajua watu ambao tunapata ni wenye kiburi kwa njia moja au nyingine, na tunatakiwa kukabiliana na watu wenye kiburi kwa wakati mmoja au mwingine. Mtu mwenye kiburi anaweza kuwa mtu anayejishughulisha, anayepinga mashaka, mwenye chuki, mwenye ubinafsi, mwenye kukosa heshima, mwenye kusasirisha, au pia mwenye kiburi. Watu wenye kiburi wanaonekana kujua jinsi ya kutukasirisha, kuumiza hisia zetu, na kuchochea shida. Kushughulika na watu wenye shida huwa zoezi la uvumilivu, upendo, na neema.

Mitikio yetu kwa watu wenye kiburi inapaswa kuonyesha mifano iliyotolewa na Yesu, kwa hakika Yeye alihusika na watu wengi wenye kiburi wakati wake hapa duniani. Katika utangamano wake na watu wenye kiburi, Yesu hakuwahi kuonyesha mtazamo wa ukali au kiburi; badala yake, alionyesha mamlaka chini ya udhibiti. Aliwakemea alipolazimaka kufanya hivyo (Yohana 8:47), lakini pia alishughulika na watu wenye kiburi kwa kubaki kimya (Yohana 8: 6), akiuliza maswali (Marko 11: 28-29), akiwaelezea maandiko (Marko 10: 2- 3), na kuwaambia hadithi (Luka 7: 40-42).

Katika Mahubiri ya Mlimani, Yesu alikuwa wazi sana kuhusu kushughulika na watu wenye kiburi kwa upendo na unyenyekevu: "Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo."(Luka 6: 27-31). Petro wa Kwanza 3: 9 inasema, "Usilipize baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka."

Katika kukabiliana na watu wenye kiburi, tunapaswa kuepuka kiburi. Ni muhimu kukumbuka ushauri uliotolewa na mtume Paulo katika Warumi 12: 3: "Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani."(angalia pia Wafilipi 2: 3-4). Kwa hivyo, tunapojua kwamba tunapaswa kushughulika na mtu mwenye kiburi tunatatua hali hiyo kwa upole. Upendo pia ni muhimu: "Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe" (Wagalatia 5:14). Tunapaswa kuonyesha upendo wa Mungu kwa kila mtu-ikiwa ni pamoja na watu wenye kiburi.

Kitabu cha Mithali hutoa hekima nyingi katika kushughulika na watu wenye kiburi. Mithali 12:16 inalenga uvumilivu katika mahusiano yetu: "Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.''Mithali 20: 3 inasisitiza maamuzi ya amani: "Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana." Mithali 10:12 inahimiza upendo: "Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote."Mithali 17:14 huthamini mtazamo na ufafanuzi:"Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika." Kama inawezekana, inaweza kuwa bora kuepuka hali hiyo kabisa kwa kuchagua kwa uangalifu ambao tunashirikiana nao:"Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi"(Methali 22:24).

Hatuwezi kuepuka kabisa kushughulika na watu wenye kiburi. Tunapohusika na watu wenye kiburi, ni rahisi kujibu kimwili. Lakini hiyo huleta tu mabaya zaidi kwetu. Ni bora zaidi kuruhusu ushiriki wetu na watu wenye kiburi kuleta matunda ya Roho ndani yetu (Wagalatia 5: 22-23)! Kwa neema ya Mungu, tushirikiane na watu wenye kiburi katika upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili,uaminifu, upole, na juu ya yote ya kujizuia. Hebu tuendeleze upendo huo, neema, na rehema ambayo Mungu alitupatia. Na tupate kuwa makini kuwa "watu wenye kiburi" sisi wenyewe!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kushughulika na watu wenye kiburi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries