settings icon
share icon
Swali

Kushughulika na mama mkwe...?

Jibu


Mama mkwe ambaye anaingililia shughuli , na kudhibiti, na kuvuruga maisha ya mwanawe / binti yake na mkwewe na binti-mkwe ni kile ambacho Biblia inaita "busybody" (1 Timotheo 5) : 13). Maana ya neno la Kiyunani ambalo linalotafsiriwa "kujushughulisha" katika kifungu cha 1 Timotheo ina maana ya " aliyejiteua kuwa mwangalizi katika masuala ya wanadamu wengine." Kungililia shughuli za wengine ni baadhi ya mambo ambao mama-mkwe anahusika nayo, au angalau wanashutumiwa kufanya hivyo. Tabia hii inakadhaisha, inakera, na kinyume na mpango wa Mungu kwa familia.

Ni dhahiri kuwa mienendo katika hali kama hiyo ni ya kusisirisha. Mama-mkwe anaweza kufanya mambo haya kwa sababu hakuna mtu mwingine katika familia amabaye ameweka mipaka yake. Kwa hiyo, anakuwa mtu wa "kuvuruga." Labda yeye hata hatambui jinsi anavyoleta vurugu na kudhibiti. Kwake, inaweza tu kuwa "upendo." Ikiwa ndivyo ilivyo, labda majadiliano ya moyo kwa moyo yataweka mabo wazi. Ikiwa anaelewa anachofanya na anafanya kwa kusudi hata baada ya kuulizwa kuacha, basi hakuna kitu ambacho unaweza kufanya ili kubadilisha hayo.

Haijalishi ni upande gani wa familia unaoleta vurugu. Hii ni shambulio juu ya utakatifu wa ndoa na inakiuka "kuondoka na kuunganika" ambayo ni amri ya Mungu ya ndoa (Mwanzo 2: 23-24). Mwanamume na mwanamke huwaacha familia zao za kuzaliwa na kuanza familia mpya, na wanapaswa kupendana na kulindana. Mume ambaye anaruhusu mama yake au mkwewe kuingilia kati ndoa yake haishi kulingana na amri iliyotolewa kwa waume katika Waefeso 5: 25-33. Mipaka inapaswa kuwekwa na kisha kudumishwa bila kujali upinzani unaozuka. Ukweli ni kwamba watu hutufanyia njisi tunavyowaruhusu watutendee. Ikiwa tunawaruhusu kuharibu utakatifu wa familia yetu, basi ndivyo watakavyofanya. Hakuna mtu, hata katika familia yetu iliyopanuliwa, ana haki ya kuharibu au kuvuruga mambo ya nyumba yetu, na ni wajibu wa mume kulinda faragha. Anapaswa kuongoza kwa upole-lakini kwa uwazi-akielezea mama mkwewe kile anachokifanya ni kibaya na kumhakikishia kwamba tabia hiyo haiwezi kuvumiliwa. Anapaswa kumkumbusha kwamba Mungu amempa jukumu la familia yake na kuacha yoyote ya jukumu hilo kwake ni kuomtii Mungu. Anapaswa pia kumhakikishia kuwa yeye na mke wake bado wanampenda, lakini kwamba uhusiano umebadilika na yeye amechukua usukani sasa. Huo ni mpango wa Mungu kwa ajili ya familia, na ndivyo itakavyokuwa. Kisha wanandoa wanapaswa kusimama imara katika uamuzi wao.

Tunaweza kufanya nini kuhusu mama mkwe anayevuruga? Tunaweza kufanya uchaguzi tusimruhusu aondoe amani yetu ya akili. Hatuwezi kubadili jinsi wengine wanavyofanya, lakini jinsi tunavyoitikia tabia zao ni chaguo letu. Tunaweza kuruhusu vitendo vya watu wengine kutuadhiri, au tunaweza kuchagua kumpa Mungu na kumruhusu kutumia vitendo hivyo ili kutuimarisha kiroho. Ni majibu yetu wenyewe kwa aina hali ambayo huchochea kukasirika kwetu. Ni sisi tunaweza kuacha kujichocha kihisia kwa kutoruhusu vitendo vya mama mkwe kuingilia kati ya amani yetu. Tabia yake sio wajibu wetu; bali majibu yetu.

Wazazi na wakwe wa sheria wanapaswa kupatiwa heshima na upendo, lakini hatupaswi kuruhusu hisia zetu ziwe kikwazo. Njia bora ya kumfukuza adui ni kumfanya mshirika. Hii inafanyika kupitia neema ya Mungu. Wakristo wanaweza daima kutoa neema ya msamaha (Waefeso 4:32). Huenda isimfanye mama mkwe kuacha kuingilia kati, lakini itakuwa chanzo cha nguvu na amani cha kuegemea (Waefeso 6: 11-17). Mahali pekee ya kupata amani ya kweli ya moyo ni katika uhusiano wa kibinafsi na Mungu kupitia Kristo. Basi tunaweza tu kupumzika katika amani Yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kushughulika na mama mkwe...?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries