settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kurudi nyuma?

Jibu


Maneno kurudi nyuma, katika mazingira ya Kikristo, yana maana ya kuondoka mbali na Kristo badala ya kuenda kwake. Aliyerudi nyuma ni mtu ambaye anaenda njia mbaya, kiroho. Anadidimia badala ya kuendelea. Aliyerudi nyuma alikuwa kwa wakati mmoja ameonyesha kujitoa kwa Kristo au aliweka kiwango fulani cha tabia, lakini hajawahi rejea kwa njia za zamani. Kurudi nyuma kunaweza kujionyesha kwa njia kadhaa, k.m., kuacha kanisa, kupoteza juhudi katika Bwana, kutembea mbali na huduma au familia, au kurudi katika tabia za kale.

Watu wengine hutumia maneno kurudi nyuma kumaanisha kuwa mtu amepoteza wokovu wake. Hata hivyo, mtu aliyeokoka ako salama katika Kristo (Yohana 10: 28-29) — Mungu hatatupa watoto wake nje ya familia yake – hatutatumia maneno hayo hivyo. Badala yake, tunapozungumza juu ya kurudi nyuma, tunamaanisha kwamba mtu anazidi kuwa baridi katika Kristo. Hali ya kurudi nyuma iliyorejeshwa inaweza kuonyesha kwamba mtu hakuwahi kamwe kuokolewa ili aanze-katika hali hiyo, aliyerudi nyuma anaonyesha tu rangi zake za kweli. Lakini pia inawezekana kwa watoto wa Mungu kurudi nyuma, kwa muda.

Bibilia inatumia maneno kuanguka mbali badala ya kurudi nyuma, lakini wazo ni sawa. Katika Bibilia "kuanguka" inaweza kumaanisha mambo mawili tofauti. Katika mfano mmoja, mtu huyo anaokolewa lakini anapata muda wa kujiuliza maswali ambayo tunaweza kuiita "mgogoro wa imani." Kwa upande mwingine, mtu huyo hakuwahi kamwe kuokolewa lakini anajifanya tu kama mtu aliyeokolewa. Tutaita hii kuchukua Ukristo kama "gari la mtihani."

Mgogoro wa kurudi nyuma wa Imani:
Katika Marko 14:27 Yesu anawaambia wanafunzi wake, "Ninyi nyote mtaanguka." Alichomaanisha ni kwamba, wakati alipokamatwa, watapata shida ya imani, tukio la maisha la kushangaza ya kwamba watakimbia kutoka kwa Yesu na kuuliza msingi wa imani zao. Ilikuwa usiku wa kosa, usiku wa kuwakumbusha kwao. Lakini hii ilikuwa hali ya muda. Siku tatu baadaye, Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na akaonekana kwa wanafunzi. Imani na matumaini yao yalirejeshwa, imara zaidi kuliko hapo awali.

Mtume Paulo anatuambia jinsi ya kushughulika na mwamini mwezetu ambaye anarudi nyuma: "Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe"(Wagalatia 6: 1). Yakobo anakubaliana: "Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli. . . mtu anapaswa kumleta mtu huyo "(Yakobo 5:19). Aliyerudi nyuma ametembea kutoka mahali ambapo anapaswa kuwa na ana "kushikamana" katika dhambi, lakini kanisa litafanya kazi kumrejesha na kumrudisha katika njia ya haki.

Kuna matukio katika maisha, kama kifo cha mpendwa, ambacho kinaweza kutufanya tuulize Mungu. Hii ni sawa, ili mradi tuende kwa Mungu na maswali hayo badala ya kuyatumia kama sababu za kuishi katika uasi. Matokeo ya mgogoro wa imani ni mara nyingi kwamba tunamjua Mungu zaidi kwa karibu kuliko hapo awali. Wakati wa majaribio, tunapaswa kuingia ndani ya Neno, kuomba kwa uvumilivu (Luka 18: 1), na kuzungukwa na wale ambao imani yao ni imara.

Jaribio la kurudi nyuma:
Tunaona aina nyingine ya "kuanguka" katika Waebrania 6: 4-6 na Luka 8:13. Waebrania 6 inaelezea mpotofu, mtu ambaye "aliwahi onja tu uzuri wa neno" (mstari wa 5) na baadaye analikataa. Katika Luka 8:13 Yesu anafananisha upotofu na udongo wenye mwamba-baadhi ya watu huanguka au kurudi nyuma kwa sababu "hawana mizizi." Katika kila fungu hili, mtu huonekana kwa nje kuwa Mkristo, angalau kwa muda, lakini hajajitolea kwa Mungu. Mtu kama huyo anaweza kuhudhuria kanisa, kusoma Bibilia yake, kusikiliza muziki wa Kikristo, na kutembea na marafiki wakristo. Anapenda mazingira hayo yote mazuri na urafiki mzuri ambao kuwa karibu na Wakristo hutoa. Lakini moyo wake haujabadilika; yeye hajawahi kuzaliwa tena. Hatimaye, anarudi nyuma au kuanguka. Alikuwa amechukua Ukristo kama gari la mtihani na akaamua kuwa hakuwa anunue.

Wokovu huja kwa njia ya kukiri halisi wa Yesu kama Bwana kwa moyo unaoamini katika kifo cha Yesu na ufufuo (Warumi 10: 9-10). Ikiwa mtu aliyeokolewa ya kweli hurudi nyuma-yaani, anarudi tena katika mitazamo na tabia za kiroho za uharibifu-kurudi iyo nyuma itakuwa ya muda mfupi. Adhabu ya Bwana itamrudisha (angalia Waebrania 12: 4-13). Mchungaji Mzuri atamtafuta mwana-kondoo aliyepotea (Luka 15: 3-7).

Ikiwa mtu ambaye hakuwahi okolewa lakini anaweka tu kurudi nyuma ya uzuri-yaani, anaacha matone na kuonyesha rangi yake ya kweli-hali yake ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ya kwanza (Waebrania 10: 26-31). Tunawezaje kuwaambia aina moja ya kurudi nyuma kutoka kwa nyingine? Hatuwezi daima, isipokuwa tu kupewa wakati, na hata hivyo hatujui muda gani Mungu atachukua katika kurejesha aliyerudi nyuma. Mungu pekee ndiye anayeweza kuona moyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kurudi nyuma?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries