settings icon
share icon
Swali

Je! Kurithi nafsi kutoka kwa wazazi ina maana gani?

Jibu


Dhana ya kurithi nafsi kutoka kwa wazazi ina imani kwamba wakati wa utungaji mimba, mwili wa mtoto na nafsi au roho hupitishwa kwa mtoto kutoka kwa wazazi. Kwa maneno mengine, mtoto hurithi sehemu zote mbili za uhai wake, sehemu ya mwili na isiyo na mwili kutoka kwa wazazi wake.

Maoni tofauti ni imani ya uumbaji, ambayo inashikilia kuwa Mungu huumba nafsi mpya kutoka kwa utupu, kwa kila mtoto ambaye ametungwa. Dhana ya kurithi nafsi kutoka kwa wazazi na ile ya uumbaji zote zina uwezo na udhaifu, na zote zimeshikiliwa na wanatheolojia mbalimbali katika siku za nyuma. Kuna mtazamo wa tatu, ambao haujaungwa mkono na Biblia hata kamwe, ambao huanzisha nadharia kuwa Mungu aliumba nafsi zote za mwanadamu kwa wakati mmoja, kabla ya Adamu katika Mwanzo 1.

Wakati wa utungaji mimba, Mungu hushikanisha nafsi na mwili wa mtoto.

Wengine huonelea kuwa uungwaji mkono wa Biblia wa dhana ya kurithi kwa nafsi kutoka kwa wazazi upo katika simulizi ya uumbaji. Mwanzo 2:7 inasema kwamba “Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.” Hii inatufaahamisha kuwa Adamu hakuwa kiumbe kinachoonekana tu, mwenye mwili, lakini pia alikuwa na sehemu isiyo na mwili iliyoumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27)- alikuwa na roho na utu. Hukuna mahali Maandiko yamenakili kuwa Mungu anafanya hivi tena. Kwa hakika Mwanzo 2:2-3 inaonyesha kwamba Mungu alikamilisha kazi Yake ya uumbaji. Baadaye Adamu “alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi” (Mwanzo 5:3)-maneno hayo ni sawa na yale yaliyotumiwa wakati wa kuumbwa kwa Adamu kwenye Mwanzo 1:26. Na kama vile Adamu, Sethi alikuwa na mwili na nafsi.

Zaburi 51:5 inasema, “Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.” Kwanzia wakati wa utungaji mimba, Daudi alikuwa na asili ya dhambi. Kumbuka maneno mimi na mimi, yanaonyesha kuwa Daudi alijichukulia yeye mwenyewe kuwa mtu kamili (mwili na roho) katika utungaji. Dhana ya kurithi nafsi kutoka kwa waazi inasaidia kuelezea jinsi Daudi alipokea asili ya dhambi wakati waa utungaji mimba-roho yake/nafsi zilirithiwa kutoka kwa baba yake, ambaye pia alirithi roho/nafsi kutoka kwa baba yake, na kadhalika, hadi kwa Adamu mwenye dhambi.

Kifungu kingine kinachotumika kuunga mkono mtazamo wa kurithi kwa nafsi kutoka kwa wazazi ni Waebrania 7:9-10 ambacho kinasoma, “Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.” Lawi anachukuliwa kuwa “katika mwili” wa babu zake, hata kabla ya utungaji mimba. Katika njia hii, Lawi alitoa zaka kwa Melkizedeki kupitia kwa babu yake Abrahamu.

Ni rahisi kufuatisha nywele nyekundu au madoadoa katika ngozi kupitia mzazi mmoja au mwingine. Tabia za kimwili zinaweza kuruka kizazi, lakini hatimaye zitajitokeza. Ni hivyo hivyo kwa sifa za utu: “Oo, la, ana hasira kama yangu”; “Ana tabia kama ya baba yake”; “Ana upendo wa mama yake kwa wanyama.” Hakuna chembe ya urithi tunayoweza kutaja ambayo inaweza kufafanua nafsi, lakini kwa kawaida tunaona ushahidi wa utu uliorithiwa kutoka kwa wazazi. Je, hili linaweza kuwa matokeo ya wazazi kupitisha nafsi vile vile na mwili katika utungaji mimba? Maandiko hayathibitishi wala kukana dhana ya kurithi nafsi kutoka kwa wazazi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kurithi nafsi kutoka kwa wazazi ina maana gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries