settings icon
share icon
Swali

Ninawezaje kurejesha nafsi yangu?

Jibu


Kifungu cha pekee cha kibiblia kilicho na maneno haya ni Zaburi 23: 3: "Hunihuisha nafsi yangu..." Hii ni katika mazingira ya Mchungaji anayeongoza kondoo wake kwa "malisho ya kijani," "maji ya utulivu" na "njia za haki. " Kama Wakristo, sisi ni kondoo wa malisho ya Mungu (Zaburi 100: 3), na ni Yeye tu anayeweza kurejesha roho zetu. Kurejesha maana yake ni "kutengeneza, kurekebisha, au kurudi kwenye hali ya zamani." Roho ni sehemu ya kina sana kwetu, roho yetu ni sehemu ya ndani yetu. Kwa kuwa Mungu ndiye aliyetuumba, ndiye Yeye tu anaweza kutuwezesha, kwa sababu Yeye ndiye anayejua tu tunachohitaji kwa kweli ili kurejesha nafsi zetu.

Mungu ametupa majibu kuhusu kurejesha nafsi zetu katika Biblia-Neno la Mungu (2 Timotheo 3: 16-17), na lina majibu na hekima ya kukabiliana na kila kitu kitakachotukabili. Linaweza kutufanya kuwa na hekima kwa wokovu (2 Timotheo 3:15), kutumika kututia moyo wakati tuko na moyo wenye kukata tamaa (2 Wakorintho 1: 3), na kuwa mwongozo wetu kwa maisha ya amani na kuridhika (Zaburi 119: 97- 105). Ingawa kuna aina zote za vitabu zilizoandikwa na wanadamu kutoa hekima ya kidunia, Neno la Mungu pekee ndilo lina uwezo wa kurejesha roho na kutoa matumaini wakati wa shida.

Kwa kweli, kurejesha nafsi inawezekana tu kwa wale ambao roho zao zimekombolewa kupitia imani katika Kristo. Yesu aliahidi mapumziko kwa wale wote watakaokuja kwake (Mathayo 11: 28-30), kwa hiyo ni muhimu kuwa tuna uhakika wa wokovu wetu na uhusiano wetu na Mungu. Ni wale tu waliozaliwa tena katika Kristo wanaweza kupata amani na furaha ambayo Mungu ameahidi katika Neno Lake.

cha muimu, Mungu ameshatupatia kile tunachohitaji wakati tunapokabiliwa na kukata tamaa, magumu na majaribu. Amewapa vyanzo vitatu vya msingi vya faraja na nguvu. Kwanza, ametupatia Neno Lake kutuongoza, kututia moyo na kutulea kiroho. Tunapaswa kutumia wakati kukiisoma neno, kulisikiza likihubiriwa (Waroma 10:17) na zaidi ya yote kulitii (Zaburi 119: 2, Mithali 3: 1-2; Yakobo 1:25). Pili, Mungu ametupa fursa na nguvu ya sala (Mathayo 7: 7-11, Marko 11: 24-25, Yohana 15: 7; Waebrania 4:16, 1 Yohana 5:14). Tunahitaji kuchukua matatizo yetu, kukata tamaa kwetu na uchovu wetu kwa Mungu katika sala, kujua kwamba anatupenda na anatujali (1 Petro 5: 6-7). Tatu, ametupa Wakristo wengine ili kututia moyo na kutuunga mkono (Mhubiri 4: 9-19, Waefeso 4:29; Waebrania 3:13). Ni muhimu kuwa sehemu ya kanisa lenye afya, lenye usawa na kuabudu mara kwa mara na ushirika na waumini wengine (Waebrania 10: 23-25). Wakristo ambao wamekwenda katika mapambano kama hayo wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuhimiza na kusaidia wakati tunapopitia wakati mgumu (2 Wakorintho 1: 3-4).

Kuvunjika moyo wakati wa shida na dhiki sio kawaida. Katika Biblia tunaona mifano ya wanaume na wanawake wa Mungu ambao wamekabiliwa na hali kama hiyo. Mifano hizi zinaweza kututia moyo hii leo, kwa sababu Mungu mmoja aliyekuwa mwaminifu kwao basi atakuwa mwaminifu kwetu hii leo. Ni muhimu kuanza kwa kusoma Zaburi kwa sababu Mfalme Daudi aliandika mengi ya haya wakati wa giza katika maisha yake, na zinaweza kututumika kututia moyo wakati tunapofadhaika, uchovu na kukata tamaa. Kwa sababu Daudi alikuwa amepata furaha ya roho iliyorejeshwa na Mungu, angeweza kuandika maneno mazuri ya Zaburi ya 23: "Hunihuisha nafsi yangu."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kurejesha nafsi yangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries