settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu anarejesha ofisi za mtume na nabii katika kanisa leo?

Jibu


Harakati ya kurejesha ofisi ya mtume na nabii huweka madai yao kwamba mitume na manabii watakuwa sehemu ya kanisa katika Waefeso 4: 11-12, "Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na walimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe."

Wakati wa kanisa la karne ya kwanza, kulikuwa na ofisi ya mtume, na kulikuwa na kipawa cha kiroho cha utume. Ofisi au cheo cha mtume kilikuwa kimeshikiliwa na wanafunzi 12 wa Yesu pamoja na Mathiya, ambaye alichukua nafasi ya Yuda, na Paulo. Mitume walichaguliwa hasa na Kristo (Marko 3: 16-19). Uchaguzi wa ubadili wa Yuda unaonekana katika Matendo 1: 20-26. Kumbuka katika kifungu hiki nafasi ya Yuda inaitwa "ofisi." Pia inapaswa kukumbukwa kwamba Paulo alichaguliwa na Kristo (1 Wakorintho 15: 8-9; Wagalatia 1: 1; 2: 6-9). Wanaume hawa walipewa kazi ya kuweka msingi wa kanisa la ulimwengu (Waefeso 2:20). Msingi wa kanisa la ulimwengu uliwekwa katika karne ya kwanza. Hii ndiyo sababu ofisi ya mtume haitumiki tena. Mara tu msingi ukiwekwa, hatuhitaji tena wawekaji msingi.

Pia kulikuwa na kipawa cha kiroho cha utume (hii haipaswi kuchanganyikiwa na ofisi — ni tofauti). Baadhi ya wale waliokuwa na kipawa cha kiroho walikuwa Yakobo (1 Wakorintho 15: 7; Wagalatia 1:19), Barnaba (Matendo 14: 4, 14, 1 Wakorintho 9: 6), Androniko na Yunia (Warumi 16: 7), labda Sila na Timotheo (1 Wathesalonike 1: 1; 2: 7), na Apolo (1 Wakorintho 4: 6, 9). Hiki kikundi cha mwisho kilikuwa na kipawa cha utume lakini sio "ofisi" ya utume iliyotunukiwa wale kumi na wawili na Paulo. Wale ambao walikuwa na kipawa cha utume, basi, walikuwa wale waliobeba ujumbe wa injili na mamlaka ya Mungu. Neno mtume lina maana "mtu aliyetumwa kama mjumbe mwenye mamlaka." Hiyo ilikuwa kweli kwa wale walioshikilia ofisi ya mtume (kama Paulo) na wale waliokuwa na kipawa cha kiroho (kama Apolo). Ingawa kuna watu kama hao leo, wanaume ambao wametumwa na Mungu kueneza injili, ni bora tusiwaite kama mitume kwa sababu ya mchanganyiko inasababisha. Wengi hawajui matumizi mbili tofauti ya neno mtume.

Kipawa cha unabii pia kilikuwa kipawa cha muda mfupi kilichotolewa na Kristo kwa kuweka msingi wa kanisa la ulimwengu (Waefeso 2:20). Nabii alitangaza ujumbe kutoka kwa Bwana kwa waumini katika karne ya kwanza. Waumini hawa hawakuwa na faida tunayo leo ya kuwa na Biblia kamili. Kitabu cha mwisho cha Agano Jipya (Ufunuo) hakikumalizika hadi mwishoni mwa karne ya kwanza. Kwa hivyo Bwana aliwapa wanaume wenye vipawa walioitwa manabii ambao walitangaza ujumbe kutoka kwa Mungu mpaka hadi sheria ya Maandiko ilikuwa kamili.

Inapaswa kukumbukwa kwamba mafundisho ya sasa ya kurejeshwa kwa manabii na mitume ni mbali na yale Maandiko yanavyoeleza juu ya wanaume walioshikilia kipawa cha unabii na ofisi ya mtume. Wale wanaofundisha urejesho huo hufundisha kuwa mitume na manabii hawapaswi kamwe kuzungumzwa dhidi yao au hata kuulizwa swali, kwa sababu kuzungumza dhidi yao ni kusema dhidi ya Mungu. Hata hivyo, Mtume Paulo aliwamuru watu wa Beroya kwa kuchunguza kile alichosema dhidi ya Neno la Mungu ili kuhakikisha kwamba alisema ukweli (Matendo 17: 10-11). Mtume Paulo pia aliwaambia wale walio Galatia kuwa ikiwa mtu yeyote, pamoja na yeye mwenyewe, anapaswa kufundisha injili nyingine, mtu huyo lazima "alaaniwe" (Wagalatia 1: 8-9). Katika kila kitu, Paulo aliwaelekeza watu kwa Biblia kama mamlaka ya mwisho. Wanaume wanaodai kuwa mitume na manabii leo hujifanya kuwa mamlaka ya mwisho, kitu ambacho Paulo na wale kumi na wawili hawakufanya.

Pia inapaswa kukumbukwa kwamba Maandiko yanataja mitume na manabii kwa wakati uliopita. 2 Petro 3: 2 na Yuda 3-4 inasema kwamba watu hawapaswi kupotea kutoka kwa ujumbe ambao mitume walitoa (wakati uliopita). Waebrania 2: 3-4 pia huzungumzia kwa wakati uliopita kwa yale waliyofanya (zamani) "ishara, maajabu, na miujiza mbalimbali" kupitia kipawa cha Roho Mtakatifu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu anarejesha ofisi za mtume na nabii katika kanisa leo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries