settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kupoteza mimba?

Jibu


Labda swali la kawaida zaidi watu huuliza baada ya kupoteza mimba ni "Kwa nini hii ilitokea?" Au "Kwa nini Mungu alinifanyia hivyo?" Hakuna majibu rahisi kwa maswali haya. Hakika, hakuna hitimisho lenye kuridhisha katika kuelezea kwanini mambo mabaya yanafanyika kwa watu, hasa watoto wasio na hatia ambao hawajaanza kuishi. Lazima tuelewe kwamba Mungu haondoi wapendwa wetu kama adhabu ya kikatili. Biblia inatuambia kwamba "hakuna hukumu kwa wale walio katika Kristo Yesu" (Warumi 8: 1).

Kupoteza mimba husababishwa na mifumo isiyo ya kawaida ya kromosomu katika fetusi(fetus). Wakati hitilafu hii inaonekana, ukuaji unahitimishwa na basi kusababisha kupoteza mimba hiyo. Katika matukio mengine, kupeteza mimba kunasababishwa na uharibifu wa uterini, uharibifu wa homoni, matatizo ya mfumo wa kinga, maambukizi ya muda mrefu, na magonjwa. Baada ya maelfu ya miaka ya dhambi, kifo na uharibifu wa kibinafsi, haipaswi kutushangaza kwamba matatizo ya maumbile hatimaye yatakuwa kawaida.

Biblia haina maoni mahususi kuhusu kupozeza mimba. Tunaweza kuwa na hakika, hata hivyo, kwamba Mungu ana huruma kwa wale ambao wameteseka kwa njia ya kupoteza mima. Analia na kuteseka na sisi, kwa sababu tu anatupenda na anahisi maumivu yetu. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, aliahidi kutuma Roho Wake kwa waamini wote ili tusipitie majaribio peke yetu (Yohana 14:16). Yesu alisema katika Mathayo 28:20, "Na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."

Mwamini yeyote ambaye ameteseka kupitia kupoteza mimba lazima awe na imani katika tumaini lenye utukufu kuwa siku moja ataona mtoto wake tena. Mtoto aliyezaliwa sio fetusi au "kipande cha tishu" kwa Mungu, lakini ni mmoja wa watoto Wake. Yeremia 1: 5 inasema kwamba Mungu anatujua tunapokuwa tumboni. Maombolezo 3:33 inatuambia kwamba Mungu "hafurahi watu wanapoteseka au hapendi kuwahuzunisha." Yesu aliahidi kutuacha na zawadi ya amani tofauti na aina yoyote ambayo dunia inaweza kutoa (Yohana 14:27).

Warumi 11:36 inatukumbusha kwamba kila kitu kiko kwa nguvu za Mungu na ni kwa ajili ya utukufu Wake. Ingawa Yeye hatatuletea mateso kwa adhabu, ataruhusu mambo kuingia katika maisha yetu ambayo tunaweza kutumia kumletea utukufu. Yesu akasema, "Hayo Nimewaambieni mpate kuwa na amani nadni yangu. Ulimwengu mnayo dhiki; lakini jipeni moyo ; kwa kuwa nimeushinda ulimwengu "(Yohana 16:33).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kupoteza mimba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries